Hello JF members,
Ilibaki kidogo tu nijiengue ndani ya JF baada ya kupondwa na wengi kuhusu tatizo langu lililousumbua moyo wangu, lakini ntafanya nini, sikuwa na mtu wa kumlilia, ndo maana niliamua kuanika dukuduku la moyo wangu kwenu nikiamini ningepata kutiwa moyo, lakini ilikuwa tofauti
Labda utoto still unanisumbua, ni mgeni katika mapenzi, mwanaume pekee ambaye hajaumiza moyo wangu ni aliyenifunza mapenzi, tuliachana kwa amani pasipo maumivu yoyote yale na kwa sababu maalumu
Kwamba pesa ya mwanaume hailiwi bure [emoji3][emoji3] Nalijua hilo, lakini sijui niwaeleze vipi kumhusu huyu mwanaume ili muone kuwa mimi ni mwenye haki
MSAADA NINAO UHITAJI KUTOKA KWENU
Kwa sasa sitaki kutegemea tena pesa za mwanaume yeyote yule, hata za boss wangu (mshahara) sizihitaji tena maake inaelekea atakuja tu kunitaka kimapenzi nikose cha kufanya kwa kuhofia kupoteza kazi, kisha nimkabidhi penzi, aumize moyo wangu, nirudi kwenu kulia, mnishushue tena
Kwa kiasi hiki cha laki moja nilichonacho mkononi sasa hivi, natamani kukifanya mtaji kiasi kwamba hata kesho nianze biashara yangu mwenyewe nikiwa huru, niachane na mambo ya ku supply bidhaa za watu, una drive gari zao wanaishia kukusimanga kuwa pesa za mafuta unakula, mara unachelewesha mizigo, at the end taarifa zinafika kwa boss, badala atake action utamsikia anakwambia "tulia Rose, achana na maneno ya watu" mwanaume hajawahi kuwa mwema kiasi hiki, kuna kitu anakitafuta kwangu, na ni mume wa wake watatu, anakesha club nnavyosikia, siku nyingine anakuja ananukia k vant
Hivyo itapendeza kama mtanishauri biashara ya kufanya kwenye hili jiji la watu kwa kiasi hicho cha laki ili nitengeneze pesa zangu, niishi maisha yangu mwenyewe
Pindi ntakapopokea mshahara tarehe 8 July ntatenga kiasi cha laki mbili ili nifungue biashara nyingine, au nikuze biashara mtakayonishauri kufanya
Sintojari status yangu mtaani, urembo ntatupa kule, aibu nitaitoa machoni mwangu ili mradi najua ninachokitafuta ni kipi, malengo yangu ni yapi
Please, nahitaji ushauri wenu
NB: Samahani kwa mwandiko wangu mbovu