Ndugu mtoa mada
Una tatizo mahali, Tena kubwa Sana kwa mfumo unaokwenda nao kimahusiano.
Na usipojirekebisha haraka na ukadhani sisi tunaokwambia ukweli tunakuchukia,
Utajikuta unaishia kufedheheshwa Sana na wanawake zako, na mahusiano yako yatakua magumu Sana.
Ni kweli "hayana muongozo" Kama navyojisemeaga ndugu yetu
Smart911
Ila Kuna vitu Kama mwanaume Lazima uviepuke sana, navyo Ni Kama
1. kumlala mwanamke ukamuacha mikono mitupu, ile Ela ya Asante inakujengea heshima sana Kama ulikua hujui.
Hata Kama Ni ndogo Kia's gani, ila unahesabika umetoa shukrani
2. Kwenda Kwny matumizi ukaitegemea Ela ya mwanamke kuclear bills.
Tambua wanawake wanapata Ela ktk mazingira magum sana tofaut na sisi, (unyanyasaji,udhalilishaji, kufedheheshwa n.k) hata Kama mnafanya kazi Aina moja.
Hasa uyo wako anayefanya biashara.
Kwaiyo pesa yake
tambua ameisotea kwa jasho na damu,
na huna mamlaka nayo, isipokua kwa hiari yake.
Nako hiari iwe Ni Mara moja moja tu. Usiruhusu iwe ni maZoea.
Simamia wajibu wako Kama mwanaume wako umhakikishie usalama wake kiuchumi,kimwili na kijamii popote pale anapokua na wewe.
3. Kuvipa vipaumbele vitu vya muhimu Ila sio visivyo na msingi Kwny mahusiano,
Mf: kupenda kutamkiwa unapendwa kila mara, kupigiwa Simu kila Mara, n.k
Mwenzio anafanya kazi,
Yanini umpigie pigie Simu na sms ovyo umtake akwambie anakupenda,
Kwani asipokwambia anakupenda wee huwez gundua unapendwa?
4. Kua na matarajio hasi unapoingia Kwny mahusiao na mtu aliekuzidi umri
-Ondoa kabisa mawazo ya kwamba kakaribia miaka 30 kwaiyo kaja kwako kutafuta ndoa na mtoto,
kwani kuoa Unaeweza kuoa ni wewe peke ako TU?
Hizo hizo shahawa za mimba unazo peke ako TU?
Kwanini hajaenda kwa wengine, Yuko na wewe?
Hebu jitahidi kua positive minded unapoanzisha mahusiano yoyote yale ubongo wako uwe free.
5. Kuwasema vibaya wanawake zako punde TU mnapoachana,Hii sio tabia nzur hata kidg.
Kumbuka ulishatwambia mlishaachana mkarudiana, Sasa vipi Tena mkija rudiana?
Maana ake utakua umerudia kula matapishi yako mwenyewe au?
Huoni kwa matatizo yote uliyomsemea vibaya, ukija kurudiana nae utakua umejivua nguo zako wewe mwenyewe?
Hebu epuka uadui usiokua na kichwa Wala miguu na wanawake zako, huwezi kuijua kesho yako au ya mwenzi wako.
Hii duniani Ni tambala bovu mkuu, Zingatia ayo kwanza.[emoji848]