Nimekoma kupiga mwanamke bora nimemwacha aende kwa amani., majuto ni mjukuu.

mwandende

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2017
Posts
11,848
Reaction score
22,392
Kila nikifikiria yaliyonikuta ktk maisha yng ya ndoa Miaka kadhaa iliyopita, najiona nilifanya uamuzi sahihi sana kumwacha aende kwa amani.
Nikiwa na umri wa miaka 25 nilibahatika kuoa msichana mmoja wa kitanga,,sijawahi kumpenda mwanamke kama nilivyompenda huyu binti wa kuitwa Mwanamkasi.
Baada ya penzi tamu la ndoa kama mwaka hivi ndy hapo nilipoonza kuona chungu ya ndoa...
Nilikuwa na kawaida ya kumpiga sn mara kwa mara kwa sababu ya usaliti ,ujeuri na ulevi , kutoka nyumbani bila kuaga anakwenda wapi,,
mara zote Mwanamkasi ananidai talaka lakini nashindwa kumwacha kwa sababu nilimpenda sn,,kwa kudhani kuwa nikimwacha siwezipata mwanamke mwingine kama yeye.

Siku moja narudi kazini nakuta mke wngu hayupo nyumbani,niliumia sn kwa wivu na hasira.
Nikasubiri kwa muda kadhaa,,
akarudi baadae sana usiku wa saa nne ,,halafu kaletwa na gari fulani hadi mtaa wa pili, tena akiwa amelewa sn..
kumbuka muda wote simu yake haipatikani,
Alipofika nyumbani namuuliza alipotoka hanyooshi maelezo zaidi ya kuleta majibu ya pombe na ulevi,.
Nilimrukia kichwa cha mbuzi usoni hata akadondoka kama gunia la nazi huku damu zikiruka kama bomba lililopasuka hata akapoteza fahamu ,,akawa amezima kabisa kama mfu,, ,,Nilipoona haamki baada ya dk kadhaa,,ikabidi nimwite baba nimweleze lile tukio..,,akamwangalia kwa makini baada ya huduma ya kwnza Mwanamkasi akaamka...
Baba akanambiya,,usipige mwanamke tena ktk maisha yko, wanawake wapo wengine wengi sn,utakuja kuua ufungwe maisha kwa sababu ya kijinga,kama mwanamke hataki kuwa na wewe usilazimishe..
mwache aende zake.. ndoa sio lazima wala sio lazima kuishi na yeye kama hakutaki..
Baada ya siku kadhaa nilimpa talaka Mwanamkasi.
Hii code ndy natembea nayo hadi sasa,,silazimishi mwanamke aishi na mimi au anipende...
Maisha ya ndoa ni safari ya hiyari,kama mmoja wenu kaamua kuacha ndoa wachaneni kwa amani.

Yale majuto niliyokuwa napitia kipindi Mwanamkasi bado amelala pale chini, nimajuto makali sn..
Nilisema kimoyomoyo huyu akiamka sipigi tena mwanamke maisha yng yote..
Niliona milango ya gerezani imeshafunguliwa na mimi nipo ndani gerezani natumikia kifungo cha maisha.

Leo imepita miaka 18 tangu nimwache mke wangu aende kwa amani.,
Bado naendelea na maisha yng nina mke na family ingine na yeye sijuwi hata alipo kwa sasa....
Tukubali kumwacha aende,, ili maisha mengine yaendele kwa uhuru na amani..
 
Toka divorce nilijipa muda kukaa alone, solitude ndio kipaumbele changu mpaka sasa. Wanawake nakua nao mara chache sana, na ni kama wanawake wa 5 hivi ndani ya katibu miaka miwili, na huwa ni gusa achia, wengi wamekua wakiniganda kiasi cha kuwa nalipwa pesa na wao (sijui ndio kuhonga au? Maana manzi anakutumia pesa tu bila sababu maana yake nini?), but sijawahi kuwa na moyo wa kukaa kabisa na hao viumbe for long term kwasasa. Usimgande mwanamke, hata usijaribu.
 
Kila nikifikiria yaliyonikuta ktk maisha yng ya ndoa Miaka kadhaa iliyopita, najiona nilifanya uamuzi sahihi sana kumwacha aende kwa amani.
Nikiwa na umri wa miaka 25 nilibahatika kuoa msichana mmoja wa kitanga,,sijawahi kumpenda mwanamke kama nilivyompenda huyu binti wa kuitwa Mwanamkasi.
Baada ya penzi tamu la ndoa kama mwaka hivi ndy hapo nilipoonza kuona chungu ya ndoa...
Nilikuwa na kawaida ya kumpiga sn mara kwa mara kwa sababu ya usaliti ,ujeuri na ulevi , kutoka nyumbani bila kuaga anakwenda wapi,,
mara zote Mwanamkasi ananidai talaka lakini nashindwa kumwacha kwa sababu nilimpenda sn,,kwa kudhani kuwa nikimwacha siwezipata mwanamke mwingine kama yeye.

