Nimempiga boadaboda mpaka nimemuonea huruma

Ooh sawa
 
Pole sana, kwahio leo unalala kwa sista?
 
kweli kabisa.wengine utoto tu unawasumbua maana wengi ni vijana wadogo sana.Leseni zenyewe sijui wanapataje maana madereva wa magari watapata sana tabu nao.Yani wao wanaona kama wenye magari wanapaswa wavute tension wakiwaona hivyo anajiingiza kichwa kichwa akijua wewe unamwona.Sasa ukiwaparua kidogo basi hapo ugomvi matusi yani ushamba tu
Kitu nakubaliana na mleta mada wengi wa hawa bodaboda wametoka bush
 
Pole sana mkuu lakini hongera pia
 
Mkuu mleta mada mi hawa watu wananiudhi sana hapa mjini, unakuta mtu upo kwenye njia ya waenda kwa miguu lakini wao wanakuja kwa speed na mihoni kibao, hata hawajali kwamba hii njia ni ya watembea kwa miguu ni fujo tupu, na ukikaa vibaya wanakugonga, hata kama ni bangi sijui wanakula za wapi zinazowapa akili za namna hiyo.
 
Hahaaa. Kuna pub nilikuwa nimekaa. Sasa wakati nataka nitoke niingie barabara kubwa wakapita boda wawili wanafukuzana kwa speed kubwa. Mmoja akayumba akaja akaivaa gari kwa mbele na kuanguki mtaroni.
Nilipoona gari haijaumia nikataka nisepe. Sindio anakuja na kudai nimlipe eti nimemgonga. Nikaanza kumshushia kichapo. Mara yule mwenzake akaje. Nilikuwa karibu na jiko la kuchomea nyama. Nilichofanya ni kuweka nyama pembeni nikainua jiko lenye Moto na kumwagia yule aliyeingilia ugomvi. Asee alitoka nduki Hadi akasahau boda yake. Uzuri kwenye ile bar nafahamika so yakaisha.
 
Sasa mzee ni sababu una ngumi za kichawi
 
Mie kuna mmoja baada ya kunikosakosa, alisimamisha pkpk yake akianza kutoa matusi huku akisema alitaka kunvunja miguu.
Nilichomfanya nilimpa kichwa kimoja KITAKATIFU akaenda chini nikamuwahi huko huko nikashika kichwa chake nikaanza kukisugua kwenye lami
 
hahaa huyu ulimpa adabu mkuu hatarudia.
 
Wanaendesha wakiwawamesinzia.

Kuna mmoja mwaka jana nimesimama kwenye mataa.. nikasikia mshindo nyuma.. ile kugeuka jamaa yupo chini na bamba langu la nyuma limeharibika kumbe jamaa kagonga kwa nyuma.

Sasa ile nataka kumdhibiti akawasha boda yake aka kimbia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…