Nimeibiwa simu na mwizi ametoa pesa tiGO Pesa!

Nimeibiwa simu na mwizi ametoa pesa tiGO Pesa!

Pole sana ila mbona tigo kwenye swala la ulinzi wa pesa wapo vizuri matatizo yapo Kwa Vodacom na airtel
 
Ni Rahisi sana mtu akiweza kupata NIDA yako.Tigo wana huduma ya Kuweka Upya PIN kwa kutumia NIDA namba ambayo maswali yake wakala wao wa usajili anaweza kujibu na kufyatua Password yako Fasta.Nashauri TIGO waondoe hiyo huduma
aise kilichonifurahisha ni signature yako hii ya kuhusu maarifa na pia kujua kuwa hujui ndio kujua kwenyewe
 
hebu tufafanulie kidogo maana ya PIN
Kuna kipindi serikali ilizitaka kampuni za simu kuweka PIN kwenye laini ili kulinda wateja,mfano ukinunua laini mpya inakuwa tayari na PIN,unabadilisha unaweka ya kwako,hiyo inakusaidia pale unapoibiwa simu au laini,mtu akitaka kuweka hiyo laini yako kwenye simu nyingine au kama simu yako ikazima, inamlazimu kuweka PIN ya laini...hii inazuia mwizi au mtu asiyehusika kutumia laini yako kama ukiibiwa au kupoteza bahati mbaya.... Halotel wanayo huduma hii kwenye laini zao mpya,ila Tigo na Vodacom bado laini zao hazina hiyo option.
 
Huwa wanaenda kwa Mawakala. Wale wana connection na wafanyakazi wa tigo. Anapewa number ya siri ya mteja mzigo unapigw
Inawezekana asee, na inawezekana pia hao mawakala huwa wanapata mgao.....

Make mi nlikuaga najiuliza anapataje hizo password anaiba tu mahela ya watu, ila raia wenye hasira kali siku moja walimuotea wakamrestisha.
 
Kuna kipindi serikali ilizitaka kampuni za simu kuweka PIN kwenye laini ili kulinda wateja,mfano ukinunua laini mpya inakuwa tayari na PIN,unabadilisha unaweka ya kwako,hiyo inakusaidia pale unapoibiwa simu au laini,mtu akitaka kuweka hiyo laini yako kwenye simu nyingine au kama simu yako ikazima, inamlazimu kuweka PIN ya laini...hii inazuia mwizi au mtu asiyehusika kutumia laini yako kama ukiibiwa au kupoteza bahati mbaya.... Halotel wanayo huduma hii kwenye laini zao mpya,ila Tigo na Vodacom bado laini zao hazina hiyo option.
Mitandao yote IPO hiyo huduma ila ni optional..unaweza Kuweka au kuacha..
 
Kuna baadhi ya nchi ni Kosa kisheria kutokuweka Number za siri kwenye simu yako na Simcard..kabla ya kulaumu tigo,why laini yako haina PIN??usalama unaanza na wewe...tofauti na kuibiwa ipo siku laini yako itatumika vibaya.

Umekumbusha jambo la msingi wengi PIN hatuweki, hapa nimejaribu kuturn on inaanidai PIN ya mwanzo ambayo hata siikumbuki!
 
Back
Top Bottom