Nimeibiwa simu na mwizi ametoa pesa tiGO Pesa!

Nimeibiwa simu na mwizi ametoa pesa tiGO Pesa!

Bora tigo mimi ukinipa lain ya eatel yoyote na usinipe nida wala pin yako ya eatel money kama unapesa humo naitoa safi kabisa bila kusumbuka na hata ukienda polis watakwambia umetoa mwenyewe kiufupi kampun zetu za simu haziko security sana kwa wajanja
Ebwana we hio ikoje uwezaje
 
Ukiwa na namba ya simu wale mawakala wa kusajili laini wanaweza kukutajia namba ya nida. Yani kimantiki wewe ulichelewa kuchukua maamuzi ya kulinda laini baada ya kuibiwa. Bila shaka hapo baada ya kuiba mwizi alitaguta wakala akapata namba ya nida na detail zako kisha akafanya process ya kutengeneza password mpya na kutoa hela baadae. Scenario kama hii ni rahisi kufanikiwa
Nilishituka sina simu baada ya muda kama saa moja
 
Kuna kibaka mmoja, alikua akiiba tu simu cha kwanza ni kutoa hela iwe tigo iwe voda cha kwanza anafanya muamala.....

Sijui hata ni akili gani zinatumika.
Kuna jamaa alikuja south kwa kukimbia kesi ya wizi wa mitandao anasema Magomeni yeye alikuwa ananunua line baada ya vibaka kuiba simu line wanamuuzia yeye anatoa pesa au kama haina pesa anaomba kutumiwa pesa na ndugu sometimes no sometimes yes
 
Hiyo mbona rahisi sana Cha kwanza anatoa line kama simu yako Ina password,anajipigia ,
Akishapata namba yako anaenda Kwa wakala wale wasajiri Laini anajifanya amesahau namba NIDA yake ,wale akiwapa namba yako tu wakicheki kwenye vile vifamoko vyao NIDA yako hiyo chap inakuja na majina yako yote matatu,

Baadae ya hapo anapigia tu Customer care na kuwaambia amesahau password yake ,wao wanachoomba ni namba za NIDA ,majina matatu na mwaka wa kuzaliwa ambao ni tayari upo Kwa namba ya NIDA yako ,
Baadae ya hapo anabadilishiwa password ye anaenda kutoa pesa yako Kwa Raha mustareheee.


Hiyo process yote kwa mwizi mzoefu haizidi ata Nusu saa .

Nb
Ukipotelewa na simu pigia customer care mapema wablock line yako kuepuka mambo kama hizi.
Kweli ila iyo inafanyika kwa hela ambazo ni kawaida wanaangalia ila laini ikiwa kuanzaia laki 3 na kuendelea wanakwambia tembelea dukani kwetu kwa msaada zaid
 
Nimeona koment nyingi sana humu kuwalaumu tigo saiv attacker ni wengi mno wana tumia tool za cybersecurity ku generate password na akifungua simu yako anaanza kutest kuanzia email nk akifanikiwa kuona zimekubal ujue umekwisha..
Watu wengi hufanya password za mfanono sana ko mtu ambae ana utaalamu mkubwa ni rahis sana kutumia software mbali mbali kutest na kupata nywira zako

makosa yapo kwako ungetoa taarifa mapema now day dunia ipo kweny technology ukichangany umekwisha kaka..

Pole kwanza piga moyo konde jipange upya
Asante. Wacha nibaki. na traditional banking na cryptocurrency. Ila Tigo wanirudishie pesa zangu. Siwaachi ng'oo.
 
mtu akishajua nida no yako tu zmekwishwaaa,,,,ipo hivi hao majambazi wanakuwa lao moja na hawa wanaosajili line...hatua ya kwanza wanayofanya hao majambazi ni kucheck nida no yako kwa kupitia no zako za simu hii huduma wanayo mawakala wote wanaosajili line mtaani...wakishaijua nida no yako wanainote pembeni...hiyo nida no yako ina kila kitu chako ambapo ni tarehe ya kuzaliwa mwezi na mwaka na itakuja na majina yako yote matatu...hatua inayofuatia ni wanapiga customercare ambapo atajitambulisha kama mhusika wa line na amesahau no ya siri....customercare watamwuliza majina matatu na tarehe aliyozaliwa atajibu so coz tayari anavyo kupitia nida no yako....wanaweza muuliza balance na akasema hakumbuki ...ila watamfungulia kwa kumsetia defult jambazi ataingiza pin mpya anazozijua yy.pia wengine wana acces toka jikoni ni mwendo wa dk sifuri tu
Asante kwa taarifa. TIGO wajiandae kunirudishia pesa zangu tena upesi. Kwa hili sina mzaha hata kidogo
 
Tigo security yao huwa weak sana kwani ukikosea password mara tatu unaambiwa u reset password tena simple tu yani. Hakuna maswali muhimu ya kuulizwa wala kwenda kwa wakala
 
Back
Top Bottom