Nimemsikia Sheikh Ponda akisema kuwa hakubaliana na Wizara ya Katiba na Sheria kupeleka muswada wa umri wa ndoa kuwa miaka 18

Nimemsikia Sheikh Ponda akisema kuwa hakubaliana na Wizara ya Katiba na Sheria kupeleka muswada wa umri wa ndoa kuwa miaka 18

Naomba mtu mwenye maelezo kamili ya sheikh Ponda atusaidie kuweka hapa!!
 
Mambo ya Waislam yanawahusu Nini wakristo .

Tatizo la wakristo ni Moja kuhalalisha haram kuwa halali na halali kuwa haram.

Mfano Ijumaa ilikua ni sabato takatifu lakini bila andiko lolote wakaibadilisha na kuwa Jumapili.

Ubatizo mwanzo ulikua wa kubatizwa na maji Mengi kwenye Mto au maji yanayotiririka lakini bila kutumia andiko lolote kwenye Biblia wakabadili na kuwa ubatizo wa maji kichwani na kwenye maswiming pool.

Chakula Cha bwana kilikua kinaliwa wakati wa pasaka kama kumbukumbu ya kifo Cha Yesu Tena Kwa kutumia mikate na uzao wa mizabibu usiotiwa chachu lakini ikabadilishwa na kuwa kila ibada ili tu wengine watumie nafasi hiyo kupata mvinyo muda wote . Bila kutumia maandiko .

Bila maandiko yoyote Kanisani watu wanakalia viti na kuingia na viatu Kanisani badala ya kuvua viatu na kukaa sakafuni.

Yesu alisema yeye ni Mwana wa Adam, yeye ni Masihi, yeye ni Mwana wa Mungu , yeye ni Mwakozi, yeye ni Mchungaji mwema , yeye ni njia , yeye ni uhai , yeye ni kweli . Yesu akasema pia kuwa Mungu wetu ni mmoja na ndiye anayepaswa kumwabudu. Yesu akasema pia kuwa hajui siku ya kiama Bali Mungu pekee ndiye anayejua.
Bila maandiko yoyote wakristo wanasema Yesu ndiye Mungu.
Yesu hajawahi kufundisha habari ya Mungu baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu . Bila maandiko yoyote wakristo wanafundisha mafundisho ya utatu ambao haupo kwenye Biblia.

Wakristo wanaweka Masanamu ya wazungu Makanisani na kuyasujudia bila maandiko yoyote kwenye Biblia.

Hapo ni kwamba Wakristo wanataka nchi na SHERIA za nchi zinaegemea matakwa ya kundi Moja la watu katika jamii.

Mila zetu zilizoitwa za kipagai na wapagani wa Ulaya zilikua zinawalinda watoto wa kike na wa kiume mpaka kufikia umri wa kuoa na kuolewa bila kujiingiza kwenye uasherati.
Vijana walikua wanaoa walipofikia umri wa kubalehe na wakike kuvunja ungo.
Leo hii Vijana mpaka wafikie umri wa kuolewa wanakua wameshatoa mimba nyingi na kufanya uasherati wengine mpaka kupemyezewa vitu vigumu kwenye makalio. Yote hiyo ni kwa sababu tumetegemea Wanaharakati wasio na maadili kutupangia haki zetu kama binadam.

Waislam amkeni msikubali kuchezewa na makahaba na wahuni wanayopewa misaada kutoka Ulaya kuvuruga dini kama walivyofanikiwa kuua Ukristo na Kwa nguvu ya pesa.

Suala la Waislam linawahusu Waislam na watoto wao na dini yao Sasa hao Wanaharakati ambao wengi ni Wakristo linawahusu Nini ?

Kama mtu anaona mtoto wake wa kike hataki kusoma au hajafaulu na tayari ameanza mahusiano na mwanaume Kwa Nini asiolewe na huyo mwanaume kuliko kukaa nyumbani na Kisha kuanza kubadili wanaume kama nguo na mwisho kupata ujauzito. ?

Waislam ni jamii kubwa sana hapa Tanzania ,Afrika na Duniani Sasa ni lazima wasikilizwe. Tuliwasikiliza Wapagani wa Ulaya matokeo yake wameharibu vizazi vya wanadamu wengi na kuwakosesha uadilifu kila wanapokuwa .

