Usiingize pesa kwenye mradi wa mwanamke, ungekuwa na ndoa naye sawa lkn sasa ukitoa iwe umempa tu kama sapoti ya kirafiki lkn usiweke pesa yako kama kitu chenu wote.
Waogope sana wanawake kwenye vitu vyao...ipo siku utanielewa
kuna mda anakuwa mzito nikimpatia ushauri zaidi kuhusu ujenzi.
Karibu mkuu. Nakutakia kila la kheri ikibidi mfikie hatma nzuri ya kufunga ndoa na kujenga familia pamoja.Shukran sanaaa boss, umenipa ushauri wa kina. Kwel kuna mda najisikia low hasa tukijadili mipango ya mda mfupi ambayo mwishoni inataka pesa. Ila kuna mda anakuwa mzito nikimpatia ushauri zaidi kuhusu ujenzi.
Nguvu na pesa. Jenga nyumba hio.Asante kwa ushaur boss. Na io nyumba vipi? Yan ni play kivipi hapo? Tuchangie nguvu tu au na pesa?
Hata akiwa mke ukijenga kwenye kiwanja cha mkeo hiyo nyumba ni yake si yenu, utafute kiwanja mwanaume mjenge yenu na mkeoPia akumbuke huyo ni mpenzi wake tu sio Mkewe.
Hivyo hicho kiwanja na Nyumba inayojengwa ni ya mwanamke.
Anhaa kama ni ivo mkuu na kama mna malengo ni ishu ya makaratasi tu, akubali kuthihitisha kua nyumba ni yenu wote yaani asiandikie jina lake peke ake. La sivyo basi anataka kukutumia kama ngazi.Alisema tupambane tukamilishe nyumba alafu tuanzishe familia ila Kuna mda vitu vidogo vinapelea na nipo karibu mafundi wakinicheki inakuwa mtihani kwamba nifix au nimwambie Ila kipato chake ni kikubwa Sanaa kufananisha na changu, ushauri wako ni mzuri asante boss.
Hupendi kula kuku na kifaranga chake huku mkipiga mapicha ya uchi na kujibandika mtandaoni?Unataka kunipa mabomu mzee😂
Hapana mkuu kubomoa kesi😀 labda niichome moto bahati mbayaa. Ila ushauri wako nimeupokeaMkuu usiweke hata 50 yako hapo! Wewe jenga kwako kama kuoana aje kwako...enda uweke pesa yako hapo halafu utakuja utuambie mwanaume ndie kichwa!utapelekeshwa ubaki kichwa tu...au aje aolewe kwingine utaenda ubomoe?
Chai ya baridi sanaaa hiiNatumaini ni wazima wa afya na poleni na majukumu.
Niingie kwenye mada.
Mimi ni mwanaume nina miaka 24, najishughulisha na kazi binafsi Ila bado kipato changu sio kikubwa. Miezi michache iliyopita nilifanikiwa kuwa na mahusiano na binti mrembo na muonekano wake ni kama ana miaka 20 hivi.
Nilimueleza ya moyoni akanielewa saivi tupo kwenye mahusiano. Sikujua kumbe binti ana kazi nzuri ameajiriwa na kaka yake na kipato kikubwa tu anapata. Miaka yake ni 26 Ila kimuonekano ni mdogo, juzi kanambia tuende mahali kumbe ni kununua materials ya kupeleka site, kumbe ana eneo na nyumba msingi umeanza.
Tukienda mahali hata pesa za manunuzi ananikabidhi na akiwa busy ananiomba nikasimamie mafundi. Nashindwa kuwa na ujasiri wa kuchangia ujenzi naomba ushauri halafu pia wakuu hili ni zali au nikimbie tu nimuache na projects zake.