Nimekata tamaa, nimepigika, nimeteswa, nimedharauliwa, nimeumizwa, sasa basi!

Hili pia ni somo. Lakini kuendesha rough gari yako ni hatari kuliko. Umenichekesha hapo kwenye nyimbo za misiba. Naomba niunge kwenye hiyo playlist yako
Ukiona unaziona hatari/athari za mienendo fulani angalau kwa watu wengine basi unapona, unless otherwise hapa ungeshabikia.
 
Kabisa mimi nimechelewa kuolewa na kuzaa sababu ya wadogo zangu wasome wawe na maisha yao na mama kumjengea,kwa sasa sitoi hela yangu kizembe wananiitaga mpare nilivyo bahili
Inatakiwa namna hiyo maana unaweza kuonekana huna plans...
 
kumbe tupo wengi tulopitia machungu ya namna hii? bt sijapenda umaliziaj wa uzi wako.

niliwasaidia ndg hadi wakatimiza ndoto zao bt cha ajabu baada yakuharibikiwa mambo walikua wakwanza kunicheka na kunidhihaki kwa watu niliumia sana kama mwanadam na nikaamua kujitenga kivyangu na familia yangu nikiyaishi majungu mazito yasiyo kifani..

siku1 nipo na mzee1 rafiki angu nikamuuliza hivi duniani kuna furaha? akanambia ipo bt kwa wachache waloishinda vita ya kiroho either kwa kuwa wacha mungu/kwa madawa ya miti shamba coz mahusiano ya binadam huharibiwa katika ulimwengu wa roho yaani utu wako na thamani yako inaharibiwa mbele za watu kitu ambacho husababisha kudharauliwa, kuchekwa na kuonekana usie na thaman..

hakika sikumuelewa bt niliuliza tena je kuna uwezekano nami kua na furaha? akajibu inawezekana ikiwa utafanikiwa kuzidhibiti athari hizo, dah! nilivuta pumzi kubwa kisha nikamwomba msaada zaidi..

hakua na hiyana alinipa msaada zaidi hadi leo ninamahusiano mazuri na ndgu na wananiheshmu.
 
Nakuelewa sana hapa, dunia ni vita na hakuna iliyomwacha salama, we suffer but in different ways
 
Uandishi wako tu unaonesha usipobadilika utaonewa sana ... yani mtu ashakuambia ungekua KAKA YANGU ningekupiga makofi unafikiri kuna mtu anaweza kumpiga kaka yake makofi kama hamdharau alafu we unajibu ...sasa MKUU unataka kunipiga kofi kwa sababu gani ukimaanisha kwamba kama anasababu ya kukupiga kofi akupige inaonyesha jinsi ulivyo dhaifu ndio mana wanaokuzunguka wanakuonea ...BE THE BEAST WHICH WANTS TO EAT YOU
Daaah asipokuelewa wewe hataweza kuelewa wengine mkuu, hongera sana.
 
Nakuelewa sana hapa, dunia ni vita na hakuna iliyomwacha salama, we suffer but in different ways
thamani yako ikishaporwa na walimwengu ktk ulimwengu wa roho utaonekana bure hata ufanye nini, na mleta mada anazo dalili zote zakuharibiwa thamani yake ktk ulimwengu wa roho, ni vile hajajua tu kisha akafanya utatuzi
 
I wanted to say exactly that, ila nilihisi nakosa maneno ya kueleweka, unavishwa roho za kuonewa kukataliwa kudhulumiwa kudharaulika kutwezwa, nk
Hawezi kuona mpaka itokee afundishwe ni nini maana ya mambo haya na yanafanyikaje, unaibiwaje haki zako kiroho, sababu kuna kitu huwa wanafanya, wanaondoa ufahamu wako wa kuyatambua hayo mambo.Yaani ufahamu unavurugwa,nafsi unakuwa kifungoni unaishi kadri ya how they remote you.

S
Nimekata tamaa; Nimepigika, nimeteswa, nimedharauriwa, nimeumizwa , sasa Basi !

Ndugu zangu wana MMU kama ambavyo nimetanguliza hapo awali sina namna tena.

