Nimekuwa nikiumizwa na historia yangu ya nyuma natamani kumwambia ukweli mpenzi wangu lakini nahofia ataniacha

Nimekuwa nikiumizwa na historia yangu ya nyuma natamani kumwambia ukweli mpenzi wangu lakini nahofia ataniacha

Naweza sema mimi ni moja ya aina wanaume unawaeleza, napenda sana fuatilia background ya mwenza.

Huwa nafuatilia kwa malengo tofauti, lakini kwenye swala la historia ya mahusiano napenda kujua athari ambayo mwenza aliipata kwenye mahusiano aliopitia.

Inaweza isiwe muhimu kueleza kwamsisitizo mahusiano uliopitia kwa mwenza ili umfanye ajihisi kuwa yeye ni wapekee ila ueleze kitaalamu athari ulizopitia ambazo unahisi zitaaribu mahusiano yenu.

Mfano km mahusiano yako ya nyuma yalikufanya usiwe na imani juu ya wanaume au usijiamini, unaweza ukatumia njia ykueleza background yako kwa kukandia machafu uliofanyiwa nyuma. Kitu ambacho usifanyi kosa ni kueleza kitu kinafanya kumsifia x wako.

Nyie wanawake tukitumia njia ya kuingiza urafiki kwenye mahusiano huwa mnajisahau sana, nilifanya hvyo kwa binti ambae alionesha kunipenda, baada yakumfanya awe rafiki akaanza kusema "Yani mimi sidhani km takuja kupenda km nilivyompenda G naomba naww usiwe km G" huyo G ni xwake automatically lilinifanya nikapunguza mpaka kuondoa mapenzi kwake. Sikushauri ufanye hilo kosa

Lakini vile vile usitolei macho background ya mahusiano tu angalia na malezi pamoja na mazingira uliokulia, km kunavitu unahisi ulipitia kwenye malezi na huenda vikaleta athari kwenye mahusiano ni bora umwambie.

Mfano: pengine historia yako labda pindi unasoma wazee wako walipenda kukuhusisha na mila za ajabu ambzo ukifanya kwa mtu wako anaweza hisi wewe ni mshirikina na yeye sio wa mambo hayo bora useme tu mapema vitu vinafanana na hvyo.

Generally: nivyema kuweka wazi vitu ambavyo unahisi vitakuja kuleta athari km hatovijua kipindi cha hichi cha ulevi(honeymoon)
Asante mkuu hili swala nitalifanyia kazi mapema sana
 
Habari za wakati huu wana JF ni matumaini yangu mu wazima wa Afya.
Bila kupoteza muda twende kwenye jambo husika tajwa hapo juu.

Mimi ni msichana, kipindi nasoma kuna maisha nilikuwa naishi hapo nyuma hayakuwa mazuri nadhani ni kwasababu ya utoto na kutojitambua pia, ama ni ile foolish age pia ilichangia.
Kwasasa nimekua nina kibarua nafanya nimeshakuwa kwenye mahusiano kadhaa kadhaa lakini tulishindwana, pia watu niliokuwa nao kwenye mahusiano hawakuwa tayari nadhani au walikuwa na watu wao.

Mwaka jana nilibahatika kuanzisha mahusiano na mwanaume mmoja mpaka sasa hivi nipo nae lakini hatuko kwenye mkoa mmoja, sasa jambo ninalohofia ni kwamba ikitokea siku akafatilia background yangu akaambiwa maisha niliyoishi hapo nyuma itakuwaje na mimi sijawahi kumwambia, nahofia akija kujua anaweza kuniacha.

Ninaomba ushauri wenu wadau je ni sahihi mimi kumweleza mpenzi wangu ukweli wa maisha niliyopitia hapo nyuma au ninyamaze tu haina umuhimu??
Hujasema aina ya hayo maisha tupime uzito je;
1. Ulikuwa mvuta bangi?
2. Ulikuwa msagaji?
Au jambo gani?
 
Back
Top Bottom