- Umekuwa hadimu kwangu.
- Mbona umepotea?
- Huko kwenu kuna NG'AMBI? (watokao Tanga nadhani wanajua ng'ambi)
- Siku hizi umetawishwa? au unasingwa?
- Umekuwa nyota ya Jaha!!
cc. Amavubi
Lokissa
Nyani Ngabu
Lokissa
Mkereketwa_Huyu
Chum Chang
Kingmairo
Unasema hivyo hivyo "nimekumiss".
Siyo lazima kila neno, sentensi, au msemo wa Kiingereza uwe na tafsiri yake ya moja kwa moja kwa Kiswahili.
Kama police ni polisi, judge ni jaji, schule (Kijerumani) ni shule...basi sioni ubaya miss isiazimwe kama hivyo hivyo ilivyo.
Mh, kutamani tena?
Kutafsiri hakuhusu maneno tu, kunahusu tamaduni nzima.
Muingereza akisema "I married my husband in 1983." ukaambiwa utafsiri sentensi hiyo Kiswahili utaitafsiri vipi?
Hivi we Kiranga mbona kila siku maswali tu?! Saa ingine na wewe uwe unaleta solutions... siyo maswali tu. eeh!
Katika Socratic method hata solution italetwa kwa swali. Unaweza kuona swali katika jibu, na jibu katika swali.
Haya bwana, ingalau hapo umejaribu kuleta solution--hata kama ni kwa kutumia Confucius method.
"Mapinduzi Daima" kama TVZ inatema Hegelian dialectics.
Hakuna jibu lisilozaa swali.
Hii imekaa vizuri: Banda lishavunjika, jogoo kaondoka. Vifaranga hangaika, kumtoa nyoka.
Tembe apiga vijembe, kama jeshi liso sembe...
Sasa mkuu! Tukilazimisha au kuliazima hilo neno kwa kiswahili liwe "nimekumiss" huoni kama tutakuwa tume "codemix" badala ya kutengeneza neno sahili kama SHATI kutoka neno SHIRT?
Na ikiwa limekubalika liwe nimekumiss, semantically litakuwa na maana gani kwa lugha ya kiswahili?
Kwani kuna ubaya gani tuki "codemix" kama unavyodai? Mbona sasa hivi tunafanya sana na bado tunaelewana tu. Kwani kwa mfano inaposemwa 'spika (speaker) wa bunge' kunakuwa hakuna codemixing? Au shule (schule - Kijerumani) ya sekondari (secondary), kunakuwa hakuna codemixing hapo?
Maana zinaweza zikawa kadhaa kulingana na muktadha kwani hata kwenye Kiingereza neno 'miss' lina maana tofauti tofauti kulingana na muktadha.
'Miss Becky Lindsey' sio sawa 'miss the boat'.
Na ili lugha ikue ni lazima watumiaji wake waikuze.
Ila, si lazima kila neno la msamiati wa hiyo lugha liwe linatokea kwenye lugha hiyo tu. Kuazima (na hata kufanyia modification za hapa na pale) kunakubalika kabisa.
awali nilidhani inaweza kuwa nimekukumbuka, lakini nahitaji msaada zaidi ili nisidhani tena