Dunia kwangu imekuwa chungu mno. Sioni jema wala.zuri katika dunia hii ya wanadamu. Pengine huko mbinguni aliko Mungu. Ili angalau nipate nafuu ya maumivu moyoni nawiwa kushare hapa.

Nimeumizwa sana na jamii. Kwenye siasa nimeumia sana. Kwenye jamii hivyo hivyo. Kwenye familia nina machungu makali mno. Kazini kwa moto kama kaa la mkaa wa mawe. Ndugu zangu mimi si lolote wala chochote kwao. Kifupi najiona thamani ya kuishi duniani haipo. Mwandishi wa Biblia kitabu cha Mhubiri alisema Duniani kila kitu ni upuuzi mtupu. Naungana naye kwa leo.

Ni hivi; katika makuzi yangu nilikulia mikononi mwa Mama yangu: alinilea kwa shida sana mimi na wadogo zangu. Nikiwa na miaka 9 nilianza kushirikiana na mama kutafuta kipato ili tupate japo mkate wa kila siku. Nilijishughulisha na kazi mbali mbali ikiwemo kilimo, biashara ya kuuza miwa, kuokota mavi ya ngombe na kuuza kama chanzo cha samadi, nimekata nyasi kwa ajili ya kuuzia watu wenye mifugo.

Wakati wote huo pamoja na maisha hayo nilikuwa na faraja maana siku zote mama yangu alitupa moyo mimi na wadogo zangu. Alipambana kila wakati na alidanganya hapa na pale ili tupate kuishi. Nakiri kabisa mama yangu hakuwahi kuwa mwizi wala kumuona akiwa na wanaume wengine kwa ajili ya kutafuta unafuu wa maisha. Baba yangu aliishi mjini na huko alifanya kazi ya kujiajiri na kuoa wake wengine na kutapanya mali.

Nikiwa na miaka 10 nilianza darasa la kwanza hadi nikamaliza form 4. Na nikajiunga na kidato cha kwanza hadi Elimu ya juu.

Wakati wote huo mimi nilikuwa mlezi kwa wadogo zangu na familia yangu kwa ujumla. Niliamini nitapambana hadi tufike mahali maisha yawe bora au atleast nafuu.

Sasa kazi ikaanza. Nikapata job nzuri ambayo inanilipa mshahara mzuri wa kuridhisha. Nikasema asante Mungu. Nitahakikisha wadogo zangu wote wanasoma na kufika pazuiri waliofeli nikawarudisha shuleni na wengine ku-resit mitihani yao. Alhamdulillah hawakuaniangusha wakafaulu nikawaendeleza vyuoni na sasa wengine wameahamaliza wana maisha yao.

Wengine wakawa wananidhihaki eti toka umefanya kazi una nini mpaka leo. Mbona hakuna ulichofanya cha kuendeleza maisha?? Nafsi yangu ikawa inaumia sana nikiona pesa nyingi nilizotumia kuwanyanyua wadogo zangu wa kike na wa kiume.

Kazini nilikuwa mchapa kazi Mkurugenzi wa shirika akanipa cheo kuwa msimamizi wa operasheni. Hapo ikawa kasheshe...wafanya kazi hawanisikilizi wala kutekeleza maagizo yangu. Mimi ni mkristo naamini katika kutenda haki sikuwahi kumwonea mfanya kazi yeyote. Nilifanya kazi kwa kuzingatia miongozo, kanuni, taratibu na ubinadamu. Pia. Nilijipambanua kuwa kiongozi bora lakini ikafika mahala baadhi ya wafanya kazi waliochini yangu kwenda kunisema kwa boss kuwa nawaonea( wafaya kazi hawa wana undugu na boss) nilifanyiwa kikao na Bodi ya wakurugenzi wakasikiliza malalamiko yao na hoja zangu. Wajumbe wa Bodi walikiri kuwa hawaoni Tatizo wala kasoro yoyote ktk utendaji wangu na kwamba malalamiko yaliyopelekwa na baadhi ya wafanya kazi wenzangu hayana msingi hapo nikapona.

