Nimekubali kuachwa tena

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]daaah aiseeee
 
Kwa maelezo yako,
Unaonekana una MDA mrefu Sana na Kwny mahusiano nae.

Afu unakuja kutwambia,
Mwanamke wako hajawai kula hata Mia yako mpk mnaachana,

Hivi unataka tukueleweje,
wkt mwanamke yeye ndiye anafanya biashara wewe upo upo TU umezubaa.

Kisha,
Unakuja kulalamika mwanamke Anatabia ya uchoyo na umimi Mimi,

Na hakuna mahali umetwambia uliwahi msaidia chochote Cha kumboost kiuchumi mwanamke wako,

Sasa mkuu,
TUKIKUITA MARIOO TUTAKUA TUMEKUONEA?
 
Kupitia Uzi wako,
Umetoa code zako Mwnyw tukujue wee Ni mtu wa namna gani.

Ndo Maana wkt nachangia nakuita marioo,
nilikua naquote kabisa misemo yako Kwny Uzi husika.

Haihitaji degree kabisa kujua pale kwa yule mwanamke ulikua unalelewa[emoji4]
Okay soma tag ya hapo juu,
 

Kama ni kombora, hili limedondokea capital.
 
Kaka mkubwa, SIWEZ I WEKEZA PESA ZANGU KWA MDADA AMBAE SINA IMANI NAE ASHANIACHA KABLA NA NISHATUMIA PESA ZANGU, KUANZA KUWEKEZA PESA NOW NI MAPEMA SANA, MAHUSIANO NDO KWANZA YANA MWEZI MMOJA NA KIDOGO ,ITS TOO EARLY BROO

SIJAWAHI KULA HATA MIA YAKE ELEWA HIVO
 
Naungana na DeepPond mtoa mada ni wale ma marioo wapenda vitonga wanaopenda sex life kuliko kuwaza watakua vipi bora zaidi ya leo.
Mwanamke wake kampita mbali kiupeo, Ni Aina flani ya wanawake wako matured and focused kimaisha na kimahusiano.

Mtoa mada alikua anampotezea muda na kumfuja dada wa watu TU[emoji4]
 
Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu,

Mwanzoni kabisa mwa Uzi wako,
Kuna mahali nilikuuliza the same question,

Kumbuka alinijibu humhudumiagi kwasababu yeye Ni mwanamke wa kuclear bills.

Yaani ushazoea mkishakula, wakulipa bills Ni yeye.

Tunakuelewaje Sasa, unakua unaenda mbele unarudi nyuma mkuu[emoji848]
 
Ndugu mtoa mada
Una tatizo mahali, Tena kubwa Sana kwa mfumo unaokwenda nao kimahusiano.

Na usipojirekebisha haraka na ukadhani sisi tunaokwambia ukweli tunakuchukia,

Utajikuta unaishia kufedheheshwa Sana na wanawake zako, na mahusiano yako yatakua magumu Sana.

Ni kweli "hayana muongozo" Kama navyojisemeaga ndugu yetu Smart911

Ila Kuna vitu Kama mwanaume Lazima uviepuke sana, navyo Ni Kama

1. kumlala mwanamke ukamuacha mikono mitupu, ile Ela ya Asante inakujengea heshima sana Kama ulikua hujui.

Hata Kama Ni ndogo Kia's gani, ila unahesabika umetoa shukrani

2. Kwenda Kwny matumizi ukaitegemea Ela ya mwanamke kuclear bills.

Tambua wanawake wanapata Ela ktk mazingira magum sana tofaut na sisi, (unyanyasaji,udhalilishaji, kufedheheshwa n.k) hata Kama mnafanya kazi Aina moja.

Hasa uyo wako anayefanya biashara.

Kwaiyo pesa yake
tambua ameisotea kwa jasho na damu,
na huna mamlaka nayo, isipokua kwa hiari yake.
Nako hiari iwe Ni Mara moja moja tu. Usiruhusu iwe ni maZoea.

Simamia wajibu wako Kama mwanaume wako umhakikishie usalama wake kiuchumi,kimwili na kijamii popote pale anapokua na wewe.

3. Kuvipa vipaumbele vitu vya muhimu Ila sio visivyo na msingi Kwny mahusiano,

Mf: kupenda kutamkiwa unapendwa kila mara, kupigiwa Simu kila Mara, n.k

Mwenzio anafanya kazi,
Yanini umpigie pigie Simu na sms ovyo umtake akwambie anakupenda,

Kwani asipokwambia anakupenda wee huwez gundua unapendwa?

4. Kua na matarajio hasi unapoingia Kwny mahusiao na mtu aliekuzidi umri

-Ondoa kabisa mawazo ya kwamba kakaribia miaka 30 kwaiyo kaja kwako kutafuta ndoa na mtoto,

kwani kuoa Unaeweza kuoa ni wewe peke ako TU?
Hizo hizo shahawa za mimba unazo peke ako TU?

Kwanini hajaenda kwa wengine, Yuko na wewe?

Hebu jitahidi kua positive minded unapoanzisha mahusiano yoyote yale ubongo wako uwe free.

5. Kuwasema vibaya wanawake zako punde TU mnapoachana,Hii sio tabia nzur hata kidg.

Kumbuka ulishatwambia mlishaachana mkarudiana, Sasa vipi Tena mkija rudiana?

Maana ake utakua umerudia kula matapishi yako mwenyewe au?

Huoni kwa matatizo yote uliyomsemea vibaya, ukija kurudiana nae utakua umejivua nguo zako wewe mwenyewe?

Hebu epuka uadui usiokua na kichwa Wala miguu na wanawake zako, huwezi kuijua kesho yako au ya mwenzi wako.

Hii duniani Ni tambala bovu mkuu, Zingatia ayo kwanza.[emoji848]
 
Mwanamke wake kampita mbali kiupeo, Ni Aina flani ya wanawake wako matured and focused kimaisha na kimahusiano.

Mtoa mada alikua anampotezea muda na kumfuja dada wa watu TU[emoji4]
Lakini kuliwa ni haki yakee[emoji23][emoji23]
 
Unachosema ni sahihi ,LAKINI hizo bills ana clear akiwa yeye na wenzake sio tukiwa wote, sijui kama unanipata mkuu[emoji23][emoji23] yeye bill ana clear sawa lakini akiwa huko sio akiwa nami na ndo utaratibh wake
 
Noted.

Anyway nimekusikia kaka, ila naona kama umeona mabaya yangu tu na point zangu nazotoa sion kma kuna yeyotee unaunga mkono, sawaa
 
Hii comment umelengeaa Marioo na mie sio Mario nafikiri itanufaisha watu wengine
 
Noted.

Anyway nimekusikia kaka, ila naona kama umeona mabaya yangu tu na point zangu nazotoa sion kma kuna yeyotee unaunga mkono, sawaa
Honestly,
Japokua story yako Ni ya upande mmoja.
(Yaan Sijamsikiliza mwanamke)

Siwez kukuficha,
umejikaanga mwenyewe, kwa mafuta yako mwenyewe

Mwanamke wako Yuko 100% true,

Na kingine cha kukushaur, japo sio cha lazma sana.

Kama Unaweza,
mrudie haraka Sana uyo mwanamke wako.

She's a very good wife material kwa kizazi hiki tulichonacho Sasa,

Nakuhakikishia mkuu,
Uyo mwanamke akija KUPATA mtu anayeweza kufunika Yale madhaifu yako kwake, Utaona mabadiliko ndani ya MDA mfupi sana.

TRUST ME[emoji4]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…