Nimempinga Godbless Lema ila sasa Natubu

Nimempinga Godbless Lema ila sasa Natubu

Le

Lema hajasema yeye ni tajiri,,,kasema kutaja dola 5000 anazolipwa mbunge wa tz kwamba ni hela nyingi inategemea uko katika jamii maskini kiasi gani kwa sababu usd 5000 ni malipo kwa wasiokuwa nakazi ulaya na marekani,,,,yeye ameenda uhamishoni kafanya kazi kapata kamtaji anataka awekeze angalau Dubai,,,tuwe wakweli Lema anaamsha bongo zetu zimelala Sana.
Alipotua tu nchi toka canada alisema kuwa siasa kwake si kazi mkuu
 
Le

Lema hajasema yeye ni tajiri,,,kasema kutaja dola 5000 anazolipwa mbunge wa tz kwamba ni hela nyingi inategemea uko katika jamii maskini kiasi gani kwa sababu usd 5000 ni malipo kwa wasiokuwa nakazi ulaya na marekani,,,,yeye ameenda uhamishoni kafanya kazi kapata kamtaji anataka awekeze angalau Dubai,,,tuwe wakweli Lema anaamsha bongo zetu zimelala Sana.
Akawekeze Dubai ? Sasa anakimbizana na siasa kwa ajili gani ? Ni swala la muda tu mtaono mikutano wataanza kukusanya
 
Unajua maana ya kipato halali? Huyu ambae anaoinga boda boda atauonyeshe anafanya biashara gani nje ya siasa? Hivyo wale wavivu wa baharini kazi yao sio hatarishi?je wanaofanya migodini kazi zao sio hatarishi?je madaktari wa binadamu kazi zao si hatarishi?
Wavuvi wanahitaji kuboreshewa nyenzo za kuvulia pia,,,migodini wanahitaji vifaa vya uokozi na kujikinga pia na maslahi yao kulindwa,,hajasema ni kazi Bora usimlishe maneno lkn angalau zina tija kubwa katika uchumi.
 
Nadhani hujaelewa ulinganifu wa kazi nilizotaja kubusu risk zake ikiwa ni pamoja na boda boda ,huyu kilaza wenu huenda alikuwa na hoja ila uwasilishaji wake ndio umeua dhana yote ya nia njema kama alikuwa nayo
 
Wachache sana wa kuona hili ila ukweli Lema kakamata penyewe bahati mbaya jamii ya kiafrika haitaki kusikia ukweli inataka uongo wa kujiliwaza tu lakini Lemma yuko maili mia mbele.
Lema anaongea ukweli mchungu watanzania wachache humu ndani tunaelewa
 
Kupitia hoja za Lema nimegundua watanzania wana uwezo mdogo wa kufikiri ndio mana hata hayati Magufuli tulishindwa kumuelewa
 
Lema akiwa Star Tv na Alloyce Nyanda nimemwelewa sana.
Aisee binafsi nimekuwa nampinga Lema toka afike nchini na kuibua hoja mbali mbali. Lakini sasa naomba niseme samahani Lema nimekukosea Sana.

Nimekaa kwenye tafakari siku 3 nikagundua kwamba jamii ya wtz iko gizani hivyo hiawezi kung'amua hoja nzigo za Lema,,,na bahati mbaya hata wenye kuelewa hawasemi maana pengine wananufaika na umaskini huu wa mtz.

Haiwezekani nifanye kazi ambayo hainihakikishii maisha bora uzeeni (bodaboda) alafu niite ni ajira njema,,,kwa wakulima hii tunaiita subsistance farming yaani unalimia tumbo tu.

Kuhusu kujali haki za watu Lema kaongea uhakika kabisa,,ukitaka kujua hili nenda kutafuta huduma katika ofisi za umma ndio utaelewa nchi hii ina Safari ndefu Sana .

Kuhusu afya nenda hospitali kajionee vituko katika korido za hospitali ambao mgonjwa anachukuliwa Kama mtu asiefaa,anatukanwa na manesi utadhani nguruwe pori.

Mama wajawazito maskini utadhani labda kubeba mimba ni dhambi kwao,,wanatuknwa mpaka sio poa,,,wanajifungua kwa kupigwa makofi na kusimangwa hadi huruma,,sasa Lema akisema mbwa Canada ana thamani kuliko binadamu tz ana kosa gani!?

Nimejiona mjinga nilipojaribu kusema eti huwezi fananisha Tz na Canada,,nkajijibu kwani Canada wamewezaje kufika hapo na sisi tumeshindwaje kufika hatua nzuri,,,inakuwaje tuwe na rasilimali alafu tushindwe kuzibadilisha kuwa utajiri!? Je,tumeshindwa kuwekeza katika akili za watu wetu!? Na nini kimetufanya tushindwe kuitumia rasilimali watu kuwa nyenzo muhimu kujiletea maendeleo!?

Ndg Lema amefichua misukule ya watu iliyofichwa miaka mingi hivyo lazima wenye misukule wawe wakali.

Tungekuwa na akili Kama taifa na vyombo vya hbr huru vinavyojua kuona mbali,,tungezitumia ajenda za Lema haraka Sana iwe ndo mjadala ili tujue tunatokaje kwenye mkwamo huu.

Tunahitaji akina Lema Kama 20 tu then Taifa litaacha kuzungumzia Mambo mepesi.

Jamani ubodaboda siyo kazi nmefkiria Sana,,,we mtu unafanyaje kazi eti mwl unalipwa tsh 400,000/ sijui Askari sh.400,000 alafu useme Lema anatukana watu.

Ni bahati mbaya hatuna watu wa kukuza mijadala Kama hii,,,vyombo vya habari vimekalia uchawa.
 
Kupitia hoja za Lema nimegundua watanzania wana uwezo mdogo wa kufikiri ndio mana hata hayati Magufuli tulishindwa kumuelewa
Magufuli tulimuelewa saaana ndio maana aliwashughulikia wajinga kama huyu kilaza anaetukana watanzania kuwa wanafanya kazi za laana ,ni washamba na ni maskini.
 
Magufuli tulimuelewa saaana ndio maana aliwashughulikia wajinga kama huyu kilaza anaetukana watanzania kuwa wanafanya kazi za laana ,ni washamba na ni maskini.
We sio tu mshamba wa mali na umaskini wa kipato inaonekana pia ni maskini wa Fikra.
Kaa chini msikilize Lema achana na vihabari vya kuokoteza
 
Magufuli tulimuelewa saaana ndio maana aliwashughulikia wajinga kama huyu kilaza anaetukana watanzania kuwa wanafanya kazi za laana ,ni washamba na ni maskini.
Bodaboda kweli ni kazi ya laana,ya kimasikini,na Tanzania kweli ni nchi masikini kila mtu anajua hilo.
 
Back
Top Bottom