Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Raha jipe mwenyewe ndugu yangu.Kamba sili ila natafuta furaha na mimi nimechoka.
Ni kama vile umesoma mawazo yangu!! Ushauri wangu ni kama wako kwa 90%!You are a great guy/person sikujui personally lakini nimekuelewa. Una maisha kazi nzuri etc shida yako kubwa na kinachokufanya uteseke ni tabia yako ya kuhitaji kuwaridhisha watu. Binadamu huwezi kumridhisha no matter how much u try. Hata kama ukichukua mshahara wako wote ukampa mama yako bado hautokua favourite wake. Zaidi atakulalamikia. Acha tabia ya kua people pleaser saidi kadri ya uwezo wako lakini usitegemee positive feedback. Hutopata kutoka kwa wafanyakazi wenzio, mkeo ndugu zako etc zaidi utaonekana bwege tu usie na akili badala ujenge/ ununue gari unawahonga wao. Ishi maisha yako, kua selfish kidogo, kua na boundaries. Kua disminder heshima itakuja. Binadamu hawana shukrani
Mkuu pesa sio dawa ya kila kitu. Sina shida ya pesa kabisa.
😳😳😳Kama hataki kumkaza, anambie mm nimkule kimasihara. We are here for season, usikubali mtu wa kando akutese wakati una maisha yako.
Sent using Jamii Forums mobile app
Jiarbu kufany research utaona kabsaa ww unanafuu kuna wat wana huzin kila siku ila awakati tamaa kama wwNimekata tamaa; Nimepigika, nimeteswa, nimedharauriwa, nimeumizwa , sasa Basi !
Ndugu zangu wana MMU ambavyo nimetanguliza hapo awali sina namnKumbukax
Dunia kwangu imekuwa chungu mno. Sioni jema wala.zuri katika dunia hii ya wanadamu. Pengine huko mbinguni aliko Mungu. Ili angalau nipate nafuu ya maumivu moyoni nawiwa kushare hapa.
Nimeumizwa sana na jamii. Kwenye siasa nimeumia sana. Kwenye jamii hivyo hivyo. Kwenye familia nina machungu makali mno. Kazini kwa moto kama kaa la mkaa wa mawe. Ndugu zangu mimi si lolote wala chochote kwao. Kifupi najiona thamani ya kuishi duniani haipo. Mwandishi wa Biblia kitabu cha Mhubiri alisema Duniani kila kitu ni upuuzi mtupu. Naungana naye kwa leo.
Ni hivi; katika makuzi yangu nilikulia mikononi mwa Mama yangu: alinilea kwa shida sana mimi na wadogo zangu. Nikiwa na miaka 9 nilianza kushirikiana na mama kutafuta kipato ili tupate japo mkate wa kila siku. Nilijishughulisha na kazi mbali mbali ikiwemo kilimo, biashara ya kuuza miwa, kuokota mavi ya ngombe na kuuza kama chanzo cha samadi, nimekata nyasi kwa ajili ya kuuzia watu wenye mifugo.
Wakati wote huo pamoja na maisha hayo nilikuwa na faraja maana siku zote mama yangu alitupa moyo mimi na wadogo zangu. Alipambana kila wakati na alidanganya hapa na pale ili tupate kuishi. Nakiri kabisa mama yangu hakuwahi kuwa mwizi wala kumuona akiwa na wanaume wengine kwa ajili ya kutafuta unafuu wa maisha. Baba yangu aliishi mjini na huko alifanya kazi ya kujiajiri na kuoa wake wengine na kutapanya mali.
Nikiwa na miaka 10 nilianza darasa la kwanza hadi nikamaliza form 4. Na nikajiunga na kidato cha kwanza hadi Elimu ya juu.
Wakati wote huo mimi nilikuwa mlezi kwa wadogo zangu na familia yangu kwa ujumla. Niliamini nitapambana hadi tufike mahali maisha yawe bora au atleast nafuu.
Sasa kazi ikaanza. Nikapata job nzuri ambayo inanilipa mshahara mzuri wa kuridhisha. Nikasema asante Mungu. Nitahakikisha wadogo zangu wote wanasoma na kufika pazuiri waliofeli nikawarudisha shuleni na wengine ku-resit mitihani yao. Alhamdulillah hawakuaniangusha wakafaulu nikawaendeleza vyuoni na sasa wengine wameahamaliza wana maisha yao.
Wengine wakawa wananidhihaki eti toka umefanya kazi una nini mpaka leo. Mbona hakuna ulichofanya cha kuendeleza maisha?? Nafsi yangu ikawa inaumia sana nikiona pesa nyingi nilizotumia kuwanyanyua wadogo zangu wa kike na wa kiume.