Ikaja katika kundi la wateja yaani wapokea huduma zetu. vibwanga kila kukicha. Hata niwape huduma gani basi malalamiko chini kwa chini hayakosi. Wengine Wakinitolea maneno ya dharau pengine kwa mwonekano wangu wa upole na ushamba kidogo lakini kutokana na kazi yangu ya Wito nawiwa kuwa mvumilivu tu na kusonga mbele.

Mke wangu naye hivyo hivyo haoni kama nafanya chochote kwenye familia. Napewa maneno ya kashifa ya kuudhi na kejeli. Mimi silali mchana wala usiku natafuta maisha. Nafanya kazi kampuni nikitoka naunganisha kwenye kazi zangu binafsi ili kuongeza mpunga.

Wazazi wangu nao hivyo hivyo, nawasikia wakinisema wazi wazi vimaneno vya kejeli kuwa maisha yatanipiga. Ni kama wanafurahi au wanatamani yanipige na mimi sipo tayari kwa hilo labda Mungu mwenyewe akatae.

Huku kwenye mahusaiano ya kimapenzi naomba nisiguse kabisa hali ni mbaya mno. Mimi ni wa kuumizwa tuu. Sijui neema ya dunia hii. Wanafaidi wengine.

Ili ku-make maisha mazuri na kulinda afya yangu nilikataa kata kata kunywa pombe wala kilevi cha aina yoyote nilikataa mambo ya wanawake na utumwa wa mapenzi. Mapenzi yangu yoote niliwapa wadogo zangu. Kiukweli wadogo zangu hawa tisa(9) nawapenda sana. Huniambii kitu juu yao nimewalea toka wanazaliwa hadi sasa ni wakubwa wa mwisho yuko form four now.

Kwa kuwa nimefika mwishi sioni Jema wala zuri katika dunia hii sasa Basi! imekwisha.

Nataka nianze kufaidi pesa zangu mimi mwenyewe. Sitaki mtu anisemeshe. Mimi na maisha yangu. Binadamu nimewachoka. Nitakunywa Pombe mpaka nitapike. Nitavuta sigara mpaka mapafu yakome. Nitalala kwenye madanguro. Nitahonga sana. Nataka ku- neurtralize my sadness. Siwezi kuwa mimi ni wa uchungu tu maisha yangu yote. Siwezi kuwa mimi wa majonzi tu mpaka nife.

Lengo la thread hii sio kutaka ushauri wala nini nataka wengine mjue kuwa tuko tunaoishi na machungu tangu tunazaliwa mpaka tunakufa. Ukiona una furaha katika maisha yako basi ilinde furaha hiyo wengine hatuna bahati.

Asalam aleykum.
So sad
Ila hapo kwenye pombe na uchafu mwingine ndo utazidi kuiona dunia chungu. Ila fresh coz hutaki ushauri
Soon RIP
 
I wanted to say exactly that, ila nilihisi nakosa maneno ya kueleweka, unavishwa roho za kuonewa kukataliwa kudhulumiwa kudharaulika kutwezwa, nk
Hawezi kuona mpaka itokee afundishwe ni nini maana ya mambo haya na yanafanyikaje, unaibiwaje haki zako kiroho, sababu kuna kitu huwa wanafanya, wanaondoa ufahamu wako wa kuyatambua hayo mambo.Yaani ufahamu unavurugwa,nafsi unakuwa kifungoni unaishi kadri ya how they remote you.
na hiki ndo anachopitia ndugu yetu
 
Hapa ndipo nasemaga swala la Mungu ni myth.Haiwezekani binadamu wateseke afu eti tupo majaribuni na anatujua kabla hatujazaliwa.

Anasema tusimfate shetani.Lakini shetani ni kiumbe wake si amteketeze watu tule bata.

Pole bwana
Nimekata tamaa; Nimepigika, nimeteswa, nimedharauriwa, nimeumizwa , sasa Basi !

Ndugu zangu wana MMU kama ambavyo nimetanguliza hapo awali sina namna tena.

