Nimeibiwa kuku wa nyama

Ulivyo andika tu inaonesha hauko serious tunaona kama una tania tu hii habari
 
Kwanini uliwakubalia wao ndiyo wakamate kuku ?....na kama picha zao unazo unaweza kuwa saka tu ..tatizo ushahidi watakuambia wewe muongo wao wamechukua kuku kamili ...swala la wizi wa hivyo mimi nilijua limekwisha maana siku hizi wafugaji wote wanajua huo wizi ....kuna kipindi zamani walijaribu kuiba kuku kwa njia hiyo nyumbani tuliwabana jinsi ya kuchukua kuku ...wakaanza kusema kama atutaki wawakamate wenyewe bandani basi ..wakaondoka walikuwa ni wezi.
 
Wewe upo sahihi ...ukiwabana wanajidai kuchukia
 
Mungu wa Israel...ila kwa maelezo ya ndugu yetu ni kwamba wezi wake ni wastaarabu..wamekuja kukagua kwanza,kisha wakaahidi kurudi na tenga,kosa naloona hapa ni kuleta pickup
Kweli wa Israel, maana hao Waua YESU KRISTO wanayoyafanya ni Mungu wao tu anaweza kuwasaidia!
 
Pole, sana nimesoma tena na tena nahisi upo kwenye mfadhaiko na maumivu makali. Pole sana rafiki wametumia ushirikina hao watu.
Hakuna ushirikina Wala dawa. Ni mzembe wa Hali ya juu na hajui kufanya biashara. Utawaamini vipi watu usiowajua
 
Pole sana dada katoe taarifa polisi upate RB kwa hizo picha ulizowekwa hapo ni rahisi sana kuwapata
Nakumbuka miaka 26 iliyopita wapo walionijaribu na noti bandia na hawakutoboa
Hakuna kesi hapo. Sababu walilipa kuku 60 na hao wengine ushahidi uko wapi kuwa walichukua wao. Hizo picha aliwapiga wakati wanachukua akiwa nao
 
Au upo China maan huko ndio ilikuwa Asubuh huku ilikuwa bado usiku wa saa 9
 
Mwezi wa 10 tar 12 na nilipanga mwezi wa 11 nikatoe sadaka kwa watoto but still nitapeleka asilimia kadhaa
Wewe ni mzembe sana na rahisi kutapeliwa. Unachukua pesa unawapelekea wachungaji maombi. Wahi kitengo Cha tiba ya akili usiendelee kusumbua watu, kumbe wewe ndiyo tatizo
 
Hujaeleweka. Funguka vzr wameibaje
 
Pole sana dada katoe taarifa polisi upate RB kwa hizo picha ulizowekwa hapo ni rahisi sana kuwapata
Nakumbuka miaka 26 iliyopita wapo walionijaribu na noti bandia na hawakutoboa
Hii kesi hashindi wala asihangaike na polisi, labda atumie njia nyingine kulipa kisasi.
 
Asanteni πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½

Yan total waliyoniibia ni kuku 208
208x6500=1,352,000
Kiulainiiii kmmm


Yan wale wanatumia dawa plus kukuzubaisha kila mtu anakuongelesha huyu anakushauri hivi huyu hivi yani maneno mengi
Wanakuchanganya wakati wa kuhesabu, wewe unatakiwa kukaa mlangoni akishachagua wewe unahesabu unampa wa nje akapakie kwenye tenga / gari.

Wanachofanya anaweza kukwambia nabeba kushoto wanne na kulia wanne kumbe amebeba watano au sita kwa wakati mmoja sasa kama wewe umemwamini inakula kwako.

Kitu najiuliza hiyo picha inaonekana kama camera ya simu na sio cctv camera.

Je ulikosa uaminifu mapema ukawapiga ai ilikuwaje hadi kuwachukua picha?
 
Hizo picha uliwa pigaje au ulizipata wapi? Pia naomba kujua kama nani aliwaconnect na wewe ili uanze nae cha Mwisho tuliza kichwa nenda kituo cha police karipoti
 
Hii kesi hashindi wala asihangaike na polisi, labda atumie njia nyingine kulipa kisasi.
Ogopa Mungu na tekinolojia
Hakuna kesi hapo. Sababu walilipa kuku 60 na hao wengine ushahidi uko wapi kuwa walichukua wao. Hizo picha aliwapiga wakati wanachukua akiwa nao
Akiwakamata wanafungwa kufundisha kupata ushahidi hapa ni kufunza uhalifu, sio kila kitu husemwa
 
Ogopa Mungu na tekinolojia

Akiwakamata wanafungwa kufundisha kupata ushahidi hapa ni kufunza uhalifu, sio kila kitu husemwa
Watafungwa Kwa ushahidi upi wakati walilipia kuku 60, hao wengine ana ushahidi gani kama wao ndiyo waliiba. Jiulize
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…