Nimekuwa nikiumizwa na historia yangu ya nyuma natamani kumwambia ukweli mpenzi wangu lakini nahofia ataniacha

Usiishi kwa kujihisi. Ktk ukristo ukishaoka na kuoshwa na damu ya Yesu Kristo unakuwa mpya. Kwa sababu hiyo historia yako ya mambo ya zamani ilishapita na hao watu haupo nao tena, hakuna haja ya kusimulia wewe endelea na maisha mapya!
 
Habari za wakati huu wana JF ni matumaini yangu mu wazima wa Afya.
Bila kupoteza muda twende kwenye jambo husika tajwa hapo juu.

Mimi ni msichana, kipindi nasoma kuna maisha nilikuwa naishi hapo nyuma hayakuwa mazuri nadhani ni kwasababu ya utoto na kutojitambua pia, ama ni ile foolish age pia ilichangia.
Kwasasa nimekua nina kibarua nafanya nimeshakuwa kwenye mahusiano kadhaa kadhaa lakini tulishindwana, pia watu niliokuwa nao kwenye mahusiano hawakuwa tayari nadhani au walikuwa na watu wao.

Mwaka jana nilibahatika kuanzisha mahusiano na mwanaume mmoja mpaka sasa hivi nipo nae lakini hatuko kwenye mkoa mmoja, sasa jambo ninalohofia ni kwamba ikitokea siku akafatilia background yangu akaambiwa maisha niliyoishi hapo nyuma itakuwaje na mimi sijawahi kumwambia, nahofia akija kujua anaweza kuniacha.

Ninaomba ushauri wenu wadau je ni sahihi mimi kumweleza mpenzi wangu ukweli wa maisha niliyopitia hapo nyuma au ninyamaze tu haina umuhimu??
Mpenzi au mume?
 
Kuna binti tulikuwa kwenyw serious relationship katikati ya mapenzi mazito siku moja nikamtania kuwa unaonekana enzi zako watu uliotoka nao Hiece inajaa sio kwa uzuri huo akarukia kwa juu akasema Hiece tu Costa kabisa inajaa
Baada ya hapo nilianza mikakati ya kumuacha,ikawa ndio bye bye.
 
Ni muhimu sana mwanamke kujitunza na kama unaona ulifanya blinders huko nyuma ni mara 💯 umueleze mwenzio hata kimafumbo ili awe aware na sio kuja kusikia kwa marafiki au nduguzo.
Utahatarisha mahusiano yako
Ni ngumu hii wengi wamenishauri nikae kimya, naona bora nikae kimya tu naweza kuongea nikawa kwenye hatari zaidi
 
Kuna binti tulikuwa kwenyw serious relationship katikati ya mapenzi mazito siku moja nikamtania kuwa unaonekana enzi zako watu uliotoka nao Hiece inajaa sio kwa uzuri huo akarukia kwa juu akasema Hiece tu Costa kabisa inajaa
Baada ya hapo nilianza mikakati ya kumuacha,ikawa ndio bye bye.
Pengine na yeye alikuwa anakutania tu
 
Habari za wakati huu wana JF ni matumaini yangu mu wazima wa Afya.
Bila kupoteza muda twende kwenye jambo husika tajwa hapo juu.

Mimi ni msichana, kipindi nasoma kuna maisha nilikuwa naishi hapo nyuma hayakuwa mazuri nadhani ni kwasababu ya utoto na kutojitambua pia, ama ni ile foolish age pia ilichangia.
Kwasasa nimekua nina kibarua nafanya nimeshakuwa kwenye mahusiano kadhaa kadhaa lakini tulishindwana, pia watu niliokuwa nao kwenye mahusiano hawakuwa tayari nadhani au walikuwa na watu wao.

Mwaka jana nilibahatika kuanzisha mahusiano na mwanaume mmoja mpaka sasa hivi nipo nae lakini hatuko kwenye mkoa mmoja, sasa jambo ninalohofia ni kwamba ikitokea siku akafatilia background yangu akaambiwa maisha niliyoishi hapo nyuma itakuwaje na mimi sijawahi kumwambia, nahofia akija kujua anaweza kuniacha.

Ninaomba ushauri wenu wadau je ni sahihi mimi kumweleza mpenzi wangu ukweli wa maisha niliyopitia hapo nyuma au ninyamaze tu haina umuhimu??
Taja hiyo background kwanza tuone tunakushaurije, maana kuna background zingine ngumu kumesa
 
Kwenye ofisi za umma huwa tunaanzia kazi pale tunapokabidhiwa ofisi na kuendelea na utapimwa kuanzia kwa kuanzia hapo ulipoanza.
Kwa kadiri changamoto zilizoachwa na mtangulizi wako zinavyojitokeza ndivyo tunavyo solve.
Huwa hatufukui makaburi kwenye ofisi za umma.
Kuwa na amani.
New Boss akitaka kujua, atajulia hukohuko, ukijifanya mtakatifu maria utahama ofis kila siku.

Nadhani umenielewa.
 
Back
Top Bottom