Dunia kwangu imekuwa chungu mno. Sioni jema wala.zuri katika dunia hii ya wanadamu. Pengine huko mbinguni aliko Mungu. Ili angalau nipate nafuu ya maumivu moyoni nawiwa kushare hapa.

Nimeumizwa sana na jamii. Kwenye siasa nimeumia sana. Kwenye jamii hivyo hivyo. Kwenye familia nina machungu makali mno. Kazini kwa moto kama kaa la mkaa wa mawe. Ndugu zangu mimi si lolote wala chochote kwao. Kifupi najiona thamani ya kuishi duniani haipo. Mwandishi wa Biblia kitabu cha Mhubiri alisema Duniani kila kitu ni upuuzi mtupu. Naungana naye kwa leo.

Ni hivi; katika makuzi yangu nilikulia mikononi mwa Mama yangu: alinilea kwa shida sana mimi na wadogo zangu. Nikiwa na miaka 9 nilianza kushirikiana na mama kutafuta kipato ili tupate japo mkate wa kila siku. Nilijishughulisha na kazi mbali mbali ikiwemo kilimo, biashara ya kuuza miwa, kuokota mavi ya ngombe na kuuza kama chanzo cha samadi, nimekata nyasi kwa ajili ya kuuzia watu wenye mifugo.

Wakati wote huo pamoja na maisha hayo nilikuwa na faraja maana siku zote mama yangu alitupa moyo mimi na wadogo zangu. Alipambana kila wakati na alidanganya hapa na pale ili tupate kuishi. Nakiri kabisa mama yangu hakuwahi kuwa mwizi wala kumuona akiwa na wanaume wengine kwa ajili ya kutafuta unafuu wa maisha. Baba yangu aliishi mjini na huko alifanya kazi ya kujiajiri na kuoa wake wengine na kutapanya mali.

Nikiwa na miaka 10 nilianza darasa la kwanza hadi nikamaliza form 4. Na nikajiunga na kidato cha kwanza hadi Elimu ya juu.

Wakati wote huo mimi nilikuwa mlezi kwa wadogo zangu na familia yangu kwa ujumla. Niliamini nitapambana hadi tufike mahali maisha yawe bora au atleast nafuu.

Sasa kazi ikaanza. Nikapata job nzuri ambayo inanilipa mshahara mzuri wa kuridhisha. Nikasema asante Mungu. Nitahakikisha wadogo zangu wote wanasoma na kufika pazuiri waliofeli nikawarudisha shuleni na wengine ku-resit mitihani yao. Alhamdulillah hawakuaniangusha wakafaulu nikawaendeleza vyuoni na sasa wengine wameahamaliza wana maisha yao.

Wengine wakawa wananidhihaki eti toka umefanya kazi una nini mpaka leo. Mbona hakuna ulichofanya cha kuendeleza maisha?? Nafsi yangu ikawa inaumia sana nikiona pesa nyingi nilizotumia kuwanyanyua wadogo zangu wa kike na wa kiume.

Kazini nilikuwa mchapa kazi Mkurugenzi wa shirika akanipa cheo kuwa msimamizi wa operasheni. Hapo ikawa kasheshe...wafanya kazi hawanisikilizi wala kutekeleza maagizo yangu. Mimi ni mkristo naamini katika kutenda haki sikuwahi kumwonea mfanya kazi yeyote. Nilifanya kazi kwa kuzingatia miongozo, kanuni, taratibu na ubinadamu. Pia. Nilijipambanua kuwa kiongozi bora lakini ikafika mahala baadhi ya wafanya kazi waliochini yangu kwenda kunisema kwa boss kuwa nawaonea( wafaya kazi hawa wana undugu na boss) nilifanyiwa kikao na Bodi ya wakurugenzi wakasikiliza malalamiko yao na hoja zangu. Wajumbe wa Bodi walikiri kuwa hawaoni Tatizo wala kasoro yoyote ktk utendaji wangu na kwamba malalamiko yaliyopelekwa na baadhi ya wafanya kazi wenzangu hayana msingi hapo nikapona.

