Nimekoma walahi! Pilau la buku nimelinunua kwa 32,000 za dripu mbili

Usipendelee kula vyakula vya bei chee hasa uswahilin.
Ni bora nishinde njaa ila maeneo haya ya uswazi nitatafuta atleast hotel inayoeleweka ndio nile kama nimebanwa sana.
 
Ukiendelea kujilegeza hapo hospital utapigwa drip hata 5 .
 
Nipo Kaka ,sema siku mbili hizi nilikuwa mpakani huko niliipata mteja wa vidonge vya Arvs ikabidi nimpelekee Kaka nisije kufa njaa kwa watu huku
Ah sawasawa mzee mapambano tu. Muhimu siku zinakwenda kidogokidogo hivyohivyo. Mpakani kuna fursa gan huko? Vijana wana mitaji humu hawana exposure wanang'ang'ania dar alaf haiwalipi.

Fursa fursa huko shea nao wa kujilipua wajilipue tu
 
Hapo mchawi anaweza kuwa Pilau (limechacha kisha likafufuliwa kwa kupikwa upya kwa madiko diko mengine ili kukata mchacho) au hiyo Juice ya miwa (maana usafi wake huwa ni mgumu).
Juice ya miwa napenda ila nawazaga sana wanavyokamua pale na ile mchanganyo na barafu..ila pia kweli hali ngumu , sasa misosi ya buku au msosi chini ya 2000 sh lolote linawezekana ..nyama kwasukwasu, nyanya kwasu, mchele ovyo..kula vya jana vilivyochanganywa na vya leo..ndo mana madiko diko huwa mengi ili kuficha mambo ya radha na harufu
 
Hii kama Mbagala nini pale fremu za kanisa la RomaπŸ˜†πŸ˜€πŸ˜€πŸ€£
 
Kipato kikiwamba mkuu unajishindilia tu πŸ˜‚
Hapana hapana mdogo angu. Umeona sasa matokeo yake.. ulishindwa bas hata kuomba upimiwe chips za 1500 zimetoka jikon unywe na Afiya au maji ya 500???
Kuna time lazima ujipe thaman bila kujali hali ulionayo.
Mtaji pekee wa masikin ni afya.
SIchezagi michezo ku mess up na afya yangu.
 
Juisi za miwa usafi sio standard japo uchafu ule sio wa kukera au kumpeleka mtu kitandani. Lakin pale kuna muingiliano mkubwa sana na wadudu hasa nzi wa njano na usafi wa miwa au mashine. Mana mashine zinalala nje na miwa haioshwi inaparwa tu
 
Hii kama Mbagala nini pale fremu za kanisa la RomaπŸ˜†πŸ˜€πŸ˜€πŸ€£
Ushaanza sasa! Sijaja kuharibu biashara ya mtu mkuu. Unapita pita mazingira yale? Mm pale njia yangu kila siku naishi hapa chini ya kanisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…