Mkuu, yaani afanye kumfurahisha mwanamke ambaye ameonesha wazi kabisa hapendi ndugu wa mmewe!!?Basi jitahidi ndani ya miezi 3 uwe umemtafutia Chumba cha kupanga, Kuna Vyumba vinapangishwa Kwa shilingi 40,000 hadi 50,000
Ukiweza Fanya hivyo ili kumpa furaha Mke wako
Ndoa yako ikiwa na amani, hupelekea kukupa Utulivu Mwanaume
Lakini ikishaanza migogoro midogo midogo kama hiyo, inaweza kuwa ni tiketi ya kuanza kurudi nyumbani saa nane za Usiku
Nani atawaza kusogea hapo kwake miongoni mwa ndugu zake!!?
Mwanamke siyo ndugu yako aisee, akiamua kukuacha anakuacha na ulishakosana na ndugu zako kwa sababu yake..
Heshima kwako mkuu mleta uzi, umeshaoneshwa una mke wa aina gani. Ongeza umakini vinginevyo wewe au mpwa au wote kwa pamoja mnaweza kukinywea kikombe cha hasira yake.