Ikaja katika kundi la wateja yaani wapokea huduma zetu. vibwanga kila kukicha. Hata niwape huduma gani basi malalamiko chini kwa chini hayakosi. Wengine Wakinitolea maneno ya dharau pengine kwa mwonekano wangu wa upole na ushamba kidogo lakini kutokana na kazi yangu ya Wito nawiwa kuwa mvumilivu tu na kusonga mbele.

Mke wangu naye hivyo hivyo haoni kama nafanya chochote kwenye familia. Napewa maneno ya kashifa ya kuudhi na kejeli. Mimi silali mchana wala usiku natafuta maisha. Nafanya kazi kampuni nikitoka naunganisha kwenye kazi zangu binafsi ili kuongeza mpunga.

Wazazi wangu nao hivyo hivyo, nawasikia wakinisema wazi wazi vimaneno vya kejeli kuwa maisha yatanipiga. Ni kama wanafurahi au wanatamani yanipige na mimi sipo tayari kwa hilo labda Mungu mwenyewe akatae.

Huku kwenye mahusaiano ya kimapenzi naomba nisiguse kabisa hali ni mbaya mno. Mimi ni wa kuumizwa tuu. Sijui neema ya dunia hii. Wanafaidi wengine.

Ili ku-make maisha mazuri na kulinda afya yangu nilikataa kata kata kunywa pombe wala kilevi cha aina yoyote nilikataa mambo ya wanawake na utumwa wa mapenzi. Mapenzi yangu yoote niliwapa wadogo zangu. Kiukweli wadogo zangu hawa tisa(9) nawapenda sana. Huniambii kitu juu yao nimewalea toka wanazaliwa hadi sasa ni wakubwa wa mwisho yuko form four now.

Kwa kuwa nimefika mwishi sioni Jema wala zuri katika dunia hii sasa Basi! imekwisha.

Nataka nianze kufaidi pesa zangu mimi mwenyewe. Sitaki mtu anisemeshe. Mimi na maisha yangu. Binadamu nimewachoka. Nitakunywa Pombe mpaka nitapike. Nitavuta sigara mpaka mapafu yakome. Nitalala kwenye madanguro. Nitahonga sana. Nataka ku- neurtralize my sadness. Siwezi kuwa mimi ni wa uchungu tu maisha yangu yote. Siwezi kuwa mimi wa majonzi tu mpaka nife.

Lengo la thread hii sio kutaka ushauri wala nini nataka wengine mjue kuwa tuko tunaoishi na machungu tangu tunazaliwa mpaka tunakufa. Ukiona una furaha katika maisha yako basi ilinde furaha hiyo wengine hatuna bahati.

Asalam aleykum.
 
You are a great guy/person sikujui personally lakini nimekuelewa. Una maisha kazi nzuri etc shida yako kubwa na kinachokufanya uteseke ni tabia yako ya kuhitaji kuwaridhisha watu. Binadamu huwezi kumridhisha no matter how much u try. Hata kama ukichukua mshahara wako wote ukampa mama yako bado hautokua favourite wake. Zaidi atakulalamikia. Acha tabia ya kua people pleaser saidi kadri ya uwezo wako lakini usitegemee positive feedback. Hutopata kutoka kwa wafanyakazi wenzio, mkeo ndugu zako etc zaidi utaonekana bwege tu usie na akili badala ujenge/ ununue gari unawahonga wao. Ishi maisha yako, kua selfish kidogo, kua na boundaries. Kua disminder heshima itakuja. Binadamu hawana shukrani
Asipoelewa na hapa basi tena.

Sent from my Nokia 2 using Tapatalk
 
Acha hizo bana.
Kuendeleza wadogo 9 it's not a joke.

Sasa jiajiri, anza kidogo kidogo then ukiona unaenda vzr uachane na ajira.

Pombe na cigarette tulia kwanza, huko uendako mwisho utashindwa kusomesha wanao like your father.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo mwisho umemalizia vizuri kwamba sasa unakula bata la maana. Nafurahi umeligundua mapema. Binadamu hata umfanye nini haridhiki. Kumbuka self care is not selfish. Maisha ni haya haya tabu haziishi hadi unaingia kaburini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom