nasisitiza tuanze kuwa tunatumia akili zetu zifanye kazi . kuna utapeli mwingine wa kizembe sana tena sana. unapoambiwa biashara nawe ni msomi au mtoto wa mjini hebu tikisa kichwa kidogo ubongo ushtuke ikiwa ulikuwa umelala kwa muda mrefu. linganisha bei ya hicho kitu na anayokuuzia muuzaji tena ameweka kwenye mtandao hujiulizi huyu mtu kwa bei hii alikuwa na bidhaa ngapi? na tangazo smetme limekaa siku 2 hujiulizi kuwa ina maana wenzio hawalioni? but pia bei halisi na ya kuuzia ziwe na uhusiano kiasi flan hata kama ni za deal kuna kiwango unless otherwise uwe hujui kabisa bei ya hicho kitu. ni sawa na leo mtu anakuja kukwambia anauza gari yake toyota rav namba c model letsa say ya 2010 kwa tsh mil Moja. ukimuuliza anakwambia anashida sana na pesa. picha anakutumia gari bado ipo safi kabisa. then anakwambia mtumie advance ili mtu mwingine asije akaichukua nawe unamtumia pesa una akili wewe?
halafu unakuja hapa utuambie tukutafutie huyo mtu? anyway nimependa kuwa mhusika umekuwa jasiri na kuweka suala hili wazi wengine wametapeliwa wameshindwa hata kuwaelimisha wenzao. wewe Ubarikiwe kwa kuwa umeamua kuielimisha jamii hii inayopenda vitu vya utelezi,vitu vya deal n.k
huyo tapeli namtaka nimwoneshe sisi wengine tulianza utapel toka siku ya kuzaliwa. yeye utapeli wake kajifunzia tu ukubwani.