DOKEZO Nimekata tiketi VIP basi la Happy Nation, lakini halina huduma hadhi ya VIP. Naweza kulalamika wapi?

DOKEZO Nimekata tiketi VIP basi la Happy Nation, lakini halina huduma hadhi ya VIP. Naweza kulalamika wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
ametoa maelezo.sahihi swala la yeye kuwa na namba sio lazma
hapo ulipo sio namba zote unazo mfano namba za bank upatapo changamoto au dharula unayo?


punguzeni makasiriko ma agent uchwara
Tumia simu yako kupata namba zote muhimu, hauna haja ya kumuuliza mtu.
 
Sema wahuni, Uswahili sio dhambi. Ni waswahili pekee wanatumia neno mswahili kama tusi. Huu ujinga haupo kwenye race nyingine yeyote ile Duniani. Race zingine zote wanajiona wao ni superior huku waswahili mnawatukana wenzenu kwa kuwaita waswahili.
Ahsanteee sana mkuu wewe umetoka nje ya box.
 
Bongo hamna basi VIP
VIP ya Bongo ni Gari kuwa na milango miwili, siti 1x2, biskuti, pipi, maji na juisi(hivi hupewi vyote, vinatolewa viwili kati ya hivi)

Mimi huwa napanda daraja la kawaida au la kati tu kulingana na ninakoenda ambapo nauli inakuwa ni minimum recommended
 
Naona ulikua na pesa za kuspend mkuu. Sio mbaya mara moja moja kujilipua.

VIP bus sio kwa bongo hii.
 
Nimepanda Happy Nation( BUSINESS CLASS) la saa 10:00 kutoka Bukoba to Dsm kwa NAULI ya 120,000/.

Hilo basi halina AC na pia CHOO chake haki flush tunalazimishwa kuchimba dawa kwa KUJILIPIA hiyo huduma. Konda hana jibu la malalamiko yetu yote, likiwemo la kurudishiwa nauli inayobebwa na hiyo business class. Nani mhusika kwa sakata hii?

View attachment 2861202

Nijulishe na namba yake tafadhali.
Naona kuna ofa ya discount VIP hamnaga ofa, mmeyatimba
 
Kumradhi, niko nje ya mada ila ningependa kufahamu kwa nini vitu kama hivi bongo havipo?
Marcopolo_Paradiso_Mk7_G7_1800_DD_4axle_Bus_2017_1000_0001.jpg
Marcopolo_Paradiso_Mk7_G7_1800_DD_4axle_Bus_2017_1000_0002.jpg
 
Serikali naomba waondowe utararibu wa gari kusqfuri usiku, gari zisafiri kama zamani, madereva nao ni binadamu wanasinzia
 
Hata kimbinyiko ya Dodoma VIP nauli kubwa lakini hakuna udambwidambwi wa kupewa ukiwa huko tofauti na kawaida.

Sijui wanawainaje wananchi?
 
Wananchi amkeni mdai haki zenu, everything begins with you.

Mkiwa wengi hivyo watabadilika kuwafanya wajinga
 
bm dar moro aliwahi kuwa nayo
shabiby anazo dar dom
Nilipanda shabiby dar dom, si ile yemye choo ndani!? Ndio yale yale semi luxury tu, choo chenyewe kina limitations kibao, bafo kinakuwa kichaafu kinooma. Huku kwingine ni yale yale, siti watu wawili, hakuna wifi, hakuna lolote.
 
Latra Kuna upungufu wa elimu ya kujitambua na kuamua jambo walitakiwa kutambua hili

1. Xxx Transport company
💡Hapa n daraja la kawaida ambapo abiria hana haki ya kudai kitu extra Zaid ya kufika anapokwenda akiwa amekaa kwenye siti yake na basi liwe Zima na linajali muda ila latra hili daraja wanalichukulia kama n halali kwa magari mabovu yaan spana mkononi, chafu chafu halijali muda na kero kibao. Hapa kama basi Linachukua abiria 60 au 50 basi siti hzo hubaki hvyo hvyo.

2. Xxx Luxury bus company
💡Hapa nauli n Ile Ile ya daraja la kawaida ila mmiliki anaomba kupewa kubali Cha usafirishaji sababu atatoa vitu extra ya inavyotakiwa kama kinywaji, chakula, muziki, au tax baada ya kufika anapokwenda, hii kama bus linachukua abiria 50 basi Hilo halina haja ya kunguza siti Bali n huduma tuu ndio zinaongezeka

3. Xxx VIP bus service company
💡Hapa unalipa nauli zaidi hii ni kukurahisishia huduma zingine ambazo sio za usafirishaji kama kutoka nyumban mpaka kituo Cha kuanza safari, chakula, kinywaji, nafasi ya kulala ukiwa kwenye safari hii kama basi linauwezo wa kubeba abiria 50 basi siti zitapungua kuwa hata 35 Ili kutoa nafasi za kulala na kuwa huru kwenye siti

4. Xxx VIP bus service company
💡Hii inaenda mbele kabisa kuanzia kukata tiketi unakata tiketi ukiwa nyumbani kwako, wanakuwa na huduma yakuja kukuchukua sehemu ulipo ukiwa safarini unapata huduma za chakula Chochote unachotaka, kinywaji chochote unachotaka, burudani ya audio&Tv kulala uhuru wa siti na ukifika safari wanawajibika kuhakikisha umefika kwako salama. Hapa kama basi Linachukua abiria 50 basi siti zitapungua kuwa hata 30 lakin nauli itakuwa mara mbili au tatu ya kawaida.


Hii kitu inaweza kwenda sambamba na utoaji wa tiketi za kieletronic kwa maana ya hadhi ya basi na nauli husika nikimaanisha latra anavyokupa kubali wewe n VIP hvyo hata mfumo wa kulipisha anakuja system kwenye mashine Yako itoe nauli husika inayoendana na huduma husika.

Latra msiwe wajinga dhamana mliopewa ni kusimamia usafirishaji kwa pande zote mbili hvyo muwatetee abiria.
 
Hili Shalom sio Luxury ni la kawaida hao hiyo VIP wametoa wapi kwa gari viti vigumu utadhani vya Fusso..
 
Mimi sio Mswahili, kuzaliwa bongo sio lazima uwe mswahili. Kuna utamaduni kabisa wa Kiswahili. Kuna watu wanazaliwa bongo hawajuhi hata Kiswahili wala utamaduni wa Kiswahili.

Hongera mzungu/myahudi/muarabu mweusi yoda.
 
Back
Top Bottom