Nimekutana na rafiki yangu mwarabu tuliesoma shule ya Msingi, Nasikitika kuona wageni wanavyotajirika huku wenyeji tumeridhika na vimafanikio vidogo

Ukwel ambao wa Tz wanachelewa kuujua
 
Watu hawajui historia mkuu.Warabu tumesoma kuwa walianza kija karne ya 7 na kuanza kuanzisha miji.
Warabu ni watu wa wazamani sana hapa Afrika na wameoana na watu weusi kwa miaka mingi sana.
Sudani kaskazini ni warabu weusi tii. Walikuja lini? Wabantu tunejipa umiliki wa bara la Afrika kitu ambacho sio kweli.
Tushukuru mungu tu kuwa hao warabu hawakutumaliza kwa hila ila kama walivyomalizwa wahindi huko USA. wamesambaa sana bara la Afrika na kuwa sehemu ya Afrika.
Misri ilikuwa nchi ya watu weusi wakaja warabu wakamuondia mtu mweusi wakaka wao mpaka leo hakuna mtu mweusi anaweza sema ni nchi yake.
Kimsingi tuishi nao tu kama wenzetu maana hata uwezo wa kuwafukuza hatuna japo wameshikilia utajir wa TZ.
 
Mkuu,asante kwa Darasa.
 
chukua tu mfano wa shabiby, mababu na mababu wamekuja na kazaliwa na kukulia kijiji na gairo pale, amefanikiwa watu wanamwona mwarabu wakati kachanganya na wagogo sijui watu gani huko na wazazi wao wamekuja miaka mingi kuliko hata wabantu wengine. wabantu hii nchi tumehamia tu toka nchi zingine na wengi wamekuja baada ya waarabu na wahindi kuwa wameshakuja tayari.sisi sote ni wahamiaji.
 
Kama nimekuelewa vizuri, unataka kuaminisha watu kuwa wabantu waliwakuta waarabu kwenye hii nchi, na si kwamba wakati waarabu wanakuja waliwakuta wabantu.?
 
Ukipata shs.100,000/= unatafuta demu na bia, mwarabu akipata shs. 100,000/= anaipeleka nyumbani kwa mama yake wanapanga nini cha kuifanyia.
 
Yeah iko hivo ..ni Kama bodaboda ya mkataba...yani anapewa duka Kama mfanyakazi..ndani ya miaka mitano anaachiwa duka hilo linakua lake
 
Duh tunaogopa wataiba pipi [emoji3][emoji3]
Mimi bwana wahindi na waarabu nishasema sitaki kushindana nao wana maisha .

Wewe mjinga SANUNI ikiwa unanisoma hapa , endelea kunizidi hela hatuwez kuwa matajiri wote bwana .
 
Suala la kufanya biashara kwa wakuja sio jambo geni duniani
Kila nchi utakuta wenye asili ya hapo wanaburuzwa kwenye uchumi unajua kwa nini?

Kwa sababu wahamiaji wanapokuja kwenye nchi yoyote hawawezi kujihusisha na kazi za serikali kwa sababu sio wazawa na wanahitaji hela za haraka, hapo ni lazima wafanye biashara tu hakuna kingine

Awe Irishman huko ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ธ au Msomali Nairobi wao ni biashara tu maana hata mda wa kuimba wimbo wa Taifa hana
Siasa hawawezi kuingia labda wawe ni generation ya Tatu tena mmoja katika milioni
Hapo ni kuwaiga na kupata mbinu zao na sio kuwa na jicho la husda
 
Kama nimekuelewa vizuri, unataka kuaminisha watu kuwa wabantu waliwakuta waarabu kwenye hii nchi, na si kwamba wakati waarabu wanakuja waliwakuta wabantu.?
mfano, chukua Mkoa wote wa Songea, wale wa kabila la wangoni, wamekuja toka south africa kati ya 1820 and 1840 wakati waarabu na wahindi wengine wamekuja hapa tangu karne ya 7. nani mwenyeji wa mwenzake hapo? watu wa kigoma, kagera, arusha, mtwara, tanga wote hao wamehamia toka nchi walizopakana.
 
Narudia kusema

Maendeleo yakikaa kibepari lazima yakae kiubaguzi aidha kirangi, kidini au kikabila au kikanda. Hivi vyote kwa Tanzania vipoo.

Waislam wengi maskin Sanaa. Wachaga na wazaramo, wazaramo ni maskini mnooo. Waafrika na wahindi, waafrika maskin sana. Hata ukanda wa kusini hauna maendeleo ya kufananisha na mikoa ya kaskaxini
 
Wangoni waliopo hapa hawana ndugu wala hawajui asili yao tena huko SA ILA wahindi wa hapa unaowahita watanzania haswa kuliko wabantu, wanarudi INDIA kila mara!

Ni nadra kusikia majumba yale ni ya wahindi ila waarabu; wanajenga INDIA na huwasikii wakilalama kuhusu URAIA PACHA.

Unajiuliza kwanini wanafanikiwa, masikini wa kihindi au kiarabu, ni sawa tu na masikini mmakonde, hatoboi hata iwaje?

Hebu tafuta watu wa ukoo wa akina Mareale, kisha linganisha umasikini na utajiri kwao, unadhani ni kwasababu ya rangi? Ni ukoo uliotajirika kitambo sana, kutoboa kwao ni lazima. Same applies to hao Arabs na Asians, walichukuliwa kama binadamu grade 2, 3, wakapewa fursa hivyo enzi hizo za ukoloni, wakafuata akina Mareale(chiefs) etc.

Unadhani wakina Kikwete, Nyerere, Sykes, Salim walitokea tu from nowhere kama Magu?
 
Kuna askari alimkamata jamaa yangu wakati anamchukua maelezo akamuuliza we kabila gani.Jamaa akajibu mi mwarabu.Askari eti kakasirika eti usiniletee utani ntakupiga hebu nitajie kabila [emoji23][emoji23][emoji23] yule jamaa akamwambia angalia katika makabila Tanzania Hilo kabila halimo ama limo Tanzania.Ndo nikajua askari wetu ni vilaza.Watu hawajui Tanzania Kuna kabila la Waswahili ila wasiojua watabisha.
 
Ulipoongea hili swala umenikumbusha kuna wasomali nakaa nao wanaduka....yaani mtoto katoka shule anauza duka fresh tu yaani ......ila wee njoo huku kwingine ata kucheza tu ni tatizo
 
Kutoa sio lazima iwe hela.....inaweza kuwa kwa hali na namna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