Nimekata tamaa, nimepigika, nimeteswa, nimedharauliwa, nimeumizwa, sasa basi!

Sali sana
Sali sana
Sali Sana
Pray hard
Pray hard
Pray hard

Kuna faraja katika kusali Sali Sali my bro .Mungu atakupa faraja na furaha
Sali kwa Imani .Sali Sali bro Utashinda kila lilo gumu

There is Power in prayers - utaongeza Imani na mambo yako yote yatakuwa mazuri

Usiende kwenye uovu na ulevi hata hiyo kazi utapoteza utakosa future kabisa

There is hope in prayers
 
Kama wadogo zako uliowapenda umewawezesha anayekulaumu Nani?
.
Na hata Kama wanakulaumu wewe ulitenda wajubu wako- Tuliza akili-starehe hazitikiswi hivyo
Nimetenda wajibu wangu. Nimetimiza ndoto zangu za kuwasomesha wadogo zangu nao wapenda sana.
Ni muda sasa nitafuta furaha. Waliosema raha jipe mwenyewe hawakukosea.
 
Asante kwa ushuhuda wako unaponya
 
Japo hutaki ushauri, ninachokuambia ni kuwa, Sawa ulitakiwa katika hali duni, umekulia humo na kuwasaidia ndugu zako. Ile huko sahihi unaposema umezaliwa na mpaka kifo kikikukuta utakuwa katika maisha duni. Hujafariki bado, na una nafasi ya kuyaboresha maisha yako.
Huyaboreshi maisha yako kwa ulevi, uvutaji au uzinzi.
Fanya kazi yako na biashara zako, tengeneza pesa, kama unataka kujenga, mjenge, kama unataka kununua gari, nunua, ili mradi sasa uanze kuishi maisha yenye hadhi yako, ndugu akuthamini au la, hiyo isiwe tatizo kwako. Anayekupenda mpende, anayekuthamini hali kadhalika. Mkeo hakutaki, aende zake, wala usiendelee kukaa naye.
Jipe faraja mwenyewe ila sio kwa kujizamisha kwenye tabia za uchafu.

Sent from my LM-Q710(FGN) using JamiiForums mobile app
 
Simshauri mtu anywe pombe kama njia ya kupoteza mawazo lkn kama starehe fresh make alcohol makes you live the moment.

Ukinywa sababu ya stress mzee utapoteza vyote ulivyopigania miaka yote.
 
Pole sana, ila nakushauri kunywa pombe sijui kufanya anasa hakutakusaifia, sana sana vitakupoteza tu, kusaidia ndugu au kutosaidia sio kama utapokea taji hapana, unaweza pewa shukrani au dhihaka, uliofanya yote Mungu ndiye aliyeyaona, wewe kaa chini na Mungu wako hizo nuksi zikutoke kama Mungu aliye kuumba anakukubali na kukupa baraka hao watu vipi muombe Mungu fanya kazi zako usiache kumtolea Mungu sadaka, WAKATI MWINGINE UNAOWAAMINI NDIYO HUWA WABAYA WAKO HAO HAO.
 
Kuna Uzi niliandika humu kwa nini watu wenye roho nzuri na kujitolea kwa wenzao huishi maisha magumu au kawaida sana kuliko wale waliowasaidia?Tafuta huo Uzi unakuhusu mkuu.Katika dunia ya sasa jaribu kutafuta furaha yako kabla ya furaha ya wengine tunapata maisha magumu kwa kutaka kuwafurahisha au kuwahurumia wengine na kujiumiza wenyewe.
 
Kuna watu watakwambia utatenga vipi ndugu, wakati mkeo sio ndugu yako! Lakini maisha mengine ndugu huumiza kuliko mtu baki na ukiwaendekeza utashindwa kujenga familia yako, siku ya siku hao ha watakucheka na kila mtu atakuwa kwake na familia yake
 
Kuna watu watakwambia utatenga vipi ndugu, wakati mkeo sio ndugu yako! Lakini maisha mengine ndugu huumiza kuliko mtu baki na ukiwaendekeza utashindwa kujenga familia yako, siku ya siku hao ha watakucheka na kila mtu atakuwa kwake na familia yake
Huwatengi ila hufanyi lolote ambalo litaharibu maisha yako binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu watakwambia utatenga vipi ndugu, wakati mkeo sio ndugu yako! Lakini maisha mengine ndugu huumiza kuliko mtu baki na ukiwaendekeza utashindwa kujenga familia yako, siku ya siku hao ha watakucheka na kila mtu atakuwa kwake na familia yake
Ndio tabia ya ndugu utawasomesha kwa kujibana watafanikiwa na kuajiriwa au kujiajiri maisha yao yatakua mazuri wakati wewe unakonda kwa mamikopo uliokopa kuwasaidia halafu Siku utayoomba msaada watakwambia hela zako ulikua unazichezea kwa anasa ndo maana huna maendeleo hapo ndo utajua thamani ya kujiimarisha kabla kusaidia wengine
 
Na unakuta mpaka wazazi wanamgeuka mtoa misaada na kuwakubali zaidi wanaosaidiwa yaani inaumiza sana, mwanamke anayeolewa na mwanaume ambaye kwao wote wanamtizama yeye daa nimaumivu mpaka basi, yaani kama catapilah linatengeneza barabara ikiwa tayari linabebwa kwenye gar lingine ili lisiharibu hiyo barabara
 
Hujakosea ndugu mpaka matusi utapokea, yaani sijui nikitu gani sie ngozi nyeusi mpaka unashindwa kuelewa ni kitu gani!
 
Baba yangu aliwahi kuniambia "Tengeneza maisha yako, mm baba yako numesaidia sana ndugu lakin mwsho wa siku malipo yao yamekua ni kunidharau"
 
Asante mkuu
 
Mkuu kuna kosa kubwa umelifanya ndilo linalokutesa!!USIBEBE MAISHA YA MTU NA KUTAKA KUYABADILISHA!!!yaani mwache ndugu apambane mwenyewe kwenye mazingira ya kawaida hata shule ya kawaida ili usilipe magharama makubwa mno!!!waache wasome na kupambana katika mazingira ya kawaida atakaefaulu msomeshe shule za kawaida!!!!Pia usibebe maisha ya mtu moyoni boresha kwako na wanao hata wazazi wakichoka uje uwalee kwako!!sio ubadili maisha yao!utahangaika sana na kufeli!!
 
Nakwambia kuna watu utasikia una roho mbaya lakini huo ndiyo kweli

Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…