Nimejitahidi kila mbinu kuwa mwanaintelijensia bila mafanikio

Nimepotea kidogo ila nilipata wasaa was kuangalia MOVIE (RAAZ 2018)

acheni kabisa nimeona kabisa baada ya Recruitment wazo litakuja tena la kumwomba Mungu kupangiwa

1.Internal Eagle wing
Kuliko External Eagle wing


2.Center Internal Eagle wing makao makuu


Da kweli ni kazi baada ya kazi
 

Ukikosa huko usikate tamaa nenda PT hata huko zipo idara ambazo ukibahatika kuwekwa basi mtaani kwako au watu wanaokuzunguka bado watahisi wewe ni tiss kwa asilimia 70 kutokana na muonekano uliochoshwa na mikazi migumu ya kuumiza kichwa

Polisi kuna CID hawa ni undercovers wa jeshi la polisi huvaa kiraia hata unyoaji hivyo basi pesa nzuri utalipwa na kazi zao hazijatofautiana sana na tiss kama ulitaka kwa ajili ya kuvimba kitaa pia itakufaa

Usisahau kuwa wapo polisi tiss pia utakutana nao kazini yaani tiss ni idara ambayo ina watu wake sehemu zote mpaka vijijini kwa wakulima kwaio basi hata katika majeshi yetu kama JW, PT, na Magereza wapo askari ambao pia ni Tiss ila hawa huwa ni ngumu zaidi kuwasanukia

Kama utafanya kazi kwa weredi na utaonekana una kitu cha ziada cha tofauti ambacho kinaweza kuwa msaada katika idara basi watakuita wenyewe na utakuwa na mishahara miwili hapo ushidwe wewe kujenga ghorofa

Ila nakushauri acha kwenda kwenda kujichora katika ofisi au maeneo yanayosadikika ni ya tiss maana unazidi kujipunguzia sifa
 
Mkuu kwa namna sifa na tabia tunazozisikia kuwahusu hao tiss za USIRI,NiDHAM,UZALENDO nk naona kama unajitolea sifa ww Mwenyewe kwa sababu inaonekana huna KIFUA,inaonekana kama hiyo kazi unaitaka kwa MALENGO BINAFSI na MAALUM unayoyajua ww,ila mm kwa mtazamo wangu naona kama ni kwa ajili ya SHOW OFF zaidi kuliko majukumu utakayopangiwa.

Una story nyingi sana za MiTAANI,unaonekana ni mtazamaji mzuri wa Muvi za kivita na mapigano hadi zimekuathiri kiasi cha kutaka kuwa mmoja wa wahusika ktk hizo filamu.

Majukumu utakayo pewa yanaweza kuwa tofauti kabisa na uhalisia ulionao ktk hiyo kazi unayoitaka,na kwa vile unaitaka kwa Malengo Maalum kwako inakuwia vigumu kuipata sababu umeshajiDisqualify ww Mwenyewe.

Nakushauri kama unashughuli zingine za kujiingizia kipato ni heri ukaendelea nazo mana kazi zingine hazihitaji siasa.

Wasalaam.
 
Maisha magumu sana mkuu. Hata mkiwapata waacheni tu nao wanajitahidi kupeleka mkate nyumbani.

Pembaneni na wezi tu na mafisadi ambao wanatuibia daily na kurusha lawama Kwa wengine.
 
Maisha magumu sana mkuu. Hata mkiwapata waacheni tu nao wanajitahidi kupeleka mkate nyumbani.

Pembaneni na wezi tu na mafisadi ambao wanatuibia daily na kurusha lawama Kwa wengine.
Una hoja ya msingi. Lakini unaweza kukuta ndiyo hao wanawashauri wezi na mafisadi nini cha kufanya ili nchi isijitegemee kiuchumi na kisiasa. Yaani nchi inakuwa mateka wa nchi nyingine huku mkijifanyA mpo huru. Putin katuonyesha hili!

Hata hivyo, jukumu la kulinda uhuru wetu kiuchumi na kisiasa ni letu sote raia na ninyi wataalamu wa mambo hayo.

Asubuhi njema Mkuu.
 
Asubuhi njema iwe kwako pia mkuu.

Intelijensia ni biashara, kama wanatumika kutuhujumu na nyie muwatumie pia Kwa njia hiyo hiyo huko Kwa handlers wao.

Problem ni maisha ni magumu mkuu, kila mtu anataka kupeleka mkate mezani.. Na kumili vitu. Hawa wezi na mafisadi mkiwashughulikia vizuri.. Wengi watatekeleza majukumu Yao vizuri.. Otherwise kila mtu anapambania utajiri..
 
Kuna saa hii nazo ni Story tuu watu wanabadilika sana waliokuwa watundu wakiwa watoto wakiwa wakubwa wanakuwa Wastaarabu sana
 
Mtoa mada mimi nina Raia mwema nina maswali hapa

Kwanini unataka kujiunga na Idara yetu nyeti ?

Je shida yako ni Ajira au Kipato ?

Je umesema una ndugu ambao ni wastaafu ambao walikuwa kwemye Idara ina maana umeshindwa kuongea nao au ?
 
Hata USALAMA WA TAIFA TISS pesa ipo Mzee
Akili yako ni ndogo sana , tafuta kitabu cha EvaristChachali kinaitwa Afisa Usalama ni nani na anafanya kazi gani ili upate maarifa kidogo, Kama unawaza kwenda Usalama wa Taifa halafu unawaza kupiga pesa hapo kazi itakuwa ni ngumu sana. Sifa kubwa ya Afisa Usalama ni UZALENDO. Kama unawaza pesa tafuta connection za taasisi nyingine zenye mishahara na marupurupu upate hiyo pesa unayoitaka lakini sio pale TISS.
 
Kwa bahati mbaya vyoote ulivyotaja ni sawa na 1/100 kwahiyo kuwa na subra 99 sio mbali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…