Nimempiga mwizi mapanga mawili ya kichwa, akifa Mungu nisamehe

Nimempiga mwizi mapanga mawili ya kichwa, akifa Mungu nisamehe

Hahaahaa Mzee baba Kitoabu Kama nakuona vile,hapo ulicheza Kama pere dadeq bora umeliwahi maana majitu ya Moçambique nasikia yana roho ya chuma lingekutoa roho na hiyo nondo yake Bora umetumia mbinu za Afande Chacha mura piga risasi rikikwepa rusha panga!

Wasaalam hapo Cabo de galdo mkuu!

Dadeq!
 
Kwa ushahidi gani atakaoutumia ili huyo mwizi athibitishe ni Kitoabu ndiye amemuua huyo jamaa? Na motive iwe ni mwanamke? Haya sawa, mtaje huyo mwanamke ambaye bwana mwizi na kitoabu wanamjua.

Mwili wa binadamu ni complicated sana. Waweza kuta jamaa akapona
Serikali ikifanya uchunguzi itagundulika tu ww ndie umemuua (Kama akifa)na sababu ulimtoa nje kwenda kumtupa hapo ndipo ulipofanya kosa kubwa litakalokupeleka kingi
 
Wanasema akuanzae mmalize, au mchelea mwana kulia hulia mwenye.

Umepambana maana kuwa na silaha ni jambo moja na kuweza itumia kwa ufanisi ni jambo lingine.
 
Serikali ikifanya uchunguzi itagundulika tu ww ndie umemuua (Kama akifa)na sababu ulimtoa nje kwenda kumtupa hapo ndipo ulipofanya kosa kubwa litakalokupeleka kingi
Kwakua ukimtupa linakuaje kosa kubwa?
 
Mungu anajua sijawahi liua jitu hata siku moja lakini ikitokea lile jamaa likafa shauri yake na familia yake, pumbavuu.

Mwaka jana nimeibiwa mara mbili nikahama mtaa...
Mwizi ninkuacha afe tu, wamewahi safisha geto langu enzi hizo na kuniachia ndala na mapazia tu, siwapendi wezi na wafage tu...nilianza upya kila kitu.
 
Umeniudhi mmemchelesha

Siku nyingine akiwa hajakata pumzi mnamuwaisha koroga cement nusu Lita au litamoja mnywesheni kwanguvu iwezitozito uji wakati

Akawahadithie wezake ahela huko

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Ahsateni ndugu zangu kwa ushauri wenu, nipo hapa najiandaa niingie mtaani nikasikilizie habari vizuri.
Najua nikienda maskani za wahuni lazima nitajua tu kilicho endelea jana.
Chochote kitakacho jili nitawajulisha.
 
Kuna wezi walikuwa wananisumbua kila siku usiku....kuruka ukuta. Nikaweka vyupa juu wakawa wanaweka matambara wanaruka tu.

Nikaona ishiwe taaabu niingie gharama kidogo nikanunua misumari ya nchi 4 kilo 5 nikanunua na mbao 5 za 1 by 8.

nikagonga zote zikatokea upande wa pili...nikazipanga pale ambapo huwa wanarukia ukuta kisha nikafunika na gunia jepesi...nikalala zangu..

Jamaa wakaja kama kawaida yao - huwa wanavaa matambala kwenye nyao zao ili wanyate bila vishindo... siku hiyo nikawa macho nishuhudie...

Wawili wakapanda ukuta...kwa kwanza akajipupaaa...kimyaaaa....wa pili naye akajitupaa kimyaaa...

Wale wenzao kwa nje wanaita oyaa vipi...

Jamaa wamenasa kwenye misumari... nilitoka taratibu huku wakiniita braza braza tuhurumie braza....

Sikuhangaika nao, mdogo mdogo nikaenda kwa mwenyekiti serikali ya mtaa, kisha tukaenda police... walikaa kwenye misumari kama masaa 2 hivi - saa 11 na nusu pameshaaza kupambazuka majirani woote wamekuja kushuhudia wanavyongolewa..

Aisee ilikuwa mbaya sana, ila fundisho walilipata.
 
Kwa hiyo umetenda dhambi ya kuua?
Alikuwa anajilinda. Asingejilinda ile nondo ingemwua yeye.
Binafsi namkubali mshikaji kwa kitendo alichokifanya.

Hata mimi chumbani nina panga, nondo na fimbo. Hivyo ninapohama huwa vya kwanza kuingizwa kwenye gari na nimifika ndo vya kwanza kuingizwa room.
 
Back
Top Bottom