Nimeishiwa nguvu na nimekuwa Mtu mwenye kukata tamaa kwa Mkasa ulionikuta

Nimeishiwa nguvu na nimekuwa Mtu mwenye kukata tamaa kwa Mkasa ulionikuta

Sikia mtu wa kwanza wa kumpa taarifa ni mwanamke,yeye ataenda kumwambia mama yake , mama atamwambia baba, baba ataamua nn kifanyike.

Lkn pia hatujua swala lako limefika wapi kwa maaana kuna sikua ya kutajiwa mahali alafu kuna siku ya kulipa mahali, lakini hii kila familia inakuwa na taratibu zake pambana mkuu.

Pole kwa changamoto ,ulifanya maamuzi ya haraka sana kumlipa jamaa ungemweleza ukweli hauna pesa lkn upo tayali kumlipa na kama vipi mwende gereji kujua bei kish ulipie matengenezo, hapo ndio utajua umimu wa bima pole kiongozi, natumai utavuka salama
 
Kumbe hii ndio sababu inayokupa mawazo kwa vitu vidogo, kijana mahari sio aibu, huendi kumnunua binti yao, bado ataendelea kuwa na mahusiano na nyumbani kwao, anaweza kwenda huko pakitokea tatizo lolote akatoe msaada hitajika hata kama utamuoa...
Ahsante Sana mkuu kwa ushauri huu 🙏🏼
 
Achia huyo mwanamke wamuoe wenye hela...

Nyie madereva wa bajaj na bodaboda huwa mnajifanya wajuaji sana barabarani...
 
Sikia mtu wa kwanza wa kumpa taarifa ni mwanamke,yeye ataenda kumwambia mama yake , mama atamwambia baba, baba ataamua nn kifanyike...
Ahsante Sana mkuu

Jamaa alinifanyia uhuni Sana, kila nikieleza anachomoa, na alikua Hana masihara kabisa
 
Achia huyo mwanamke wamuoe wenye hela...

Nyie madereva wa bajaj na bodaboda huwa mnajifanya wajuaji sana barabarani...
Ahsante Sana Mkuu🙏🏼
 
Unaweza kwenda kwa wakwe mkabageini alafu mahari utalipa ata baada ya miezi miwili mkuu kikubwa upambane na uwaombe hao wazee wakupambanie usipigwe na kitu kizito uko kwa wakwe zako

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Team Kataa Ndoa sijui hawapo online muda huu??

Wakija watasema ndoa ni Ubatili, Shukuru Mungu amekuletea ajali kukuepusha na ndoa.
Mwenzio yupo serious wewe unafanya upuuzi na shida zako mwehu tu hivi kwanini humu jamiiforum ni vichaa tu ndio wapo wengi
 
1. Nipe namba zao niongee nao
Ukweli ni huuu shetani hapendi mtu aoe awe na familia ila nenda kwao asubuhi waelezee ukweli na pia unanamba za wahusika ulioharibu gari Yao waombe wawe mashaidi uende nao wakasema ukweli kama hawatakuamini basi haikuwa RIZIKI
 
Hivyo nilikua nauliza, Je itawezekana kwenda ku bargain mahali tu kwa sasa hiyo siku, then nitalipa siku nyingine? Hata baada ya mwezi? Au ni lazima kwenye kikao hicho watanitaka kulipa hela kidogo?
Inawezekana mkuu, ongea vizuri tu na wazee wako.
 
Nadhani kabla hujamlipa huyo jamaa ungekuja kuomba ushauri...hapakuwa na ulazima wa kumlipa cash kwa pamoja. Mngekubaliana ungekuwa unamlipa taratibu,hata kama angekufikisha kwenye sheria usingefungwa zaidi mngepeana tu utaratibu wa kulipana.
 
Mahari hulazimiki kulipa siku hiyo. Labda makabila yanatofautiana. Kabila letu sisi utalipa utakapopata kabla ya kumchukua binti.

Tena hulazimiki kulipa yote. Ukilipa kiasi, nyingine utalipa kidogo kidogo mkiwa kwenye ndoa.

Pole sana na kuwa makini huko barabarani.
🤣🤣🤣🤣
 
Wakuu habarini!
Nimekuja kwenu naomba nisaidiwe kimawazo na ushauri.

Hivi karibuni nilipeleka barua ya uchumba (posa ) na Mambo yalienda freshi tu. Kikao Cha kupangiana mahari makubaliano ...
Sio lazima ulipe siku hio mnakubaliana afu unalipa ila isizidi mwezi ila kuacha kwenda ndio utaonekana msanii
 
Swala la kipuuzi hilo ndio linakuumiza kichwa!!mbona halina ulazima wowote!!
 
