Nimekoma walahi! Pilau la buku nimelinunua kwa 32,000 za dripu mbili

Nimekoma walahi! Pilau la buku nimelinunua kwa 32,000 za dripu mbili

Kuna gf wangu, wife material anakaa kona hizi akanipa mbinu moja siku hiyo tukanunua pilau zakiem pale la buku 2 na matunda. Kufika geto likanishinda. Akalipigilia likabaki akanambia majirani hili hawalikatai. Kawaita wakaja kulibeba.

Nikaskia wanapiga bajeti ya juisi moja moja pilau tayari lipo 😂
Mbagala hii kawaida sana.........Mbagala ndio sehemu pekee ndani ya Tanzania buku 10 unaweza toboa wiki
 
Hapana hapana mdogo angu. Umeona sasa matokeo yake.. ulishindwa bas hata kuomba upimiwe chips za 1500 zimetoka jikon unywe na Afiya au maji ya 500???
Kuna time lazima ujipe thaman bila kujali hali ulionayo.
Mtaji pekee wa masikin ni afya.
SIchezagi michezo ku mess up na afya yangu.
Sawa mkuu
 
Hali hii leo mbona kazi ipo!

Katika pitapita zangu maeneo flani flani hiv nikasikia sauti kutoka katika kipaza ikinadisha "pilau buku, pilau nyama buku... njoo ujipatie". Nikaona yesss, dunia ni yetu sote.

Nikajikoki pale ndizi ya mia mbili na juisi ya muwa. Nikaketi taratiibu nijipimie. Wallahi punde baada ya kujishindilia pilau la nazi nikasikia "prrr prrrr prrr" tumbo linaunguruma na maumivu kias.

Nikajaa kujishtukia niko mlangoni mwa choo cha msikiti mana hata nauli iliishia kwemye choo cha kulipia. Nikajimaliza pale vya kutoshana nguvu ikatoweka, nikaomba msaada wa pikipiki ya msikiti nikapelekwa hospitali. Hapa nilipo nina drips ya pili na nishamaliza elfu 32 kwa matibabu haya yanayoendelea

Dua zenu wazee
Pole Sana utapona
 
hilo limebaki kwenye masherehe na migahawa mikubwa ni kwajili ya nguruwe sema baadhi hulichepusha na kuliuza kwa buku limetembelewa na mende wa chooni kijana wangu
Kuna tabia nyingine kuzidhibiti ni ngumu mana zimefungamana na umaskini. Sasa hiyo si ni kama kuuza mifupa ya kuku? Ulishwahi kuona mapaja ya kuku yamenyonyogwa yanakaangwa na kupangwa fungu?
 

Attachments

  • images (9).jpeg
    images (9).jpeg
    9.6 KB · Views: 3
Jamani tunaweza kulaumu pilau kumbe tatizo juice ya muwa,zile juice zinasagiwa sana nzii....
Nzi hana tabu yoyote yule akisagiwa anakutana na tangwizi mule na ndimu kwisha kaz. Pilau linabakia kila siku na halimwagwi 🤣
 
Back
Top Bottom