Nimemjengea mama yangu nyumba nikiwa bado nipo kwenye 20's

Nimemjengea mama yangu nyumba nikiwa bado nipo kwenye 20's

Wasalaam,

Habarini Wana jf,kwanza kabisa niseme nawashukuru wanajamii-forum wote kwa ujumla hasa hili jukwaa letu pendwa la biashara,uchumi na ujasiriamali, kwani tumekua tukipeana mbinu za kibiashara ambazo zinaweza kutusaidia kujikwamua kiuchumi kwa namna moja au nyingine...mbarikiwe sanaaa[emoji119]

Ni miaka mitatu Sasa tangu nimalize kidato cha sita na kuingia mtaani kuanza kupambana rasmi na maisha(binafsi sikufanikiwa kuingia chuo). Katika kipindi hiki Cha miaka mitatu(3) nimejifunza mamb mengi Kama kijana,itoshe kusema katika kipindi hicho chote nimejifunza kupambana till my last drop to achieve my wildest dream,pili kuwa mkweli kwa nafsi yangu

Katika vitu vinavyonipa faraja ni kumjengea mama yangu nyumba nikiwa bado nipo kwenye 20's[emoji847],hii kitu imenipa faraja sana sana,ingawa bado sijafika Ila nimeanza kuuona mwangaza kwa mbaaaali

LENGO /DHUMUNI LA HII THREAD;
Lengo la huu Uzi ni kukujulisha kijana mwenzangu kuwa sasa ivi tunaishi katika "information age"(golden era) hatuhitaji tena pesa kutengeneza pesa bali taarifa sahihi na uthubutu kutengeneza ukwasi wa kutisha,hivyo basi jitahidi Sana Sana Sana kuwa na taarifa sahihi......itakusaidia
#never lose focus#.....today is tuesday choose it wisely

View attachment 1826441

View attachment 1826439
Ungepiga picha moja tu ya jengo lote, sio vipande.
 
Umeona hawajakusifu huko coz wanakujua kwa misifa yako umetuletea sie ili usuze roho yako, maana kama ulileta wenzio wajifunze ungewaelekeza mbinu ulizotokea kimaisha ili nao wapigane. Eti sijibu PM
 
HONGERA SANA, unafanya shughuli gani mkuu?
Swali zuri sana hili...
Akilujibu nitag...
Kama habebi maboksi ng'ambo basi ana madili fulani au hela za urithi...
Mengine tusidanganyane, hata hivyo ni hatua nzuri kukamilisha baadhi ya vitu haraka iwezekanavyo cha msingi ufanyacho kama si legitimate basi usikamatwe...
 
Mungu atakubariki zaidi kamanda, zidisha mapambano.
Asante sana mkuu[emoji1666],hatupunguzi matarajio yetu yawe sawa na utendaji wa kazi,bali tunaongeza utendaji wa kazi kuyafikia matarajio tuliyojiwekea. Sababu maendeleo ni mawazo yaliyotekelezwa...
 
Asante sana mkuu[emoji1666],hatupunguzi matarajio yetu yawe sawa na utendaji wa kazi,bali tunaongeza utendaji wa kazi kuyafikia matarajio tuliyojiwekea. Sababu maendeleo ni mawazo yaliyotekelezwa...
Mbona unachagua comment za kujibu?

Unaulizwa unajishughulisha na issue gani mbona hujibu?

Kwanini unajibu comment positive na zenye maswali hujibu?

Hi njia ya kutojibu pm unazan ONTARIO hajawahi tumia?

Kwanini usije na njia tofauti ya kutapeli kuliko hii iliozoweleka hapa jukwaani ya forex?

Kijana unafikiri hapa jukwaani ana miaka 20 kama wewe?
 
Hongera sana kijana, kwa sasa usibebe mtu kwenye moyo wako chapa kazi
 
Tunaishi kwenye information age lakini wewe unatunyima hizo information, tutatoka kweli?
Na lazima ujue kuwa ili information ziwe na nguvu...lazima ziwe kwenye cycle ya watu wachache....mtoa mada endelea kuonyesha picha tu. ...if its matter of information don't ever disclose it
 
Back
Top Bottom