Kwenye kikao nenda tena bila kuonesha hofu.

Utapangiwa kiasi cha mahari, bargain nao, waambie utarudi.

Sometimes Mungu naye huwa anaepusha mengine japo kwa kibinadamu ni ngumu kuelewa
 
Mkuu jiandae kutembea na chupi kichwani,mahari yenyewe msala,kuishi na huyo manzi itakuwaje?Labda hata kuupata majanga Itakuwa ni Mababu wanakupa ishara uache upuuzi wa kuwaza ndoa.
 
Wakuu habarini!
Nimekuja kwenu naomba nisaidiwe kimawazo na ushauri.

Hivi karibuni nilipeleka barua ya uchumba (posa ) na Mambo yalienda freshi tu. Kikao Cha kupangiana mahari makubaliano yalikuwa kifanyike ijumaa hii. Nimejikuta nina mawazo Sana kwani hela niliyoiandaa kwa ajili ya kuitolea mahari kiasi Cha 700,000 nimekitumia chote kutokana na mkasa ulionipata pasipo kutegemewa jana usiku.

Hipo hivi, Mimi ni dereva bajaji DSM nilijikuta nimeikwaruza gari ubavuni na kuivunja taa ya kulia maeneo ya round about. So mwenye gari akaniamuru ili tusifikishane mbali nimlipe kiasi Cha sh. 650,000 ili akafanye matengenezo ya gari lake, vinginevyo atachukua hatua za kisheria kwani makosa yalikuwa ni yangu. Hivyo nikamlipa.

Nahisi kukata tamaa, kikao ni jumatatu na Sina mpango wa kupata hela nyingine kwa Sasa. Wazee wangu wapo mikoani hivyo hapa town nawatumia wazee tu wa kujuana, na ninaogopa hata kuwaambia kwani watahisi nafanya usanii.

Hivyo nilikua nauliza, Je itawezekana kwenda ku bargain mahali tu kwa sasa hiyo siku, then nitalipa siku nyingine? Hata baada ya mwezi? Au ni lazima kwenye kikao hicho watanitaka kulipa hela kidogo?

Kama Kuna mtu mwenye uzoefu au utaalamu na haya Mambo naomba anisaidie kimawazo au ushauri

Ahsante!

Moniely
Dsm.
Ondoa hofu mkuu we ongea na mshenga wakikupangia mahali utakuja baada ya muda flani kumalizia ,
Mahali huwa hatumalizi mkuu tunatoa sehemu tu

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu habarini!
Nimekuja kwenu naomba nisaidiwe kimawazo na ushauri.

Hivi karibuni nilipeleka barua ya uchumba (posa ) na Mambo yalienda freshi tu. Kikao Cha kupangiana mahari makubaliano yalikuwa kifanyike ijumaa hii. Nimejikuta nina mawazo Sana kwani hela niliyoiandaa kwa ajili ya kuitolea mahari kiasi Cha 700,000 nimekitumia chote kutokana na mkasa ulionipata pasipo kutegemewa jana usiku.

Hipo hivi, Mimi ni dereva bajaji DSM nilijikuta nimeikwaruza gari ubavuni na kuivunja taa ya kulia maeneo ya round about. So mwenye gari akaniamuru ili tusifikishane mbali nimlipe kiasi Cha sh. 650,000 ili akafanye matengenezo ya gari lake, vinginevyo atachukua hatua za kisheria kwani makosa yalikuwa ni yangu. Hivyo nikamlipa.

Nahisi kukata tamaa, kikao ni jumatatu na Sina mpango wa kupata hela nyingine kwa Sasa. Wazee wangu wapo mikoani hivyo hapa town nawatumia wazee tu wa kujuana, na ninaogopa hata kuwaambia kwani watahisi nafanya usanii.

Hivyo nilikua nauliza, Je itawezekana kwenda ku bargain mahali tu kwa sasa hiyo siku, then nitalipa siku nyingine? Hata baada ya mwezi? Au ni lazima kwenye kikao hicho watanitaka kulipa hela kidogo?

Kama Kuna mtu mwenye uzoefu au utaalamu na haya Mambo naomba anisaidie kimawazo au ushauri

Ahsante!

Moniely
Dsm.
pole mkuu kwa ajali, kama nimekuelewa vizuri ni kwamba umeshapeleka barua ya uchumba na ukakubaliwa hatua inayofuata ni wazee kwenda kujadiliana taratibu za mahari n.a. mambo mengine, nikwambie mahari sio lazima ilipwe siku hiyo wazee baada ya kukubaliana wataomba muda wa lini watapeleka kwa hiyo gharama zinazohitajika ni nauli tu za wazee wako.
 
Back
Top Bottom