Nimekatwa Tsh 5,300 kuhamisha Tsh 50,000 kutoka NMB mobile kwenda M-PESA

Nimekatwa Tsh 5,300 kuhamisha Tsh 50,000 kutoka NMB mobile kwenda M-PESA

ile huduma siitaki yaani ni wizi mtupu na hata ukiwa unatoa m pesa nmb ada iko juu
 
nilihamisha hela toka bank crdb kwenda tigopesa... aisee kwenye elfu 11 walikata elfu 3 nikasemaa sirudiii tenaaa
Yaani unatoa 11,000 unakatwa 3,000?

Makato ni 27% that's bullshit asee! Au serikali inafilisika jamani?
 
Nilikuwa sijawahi kutumia hii huduma lakini sasa nilijaribu wiki mbili zilizopita na sikuangalia salio.

Muda huu nimepata bank statement kwenye email ndio naona hayo makato.

Tsh. 5,300 (NMB Tsh. 4,491.53 na VAT Tsh. 808.47) imenishangaza kukatwa zaidi ya asilimia 10 ya fedha niliyohamisha.

Hongereni sana NMB Tanzania
Sera za taasisi za kifedha kuhamisha fedha kutoka au kwenda taasisi nyingine kidigitali ni mbovu,Pole. Mimi pia niliwahi kuhamisha hela kutoka benki equity elf 5 kwenda tigo pesa nilikatwa elfu 3 na equity Bank . Siji kurudia tena bora nikatoe kwa [emoji763]
 
Asante mkuu. Shukran za dhati kuwa billionaire siyo mchezo.

Ila haya makato ni mzigo kwa mtanzania. Halafu serikali haijali. Bora angalau kungekuwa na tija katika haya makato. Sijui lini tutaendelea kama taifa. Yani hata sisi wabeba boksi ukituma hela homie reciever akipokea tu ya ni makato ya hatariiii.

Wakulaumiwa hapa ni Putin na Magufuli.
Bungeni wamejaa wao tu chama kimoja,hakuna hata upizani kutupazia sauti sehemu husika
 
Wapinzani walituchelewesha sana, alisikika mlevi mmoja akitoka baa!
 
Sera za taasisi za kifedha kuhamisha fedha kutoka au kwenda taasisi nyingine kidigitali ni mbovu,Pole. Mimi pia niliwahi kuhamisha hela kutoka benki equity elf 5 kwenda tigo pesa nilikatwa elfu 3 na equity Bank . Siji kurudia tena bora nikatoe kwa [emoji763]
Hizi benki ni wezi. Reasonable charges zingepelekea uwepo wa miamala mingi. In the long run wanapoteza na hizo huduma zitakufa.
 
Hizi bank zinatupelekesha zinavyotaka yani hawajali chochote. Wakiamua kupandisha transaction fee wapandisha tu wanavyojua. BOT kama regulatory body nao wamechill tu wavuja jasho tunaumia.

Hii nchi ni Shenzistan.
Hujui serikali ilianzisha tozo kwenye miamala ya benki?
 
Gharama za kuhamisha fedha Kati ya benki na mifumo ya simu ni mfano wazi wa failure ya regulation.
 
Yaani unatoa 11,000 unakatwa 3,000?

Makato ni 27% that's bullshit asee! Au serikali inafilisika jamani?
Na hapo kumbuka tu unahamisha toka Bank kwenda mitandao ya simu. Ukitaka kutoa ili upate cash pia kuna makato yake.
 
Kuna Azania Bank, ukifanya simbanking transaction unaweza kulia, sometimes inakubidi maana unajikuta mahali ambapo hakuna umoja switch atms au wakala na uko na shida ya mpunga
 
Attachments

  • Screenshot_20220802-153043_AzaniaMobilebankingApp.jpg
    Screenshot_20220802-153043_AzaniaMobilebankingApp.jpg
    36.6 KB · Views: 16
Kuna Azania Bank, ukifanya simbanking transaction unaweza kulia, sometimes inakubidi maana unajikuta mahali ambapo hakuna umoja switch atms au wakala na uko na shida ya mpunga
Hii inaonesha wamekubaliana mabenki yote kufanya huu utapeli.
 
Back
Top Bottom