Jamani tunayasema haya kila siku Tanzania ni Tanganyika isipokuwa, penye mafao Wazanzibar ni Watanzania. Ndiyo maana tunasisitiza kwamba Tanganyika iwepo ijisimamie ili kuepuka kutumiwa vibaya
Viongozi wa EAC wakikutana wimbo wa EAC ndio unapigwa kwa ujumla wake, hawa hatuna Muungano
Nchi yenye Muungano tuna nyimbo mbili.
Waliokwenda kuomba 'Umoja Bid' ni Chama cha Mpira Tanganyika a.k.a TFA , Kenya na Uganda.
Leo Zanzibar wakiwa na Chama chao (ZFA) wanataka mechi za AFCON zipelekwe Zanzibar kwa jina la Tanzania.
Kumbuka ZFA walishajitoa TFA ili wakaendeleza mpira wao, leo wanakuja kutaka 'mafao' kupitia Tanzania
Gharama zote za AFCON atazibeba Tanganyika kwa jina la Tanzania.
Kwanini tusitumie rasilimali kuboresha viwanja vya Arusha na Mwanza! wanaolipa gharama za mambo haya!
Kuna tatizo na suluhu wanayo Watanganyika! Rudisha Tanganyika ijisimamie kama ilivyo Zanzibar.
Kama Muungano unahitajika waulizwe Wazanzibar maana Watanganyika hawana cha kupata au kupoteza
JokaKuu Pascal Mayalla