Nimekutana na Basi "Made in Tanzania", hongera Rais Samia Suluhu

Hayo magari mengine yote huko nje yanatengenezwa na marais wa nchi hizo? Utoto mwingine bana.
Kidogo ninashangaa!

Mkuu 'Figganigga' siyo mtu mgeni hapa JF. Sikuwahi kumsoma kwa nyimbo kama hizi hapa jukwaani!

Hivi inawezekana mtu kujitoa akili kirahisi namna hii?

Kwa bahati mbaya hii ndiyo hulka inayowatambulisha waTanzania wengi.
 
Kidogo ninashangaa!

Mkuu 'Figganigga' siyo mtu mgeni hapa JF. Sikuwahi kumsoma kwa nyimbo kama hizi hapa jukwaani!

Hivi inawezekana mtu kujitoa akili kirahisi namna hii?

Kwa bahati mbaya hii ndiyo hulka inayowatambulisha waTanzania wengi.
Labda kadokezwa kuna teuzi za wakuu wa wilaya.
 
Magari yote ya magereza yale ya kijani yanayobeba wafungwa yametengenezwa na Manji , diwani wa Mbagala kuu
 
Viwanda vyote vya magari duniani huwa ni assemblers tu. Wanasource vifaa mbalimbali vya magari kutoka kwa watengenezaji mbalimbali. Injini kutoka kwa huyu na suspension system kutoka kwa mwingine.
Akiba ya maneno muhimu sana.
 
Msiturudishe kule jamaaa..!! Kule ambako mchezaji anafunga gola uwanjani anasifiwa raisi. Furthermore, ni made in Tz au assembled in Tz?
Mkuu hii nchi bado kuna shida sana kwa baadhi ya watu. Sometimes unajiuliza hivi huyu mtu ni mzima kichwani? Reasoning abilities zao ni questionable kwa kweli. Na siajabu hao ndio wanapewa nafasi ya kuwa policy makers
 
Limekua Assembled au made in Tanzania? Ni swali tu
 
Kiwanda gani kimetengeneza hili basi?
 
So unaamini hiyo kazi imefanyika ndan ya siku 90? Yaan kuanzia wazo Mpka hiyo product?
Pole sana
 
Nadhani ww ndio unajua leo. lakin hivi vitu vimefanyika before jpm hajawa rais.

Na hizo mambo za kusifia mtu mwingine wkt wapo vijana waliopambana kuunda hili bodi uache.

sifa ziende kwa waliohusika
jinga wewe, sifa zinaenda kwa kwa anaeweka mazingira mazuri kuwezesha ubunifu
 
Hilo basi (sio moja) limeundwa na mzee mmoja yupo Kibaha kitambo sana, nadhani alianza harakati zake kipindi mwendazake akiwa Rais...

Katika hali ya kawaida hata kama ingekuwa ni kweli Samia kahusika (najua si kweli), ndani ya miezi 3 hakuna mtu anayaweza kubuni, kuunda gari kubwa hivyo lenye mifumo kedekede...

Wakati mwingine let's use our common sense...
 
Common sense na members [wengi] wa JF??!!

You kidding me!
 
Hilo bus la Premier limeundwa na Jn star (BM Motors) pamoja na hilo alilo post mtoa mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…