Hao Wapemba wamekua wakilalamika kwa miaka 58 sisi hiyo miaka 2 tu imekua nongwa?Kiufupi tu ni kuwa Tanzania tunaongozwa na mkoloni mpemba
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hao Wapemba wamekua wakilalamika kwa miaka 58 sisi hiyo miaka 2 tu imekua nongwa?Kiufupi tu ni kuwa Tanzania tunaongozwa na mkoloni mpemba
🤣🤣Ila mkuu Hii JobTrueTrue huwa inanichekeahaga sana. Nimekuja kusoma mambo ya msingi hapa najikuta nacheka
Inasikitisha kwa kweli.Rais Mwinyi alipongeza ZRA kwa kukusanya Takribani Bilioni 288 kwa miezi 5. (55.4 Bilioni) kwa mwezi
Ni kwa mujibu wa Gazeti la 'The Citizen'. Akitoa pongezi hizo Rais anasema mafanikio mengi katika ujenzi wa Barabara, maji, afya na elimu ni matokeo ya ukusanyaji mzuri wa kodi wa 'SMZ'
Jana Naibu Waziri mkuu Biteko amezindua Jengo la Uhamiaji Pemba lililogharimu Takribani Bilioni moja.
Katika uzinduzi huo alikuwa na kamishna wa Uhamiaji wa Tanzania na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani
Jengo limejengwa kwa gharama za Uhamiaji JMT, yaani kutoka Bajeti ya Wizara ya mambo ya ndani
Kama tulivyowahi kujadili, fedha za huduma za Uhamiaji Zanzibar zinabaki SMZ, lakini gharama za Uhamiaji zinabebwa na JMT ambayo ni kodi za Tanganyika. Kwanini SMZ isijenge jengo hilo kwavile wanakusanya fedha za Uhamiaji ?
Zanzibar inapata 10% ya Bajeti ya JMT, ina mgao wa fedha ziwe ni Mikopo au misaada na makusanyo ya kodi hayavuki bahari. Zanzibar haina mchango katika Muungano.
Gazeti la Mwananchi limetoa kanda na michango yake ya kodi kwa Taifa, Dar es Salaam ikibeba 84% , ikifuatiwa na Kanda ya Kaskazini, Ziwa, Kati , kusini na Nyanda za Juu. Zanzibar haikuonekana.
Pamoja na hayo fedha zinazokwenda Zanzibar kutoka Tanganyika a.k.a Tanzania ni nyingi kuliko kanda yoyote iliyotajwa hapo juu licha ya ukweli kwamba Zanzibar haina Bajeti za Wizara nyeti na zenye gharama
Hoja inabaki pale pale kwamba rasilimali za Tanganyika zimegeuzwa za Tanzania na hapo zinakuwa 'abuse'.
Hakuna msimamizo wa rasilimali za Tanganyika! Na abuse imekuwa kubwa sana awamu hii.
Tunahitaji Tanganyika isimamie rasilimali zake, kama Muungano unahitaji waulizwe Wazanzibar!