Ni Bora tuwe na Wasomi wachache waadilifu kuliko kuwa na takataka nyingi zilizojivika Vazi la usomi huku wakiwa ndio wezi ,mafisadi ,wahuni ,Malaya,majambazi, Wala rushwa,waongo, walaghai ,Walevi na kila aina ya mambo machafu kwenye jamii. Usomi huo unasaidia Nini jamii zaidi ya kuiangamiza.

Ukimsikiliza Mbunge Mheshimiwa Dr. Musukuma utaona tofauti ya usomi na utashi na kipaji Cha mtu alichozaliwa nacho ?

Tuwaache Waislam wafaidi kuwa Waislam kwenye nchi yao. Mana nchi hii tangu Karne ya Kumi na mbili uislam Upo. Binadam wakiweza kutumia Rasilimali zinazowazunguka Kwa haki na usawa haya mavyeti yatabaki Kama sifa TU lakini maisha yanakuwa mazuri na rahisi.

Cha msingi ni kuweka SHERIA ya kulinda Wanandoa na watoto wao na sio kuweka SHERIA ya kulazimisha jamii Moja kufuata matakwa ya jamii nyingine .

Wanawake wamekua wengi maofisini lakini Cha ajabu ufisadi ndio unaongezeka.
Ukiangalia aina ya Wanawake mafisadi wengi ni wale wanaovaa viminiskirt na mabega wazi , Wanawake nao wamekua Walevi na mambo ya Kizungu Kizungu ambayo yanahitaji gharama kubwa matokeo yake ni kuingia kwenye ufisadi na rushwa . Jamii ijikite kwenye kupambana na mafisadi yanayorudisha maendeleo ya wananchi nyuma.

Waislam wengi wamejiajiri binafsi Kwa Nini tuwalazimishe kufuata matakwa ya wanaosomea ajira .
Wale wanaoona Elimu ndio kila kitu kwao kutokana na kukalia maofisi na kujikita kwenye rushwa na dhulma basi wasiwahujumu wengine na Imani na dini yao.

Yesu alikuja na kwenda kwenye harusi za kiyahudi ambazo walikua wanaolewa mabinti wadogo wakiwa bikra lakini hakukataza Bali aliacha Mila na desturi zao kama zilivyokuwa .Yesu alichokitaka ni kubadilika na kuwa na matendo mema na kumtii na kumpenda Mungu kuliko vitu vyote huku wakiwapenda pia jirani zao.

Wanaharakati wanatumia misingi ipi kulazimisha serikali kutunga SHERIA kinyume na jamii yenyewe. Sisi ni waafrika ,ndio maana wamasai , Wahazabe, na wengi kule vijijini ndoa zao ni za kimila na wanaoa watoto waliofikia umri wa kuvunja ungo. Sasa hao Wanaharakati wametoa wapi agenda zao.?

Kwa Nini tuwasikilize watu wanaoleta mambo kinyume na Mila zetu ,dini zetu za asili, na hata dini zetu za kutoka Mashariki ya Kati tunazotumia wengi Kwa Sasa. Hao Wanaharakati ni wa Chache Kwa Nini watupangie tulio wengi .

Wanaharakati wenyewe ni wale wasio na ndoa wala familia maalumu . Mama ana watoto wa nne kila mmoja na baba yake. Wangekua wanajali haki za wangine basi wangedumu kwenye ndoa zao Kwa kulinda haki na hisia za waume zao na watoto wanaopenda kuona upendo wa baba na Mama. Sasa wanashindwa kujali haki na hisia za watoto wao halafu wanasema wanajali hisia za watoto wa Waislam mamilioni . ? Haiwezekani . Hawa ni wachumia tumbo. Serikali ikae na Waislam isikilize hoja zao. Hatutaki uhasama na waislam Kwa sababu ya kuwafurahisha watu wachache wanayopewa misaada na wa Wazungu kujidai kuwa wanatetea haki za watoto wakati wanaojenga jamii isiyo na maadili na wathirika wakuu ni watoto.
 
mwenzenu shehe Ponda yupo bize na wakatoliki dah wakatoliki nao wapo bize na pasaka yao basi miaka 18 na sheria ya ukatoliki sielewi yani sheria ya nchi unawataja wakatoliki vipi mzee kuna mkatoliki kamnyma mbususu nini?
 