Kazini nilikuwa mchapa kazi Mkurugenzi wa shirika akanipa cheo kuwa msimamizi wa operasheni. Hapo ikawa kasheshe...wafanya kazi hawanisikilizi wala kutekeleza maagizo yangu. Mimi ni mkristo naamini katika kutenda haki sikuwahi kumwonea mfanya kazi yeyote. Nilifanya kazi kwa kuzingatia miongozo, kanuni, taratibu na ubinadamu. Pia. Nilijipambanua kuwa kiongozi bora lakini ikafika mahala baadhi ya wafanya kazi waliochini yangu kwenda kunisema kwa boss kuwa nawaonea( wafaya kazi hawa wana undugu na boss) nilifanyiwa kikao na Bodi ya wakurugenzi wakasikiliza malalamiko yao na hoja zangu. Wajumbe wa Bodi walikiri kuwa hawaoni Tatizo wala kasoro yoyote ktk utendaji wangu na kwamba malalamiko yaliyopelekwa na baadhi ya wafanya kazi wenzangu hayana msingi hapo nikapona.
Ikaja katika kundi la wateja yaani wapokea huduma zetu. vibwanga kila kukicha. Hata niwape huduma gani basi malalamiko chini kwa chini hayakosi. Wengine Wakinitolea maneno ya dharau pengine kwa mwonekano wangu wa upole na ushamba kidogo lakini kutokana na kazi yangu ya Wito nawiwa kuwa mvumilivu tu na kusonga mbele.
Mke wangu naye hivyo hivyo haoni kama nafanya chochote kwenye familia. Napewa maneno ya kashifa ya kuudhi na kejeli. Mimi silali mchana wala usiku natafuta maisha. Nafanya kazi kampuni nikitoka naunganisha kwenye kazi zangu binafsi ili kuongeza mpunga.
Wazazi wangu nao hivyo hivyo, nawasikia wakinisema wazi wazi vimaneno vya kejeli kuwa maisha yatanipiga. Ni kama wanafurahi au wanatamani yanipige na mimi sipo tayari kwa hilo labda Mungu mwenyewe akatae.
Huku kwenye mahusaiano ya kimapenzi naomba nisiguse kabisa hali ni mbaya mno. Mimi ni wa kuumizwa tuu. Sijui neema ya dunia hii. Wanafaidi wengine.
Ili ku-make maisha mazuri na kulinda afya yangu nilikataa kata kata kunywa pombe wala kilevi cha aina yoyote nilikataa mambo ya wanawake na utumwa wa mapenzi. Mapenzi yangu yoote niliwapa wadogo zangu. Kiukweli wadogo zangu hawa tisa(9) nawapenda sana. Huniambii kitu juu yao nimewalea toka wanazaliwa hadi sasa ni wakubwa wa mwisho yuko form four now.
Kwa kuwa nimefika mwishi sioni Jema wala zuri katika dunia hii sasa Basi! imekwisha.
Nataka nianze kufaidi pesa zangu mimi mwenyewe. Sitaki mtu anisemeshe. Mimi na maisha yangu. Binadamu nimewachoka. Nitakunywa Pombe mpaka nitapike. Nitavuta sigara mpaka mapafu yakome. Nitalala kwenye madanguro. Nitahonga sana. Nataka ku- neurtralize my sadness. Siwezi kuwa mimi ni wa uchungu tu maisha yangu yote. Siwezi kuwa mimi wa majonzi tu mpaka nife.
Lengo la thread hii sio kutaka ushauri wala nini nataka wengine mjue kuwa tuko tunaoishi na machungu tangu tunazaliwa mpaka tunakufa. Ukiona una furaha katika maisha yako basi ilinde furaha hiyo wengine hatuna bahati.
Asalam aleykum.
👍Pole sana mkuu, ila huko unakotaka kukimbilia ndo kutakumaliza kabisa..Kujipa furaha sio kunywa pombe, kuvuta sigara wala kulala kwenye madanguro. Unaongeza matatizo juu ya matatizo. Ishi maisha yako sasa, wakupende wasikupende sawa..Endelea kutenda wema ila wema usizidi sana.
Sasa wewe unawasomesha wadogo zako, wazazi wako wanafanya shughulo gani?
Umesoma vizuri maelezo yangu??Una shida ya nini sasa?
Ndio nimeligundua hili leo. Nachukua hatua.Siku utakayoanza kuamini kuwa wewe ndiye mtu pekee anayeweza kukupa furaha ndiyo siku ambapo tatizo litaanza kutatuka, asante.
WellRaha jipe mwenyewe ndugu yangu.
Pia ukisaidia ndugu au hata rafiki usisubiri shukrani, sema tu yatosha na songa mbele na maisha yako, jihudumie kula vizuri, vaa vizuri ikibidi kuwa selfish kidogo usisubirie sijui mke au Mama au ndugu aone au athamini umuhimu wako!!
Kazini unaweza stepdown kwenye hicho cheo ikawa mtumishi wa kawaida ili kuirudisha furaha yako maana umesema kazi yako Ina mshahara mzuri.
Kumbuka furaha yako haitoki kwa mtu mwingine zaidi yako!
Almsiki.