Siku moja narudi kazini nakuta mke wngu hayupo nyumbani,niliumia sn kwa wivu na hasira.
Nikasubiri kwa muda kadhaa,,
akarudi baadae sana usiku wa saa nne ,,halafu kaletwa na gari fulani hadi mtaa wa pili, tena akiwa amelewa sn..
kumbuka muda wote simu yake haipatikani,
Alipofika nyumbani namuuliza alipotoka hanyooshi maelezo zaidi ya kuleta majibu ya pombe na ulevi,.
Nilimrukia kichwa cha mbuzi usoni hata akadondoka kama gunia la nazi huku damu zikiruka kama bomba lililopasuka hata akapoteza fahamu ,,akawa amezima kabisa kama mfu,, ,,Nilipoona haamki baada ya dk kadhaa,,ikabidi nimwite baba nimweleze lile tukio..,,akamwangalia kwa makini baada ya huduma ya kwnza Mwanamkasi akaamka...
Baba akanambiya,,usipige mwanamke tena ktk maisha yko, wanawake wapo wengine wengi sn,utakuja kuua ufungwe maisha kwa sababu ya kijinga,kama mwanamke hataki kuwa na wewe usilazimishe..
mwache aende zake.. ndoa sio lazima wala sio lazima kuishi na yeye kama hakutaki..
Baada ya siku kadhaa nilimpa talaka Mwanamkasi.
Hii code ndy natembea nayo hadi sasa,,silazimishi mwanamke aishi na mimi au anipende...
Maisha ya ndoa ni safari ya hiyari,kama mmoja wenu kaamua kuacha ndoa wachaneni kwa amani.

Yale majuto niliyokuwa napitia kipindi Mwanamkasi bado amelala pale chini, nimajuto makali sn..
Nilisema kimoyomoyo huyu akiamka sipigi tena mwanamke maisha yng yote..
Niliona milango ya gerezani imeshafunguliwa na mimi nipo ndani gerezani natumikia kifungo cha maisha.

Leo imepita miaka 18 tangu nimwache mke wangu aende kwa amani.,
Bado naendelea na maisha yng nina mke na family ingine na yeye sijuwi hata alipo kwa sasa....
Tukubali kumwacha aende,, ili maisha mengine yaendele kwa uhuru na amani..
Kumuacha aende kama huna hela ni sawa tu,ila kama una semi 29 ziko barabarani ni kazi sana,hapa ndio unamuona mwanaume mwenzako anakonda na mapresha juu huku akiendelea kuvumilia mateso au mwisho wa siku anachukua maamuzi magumu,omba sana haya maisha Mungu akujalie mke mwema...
 
Mpaka sasa pia bado unastahili kwenda gerezani kwa makosa uliyoyafanya huko nyuma. Omba sana asisome comment yangu hii maana wastahili kwenda gerezani kwa ukatili wako...

Hakika hukufanya ubinadaamu pale ulipoona mambo hayaendi sawa. Tukio hilo sio tuu kumuumiza mhusika bali hata wewe pia kiasi flani litakuumiza kihisia kwa jambo la hatari ulilofanya bila kitaraji.

Upendo na mwanga vikuongoze
 
Hakuna mwanamke anataka aende na mali zko zote, zaidi ya kudai talaka na mgawane mali..tena zile ambazo mmechuma pamoja
 
Mpaka sasa pia bado unastahili kwenda gerezani kwa makosa uliyoyafanya huko nyuma. Omba sana asisome comment yangu hii maana wastahili kwenda gerezani kwa ukatili wako...

Hakika hukufanya ubinadaamu pale ulipoona mambo hayaendi sawa. Tukio hilo sio tuu kumuumiza mhusika bali hata wewe pia kiasi flani litakuumiza kihisia kwa jambo la hatari ulilofanya bila kitaraji.

Upendo na mwanga vikuongoze
Kwni kupiga mwanamke ni mimi wa kwnz?
Hakuna jinai kwenye kupiga mkeo,,
Nimefanya vyema kuachana nae kuliko angeendelea kunisaliti na kunitendea mambo ya hovyo
 
Ngoja nikufundishe kitu ndugu maana unaonekana wew ni maamuma mkubwa wa Sheria na ustaarabu hasa unaposema hakuna jinai kumpiga mkeo.

Huna mamlaka wala haki ya kunyoosha mkono wako na kumpiga binadamu yeyote hususani mkeo Kwa kigezo cha ndoa.
Ndoa sio biashara ya ulanguzi wa binadamu , kwamba ukishatoa kimahari chako basi unamamlaka kamili juu ya binadamu mwenzio. La hasha !, mwanamke anahaki na hiari ya kuamua kile anataka juu ya mwili wake na maisha yake as long as havigusi utu wako kama binadamu na sio kama mme.Na ukiona hakufai muache aende zake..Ulipaswa kua jela Kwa kipigo ulichompa
 
Back
Top Bottom