Nimekonda sana, naomba ushauri nifanyaje nirudishe kilo zangu haraka

Nimekonda sana, naomba ushauri nifanyaje nirudishe kilo zangu haraka

Happy new year beautiful people.

Dear nutritionists mlioko JF naomba mnishauri diet itakayonisaidia kurudisha kilo zangu zilizopotea.

Nimekonda hadi nahisi watu wanahisi nina umeme(God forbid).

NB: Siumwi chochote na kila miezi 6/mwaka huwa nafanya general health check up ikijumlisha ini, figo, moyo, kansa ya mlango wa kizazi na matiti.(Ni kautamduni tu nimejiwekea)

Natanguliza shukrani
Iseme sabab ya kukonda kwanza ndio tujue tunatatua tatzo kwa njia gan
 
kunywa juisi ya ndizi iliyochanganya na maziwa korosho na karanga kila siku glasi moja kwa muda wa wiki mbili . itarudisha kilo zako zilizopotea
 
Asanteni nyote kwa michango yenu.Mlotoa ushauri nitazingatia.

Kuna waloniambia bila maokoto siwezi kunenepa hata nile nini hivyo naomba ni log off nikatafute maokoto.
Niwatakie siku njema wakuu.
📌📌
 
Haya maisha kila mtu anahangika na yake. Binafsi sijawahi kunenepa, maisha yangu yote ni mwembamba tu mpaka nishajikatia tamaa.
Ila kipindi nasononeka kwanini sinenepi walau kidogo kama wenzang, kuna jamaa angu wa karibu sana yeye alikuwa ana struggle kupungua. Jamaa alikuwa na uzito zaid ya 100kg. Kapambana sana na madawa, diet, mitishamba, kaharisha sana, tumekunywa sana visungura kumsaidia kuchoma mafuta lakini wapi... ndio kwanza kapungua kilo 5.
Sasahivi tumeamua liwalo na liwe!!
 
Yes tatizo nakula kidogo sana no appetite.
Muda wa kulala na kupumzuka ninao wa kutosha.
Stress za kawaida za kutafuta hela
Basi umeshajua undani wa tatizo lako ni kukosa hamu ya kula... jitahidi ule vizuri na upunguze mawazo.

Binafsi huwa napungua kila ninapokuwa na changamoto za upungufu wa fedha...

Na ukiona nimepatapata kamwili basi ukichungulia akaunti yangu lazima unakuta ina vimilioni milioni ....na kinyume chake huwa hivyo
 
Back
Top Bottom