Nimekonda sana, naomba ushauri nifanyaje nirudishe kilo zangu haraka

Nimekonda sana, naomba ushauri nifanyaje nirudishe kilo zangu haraka

Happy new year beautiful people.

Dear nutritionists mlioko JF naomba mnishauri diet itakayonisaidia kurudisha kilo zangu zilizopotea.

Nimekonda hadi nahisi watu wanahisi nina umeme(God forbid).

NB: Siumwi chochote na kila miezi 6/mwaka huwa nafanya general health check up ikijumlisha ini, figo, moyo, kansa ya mlango wa kizazi na matiti.(Ni kautamduni tu nimejiwekea)

Natanguliza shukrani
Hii check hapo vipimo vyote ni bei gani
 
kunywa juisi ya ndizi iliyochanganya na maziwa korosho na karanga kila siku glasi moja kwa muda wa wiki mbili . itarudisha kilo zako zilizopotea
Asante kwa ushauri mkuu🙏
 
Haya maisha kila mtu anahangika na yake. Binafsi sijawahi kunenepa, maisha yangu yote ni mwembamba tu mpaka nishajikatia tamaa.
Ila kipindi nasononeka kwanini sinenepi walau kidogo kama wenzang, kuna jamaa angu wa karibu sana yeye alikuwa ana struggle kupungua. Jamaa alikuwa na uzito zaid ya 100kg. Kapambana sana na madawa, diet, mitishamba, kaharisha sana, tumekunywa sana visungura kumsaidia kuchoma mafuta lakini wapi... ndio kwanza kapungua kilo 5.
Sasahivi tumeamua liwalo na liwe!!
Hongereni kwa kukubali matokeo mkuu
 
Mapenzi yana tabia ya kumfanya mtu awe skeleton ukikaa kizembe
Nipo home this holiday , bi mkubwa kidogo Ako na sensi of huma .. Nimefika 23rd last year Dec , nilibaki kongoro/tuu .. baada ya mapocho pocho ya Mama mzazi na kupata wasaa wa kupumzika .. juzi kanichokonoa kanambia mapenzi yatakuua mbwa wewe Mimi ni mzazi najua... Ona umeanza kunawiri

ULICHOSEMA KWELI MAPENZI KONYO
 
Basi umeshajua undani wa tatizo lako ni kukosa hamu ya kula... jitahidi ule vizuri na upunguze mawazo.

Binafsi huwa napungua kila ninapokuwa na changamoto za upungufu wa fedha...

Na ukiona nimepatapata kamwili basi ukichungulia akaunti yangu lazima unakuta ina vimilioni milioni ....na kinyume chake huwa hivyo
Nitajitahidi mkuu.
 
Back
Top Bottom