Nimekuwa nikiumizwa na historia yangu ya nyuma natamani kumwambia ukweli mpenzi wangu lakini nahofia ataniacha

Asante sana nitajaribu kufanya hivyo japo najua ni kama nimechelewa kuna siku aliwahi kuniuliza niliwahi kuwa na wangapi kabla yake nilimdanganya nadhani pale ndiyo ilikuwa nafasi ya kusema ukweli
 

Usithubutu kamwe,na akiambiwa kuhusu hiyo historia kataa, sema wanakuonea wivu tu.

Ila uache umalaya sasa utulie we mwanamke.
 
Kwasasa ninaishi maisha ya kawaida sifanyi yale mambo tena na wala sina marafiki, niliwaza tu mbeleni kama labda akafatilia akajua, kwa hili jibu lako nikimwambia kuwa niliteleza nilipokuwa mdogo atataka maelezo zaidi🥲
Huenda unaona huyo mwanaume ndiyo turufu ya maisha yako kiasi cha kuogopa kumpoteza? Ushauri wangu ni kuwa usimwone kama jambo la kufa na kupona, utakuja kuumia sana mambo yakigeuka. Mimi nilisema upige story bila kuonyesha kuwa ulipitia maisha hayo. Akija kugundua na kukuacha wala usisikitike sana kwani kila jambo lina wakati wake.
 
😁😁umewaza mbali sana mkuu, hili jina sijui hata lilitoka wapi kipindi najiunga ndiyo lilikuja kwa haraka haraka, nitaomba mods wanibadilishie waniwekee hata binti sayuni
Sawa Binti Sayuni, ...hata Paul àlikuwa mkora Leo twasoma Injili yake....! Namna unavyojibu hizi hoja ,naona umetupa chai yq Iftar!
 
Asante sana, hakika umenifungua macho
 
Asante sana nitajaribu kufanya hivyo japo najua ni kama nimechelewa kuna siku aliwahi kuniuliza niliwahi kuwa na wangapi kabla yake nilimdanganya nadhani pale ndiyo ilikuwa nafasi ya kusema ukweli
Nachelea kusema huyo hana busara (waliosema usimchunguze bata hawakuwa vichaa)..., na unaweza kudhani umepata kumbe umepatikana.., mtu ambaye ana wivu hata kabla / wakati bado hamjatambuana anaweza kuwa a one step before kuchomana visu na kuzikana kwenye septic tank....

Kumbuka boyfriend, girlfriend ni bora na raha kuliko marriage...

 
Hata mimi nilishangaa why aliniuliza hivi, ngoja tuendelee kuchunguzana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…