Nimekonda sana, naomba ushauri nifanyaje nirudishe kilo zangu haraka

Nimekonda sana, naomba ushauri nifanyaje nirudishe kilo zangu haraka

Happy new year beautiful people.

Dear nutritionists mlioko JF naomba mnishauri diet itakayonisaidia kurudisha kilo zangu zilizopotea.

Nimekonda hadi nahisi watu wanahisi nina umeme(God forbid).

NB: Siumwi chochote na kila miezi 6/mwaka huwa nafanya general health check up ikijumlisha ini, figo, moyo, kansa ya mlango wa kizazi na matiti.(Ni kautamduni tu nimejiwekea)

Natanguliza shukrani
Hakikisha unafanya mapenzi mara moja kwa week ,pata soda moja kila unapopata launch,hakikisha huvuki mlo usikose vitamin b complex kidonge kimoja daily kwa mwezi
 
Pole sana.
Ushauri achana na vikoba na mikopo ya kausha damu Kama uno humo

Pia Kama we ni kamwanamke kalevi punguza pombe au kula sana kabla ya kubugia kamunyweso.

Kingine we Kama ni mkazi wa daslam epuka kula matembele na matumbo mabichwa na magulu za kuku. Jitaidi ukule samaki wa mwanza Kama sato na kamongo yasinda nyama ndani ya mwezi tu utajua mnene Kama msechu
Vikoba navisikia tu mkuu.
Matembele nayapenda tatizo no appetite na yenyewe nalamba tu siku hizi.
Hizo vitu zinginge sivijui mkuu.
Asante na Mungu akubariki kwa ushauri mkuu🙏
 
Pole
Una appetite?
Saga lishe kama ya mtoto Ile weka ulezi,korosho,mahindi, lozi na iliki
Uwe unapika uji unakunywa uweke na siagi na maziwa

Utengeneze smoothie zenye maziwa na matunda tofauti ila ndizi mbivu isikose
Kula sana ila zingatia balance diet maana unaweza ukafumuka vibaya sana

Ila pia hakikisha hela unayo maana kama huna hata ukinywa mafuta kila siku hutonenepa ng'o
Finallly numepata ushauri.
Appetite sina ila vimiminuka vinapita labda hiyo lishe itapita pia.
Barikiwa kipenzi nitazingatia.
 
Watu wanatoa ushauri wa kipumbavu ambao hawajaombwa. Yeye kaomba namna ya kunenepa. Wapuuzi wanamwambia acalculate body index au wanataka kujua body index. Hayo hajawaambia. Mnachemka sana kuelezea kitu ambacho hajaomba. Kaomba jambo jingine mnaleta ujuaji wa kishamba. YEYE ANATAKA KUNENEPA. PERIOD.
Kunenepa that's it mkuu.

Btw, unajitambua sana mkuu.
Zidi kubarikiwa
 
Back
Top Bottom