Kuna kipindi serikali ilizitaka kampuni za simu kuweka PIN kwenye laini ili kulinda wateja,mfano ukinunua laini mpya inakuwa tayari na PIN,unabadilisha unaweka ya kwako,hiyo inakusaidia pale unapoibiwa simu au laini,mtu akitaka kuweka hiyo laini yako kwenye simu nyingine au kama simu yako ikazima, inamlazimu kuweka PIN ya laini...hii inazuia mwizi au mtu asiyehusika kutumia laini yako kama ukiibiwa au kupoteza bahati mbaya.... Halotel wanayo huduma hii kwenye laini zao mpya,ila Tigo na Vodacom bado laini zao hazina hiyo option.