Nimeibiwa, nitamkamataje huyu mtu!?

Nimeibiwa, nitamkamataje huyu mtu!?

wp_ss_20160315_0002.png
 

Attachments

  • wp_ss_20160315_0001.png
    wp_ss_20160315_0001.png
    18.9 KB · Views: 51
Nimefanya screen short muweze jionea jinsi majibizano na mr mhagama yalivyokua
 
Mkuu samahani kusema hivi lakini umeibiwa kizembe sana.Ungefuatilia tu post zake za nyuma na kama kweli wewe ni mtumiaji sana wa Kupatana ungestukia mchezo mapema

Kupatana wenyewe washasema do not pay in advance

Atawaibia wengi basi huyo jembe wa Iringa
 
Karipoti polisi mkuu...hamalizi wiki huyo wanamkamata...siku hizi kuna kitengo cha cyber crime wako vizuri balaaaa. Mi nilibiwa iphone 6, kuna kifaaa wanacho polisi kina lokate popote ulipo...mwizi wangu alikutwa bar na simu
Ulifanyafanyaje mkuu,maana mara nyingi polisi huwa hawatoi ushirikiano kabisa.
 
kumkamata huyo jamaa inabidi apatikane mtu ajifanye kapenda bidhaa zake na anataka kununua alaf awe anaishi hukohuko ludewa ili amseti wakutane wamkamate.
haha mkuu mtu kama huyo wala haishi ludewa unakuta yuko hapa hapa dar...
 
Siku ambayo mtatia mikononi wakati wa kum mimina tafadhali naomba munijulishe wadau nimuandalie ky mbili zile za 250gm akione cha moto haina haja ya kumpeleka polisi huyo ni kumf******R* mwanzo mwisho ***** zake huyo
Unawezakuta ni mzoefu atafurahije
 
Mkuu nimeona kama icho kitambulisho ni cha jeshi la zimamoto na ukoaji na sio la polisi mkuu.
Pole kwa yaliyokukuta mkuu.
Hili jeshi linatakiwa lithibitishe kama ni mfanyakazi wake au la, kwa kuwa anaharibu picha ya Kamishna wa Zimamoto. Au Jeshi la Zimamoto wasaidie upatikanaji wa huyu jamaa ila kujenga taswira zuri kwa jamii.
 
Nimefanya screen short muweze jionea jinsi majibizano na mr mhagama yalivyokua
Mkuu nime Kupm Huyu! Tatizo la huyu jamaa hivyo vitu so hata mtu akatokea amependa bidhaa ake na akataka kuonana nae haitawezekana hata kubali atataka kuonana nae ili amuoneshe nini hasa lakini kama tuna Email ake na Namba zake za simu tunashindwaje kumkamata na Sahizi Polisi wanavyo Penda sifa! Huyu tutamkamata Tuu sema watu hapa watoe ushirikiano tujue tunafanyaje!
 
Huyu mwana alimpiga dogo langu laki 5 sasa..Na huyu jamaa nimemfuatilia sana pessa anatolea DSM place N hide huyu jamaa soon ntamkamata
 
Amekuingiza mjini......Ungeshirikisha akili zako ungemstukia tu.
Bila shaka anatumia jina na kitambulisho cha mtu mwingine kufanya uhalifu.
Kitambulisho kitakua bandia cha kugushi,mbona vinatengenezwa sana tu?
 
Mkuu ni bora iwe cash kama unauza kitu. Na kama unanunua usikubali kutoa hela kabla hujauona mzigo.

Huyu jamaa inaonekana ni mtu wa tamaa sana.
Mcbook for $100??? Be serious !!
Wakati macbook used USA ni $350-800 na sio TZ ! !huyu jamaa hastahili kupewa pole akome
 
Ila sometime nasi tuwe tuna reason jaman. Kutapeliwa ni ukosefu wa ku reason tu kitu cha Mil 2 wewe unauziwa lakh 2 hujiulizi hata kidogo? Sasa akili zetu tunafanyia nini? Kutongozea mademu?
 
Hao kupatana nao watakuwa hovyo kama watu wanatumia mtandao wao kwa utapeli
 
Hao kupatana nao watakuwa hovyo kama watu wanatumia mtandao wao kwa utapeli
Tena watakuwa jipu kama agent wanatakiwa kubaini nani mwenye bidhaa na ni nani ni tapeli ili kuongeza imani kwa wateja wao. Mbona ebay watu wanafanya biashara vizuri tena kutoka mbali na unapata bidhaa yako kamili
 
nasisitiza tuanze kuwa tunatumia akili zetu zifanye kazi . kuna utapeli mwingine wa kizembe sana tena sana. unapoambiwa biashara nawe ni msomi au mtoto wa mjini hebu tikisa kichwa kidogo ubongo ushtuke ikiwa ulikuwa umelala kwa muda mrefu. linganisha bei ya hicho kitu na anayokuuzia muuzaji tena ameweka kwenye mtandao hujiulizi huyu mtu kwa bei hii alikuwa na bidhaa ngapi? na tangazo smetme limekaa siku 2 hujiulizi kuwa ina maana wenzio hawalioni? but pia bei halisi na ya kuuzia ziwe na uhusiano kiasi flan hata kama ni za deal kuna kiwango unless otherwise uwe hujui kabisa bei ya hicho kitu. ni sawa na leo mtu anakuja kukwambia anauza gari yake toyota rav namba c model letsa say ya 2010 kwa tsh mil Moja. ukimuuliza anakwambia anashida sana na pesa. picha anakutumia gari bado ipo safi kabisa. then anakwambia mtumie advance ili mtu mwingine asije akaichukua nawe unamtumia pesa una akili wewe?

halafu unakuja hapa utuambie tukutafutie huyo mtu? anyway nimependa kuwa mhusika umekuwa jasiri na kuweka suala hili wazi wengine wametapeliwa wameshindwa hata kuwaelimisha wenzao. wewe Ubarikiwe kwa kuwa umeamua kuielimisha jamii hii inayopenda vitu vya utelezi,vitu vya deal n.k

huyo tapeli namtaka nimwoneshe sisi wengine tulianza utapel toka siku ya kuzaliwa. yeye utapeli wake kajifunzia tu ukubwani.
 
Back
Top Bottom