Yan katka watu ambao hawana akili pamoja na wewe we unadhan saudia ndo uislam. Din ya kiislam inasimama yenyewe kama yenyewe hakuna cha msaudia wala nan mtume amemuowa A'isha akiwa na umr wa miaka 7 na kuanza rasim kuishi nae kindoa akiwa miaka 9 peleka mbele uko upuuzi wako
Kwa hiyo kila alichofanya "Mtume" ni sahihi?
 
Leo nimemsikia Sheikh Ponda akisema kuwa hakubaliana na Wizara ya Katiba na Sheria kupeleka muswada wa umri wa ndoa kuwa miaka 18. Anadai kuwa ni kinyume na dini ya Kiislamu kwa sababu miaka 18 ni sera ya Wakatoliki.

Kusema kweli kwa maneno haya nimeanza rasmi kumdharau Sheikh Ponda kwa sababu nchini Saudi Arabia, nchi ambayo ndo kitovu cha imani ya dini ya Kiislamu ulimwenguni umri wa ndoa ni miaka 18.

Sasa Sheikh Ponda sijui anasema Uislamu gani? Ifike kipindi sasa watu waache kutumia dini kuendekeza tabia zao za kipuuzi. Serikali iko sahihi kuweka umri wa ndoa kuwa miaka 18.

View attachment 2577735
Hakuna andiko linalo sema kuwa rejea ya dini ya uisilamu ni saudia,bali saudia imeamua kuweka kigezo hicho cha miaka 18 kama serikali ikumbukwe serikali ya saudia sio msemaji wa wadini ya kiisilamu qur,aan inamtambua mtoto wa kike akisha anza kuona damu kila mwezi na kuota nywele kwenye kinena kawa mama bila kujali umri wake wewe unge mpinga kwa hoja sio saudia sio kiigizo chetu katika dini bali tunafuata qur,an na sunnah tu sio saudia
 
Waislam Watanzania Wana uchu na uchi wa tuschana tudogo.

Ni wajinga sana, wana maujinga mengi mno.
Msichana mwisho anapo anza kuona damu kila mwezi hicho ndio kipimo chetu ss waisilm kumtambua kuwa tayali apaswa kuozeshwa nyiyi mnamtabuaje mtoto wa kike kuwa kakuawa?
 
Huwezi tenganisha Saudi Arabia na Uislamu, ile ni nchi ya kiislamu rasmi na ndo kitovu cha uislamu na ndo mana hata kuhiji waislamu wanaenda Saudi Arabia.

Kama ingekuwa Quran imesema mtu aoe au kuolewa akiwa mtoto basi wa kwanza kuzingatia walitakiwa wawe Saudia

Wewe mmanyema unaeenda kuhiji Macca Saudi Arabia kwa nini utake kuoa kitoto kidogo wakati unapoenda kufanya ibadan ya hijja wanatambua umri wa ndoa miaka 18?
Kwanza wewe ni dini gani samahani lakini
 
Hiyo quran yenyewe kuna aya kabisa imeandikwa kwamba walishushiwa quran watu waliokuwa wanaishi saudi arabia. Tena kwa lugha yao kabisa ili waielewe..

Wewe mswahili na Quran wapi na wapi huku hata kuisoma unatumia lugha ya wa saudi arabia walioshushiwa quran kwenye ardhi yao.


Waliokuletea dini ya kiislam na kushushiwa Quran wanasema ndoa miaka 18. Wewe mswahili unabisha kwa kisingizio cha kuijua dini
Tatizo lako wewe huna hoja ya msingi swali dogo tu nijibu mtume alituachia kitu gani tukifuate hili tusipotee?
 
Wewe ni muislamu kuliko Wasaudia?
Linapokuja swala la uislamu haizingatii rangi ya mtu Wala taifa lake ndio kigezo Cha ubora kwenye dini .Mwarabu hawezi kuwa bora kuliko Mwislamu asiye Mwarabu kwa sababu tu yeye ni Mwarabu. Bali ubora unatokana na taqwa (uchamungu, kumkumbuka Mwenyezi Mungu). mwenye kumcha Mwenyezi Mungu na kumtii ni bora kuliko mwenzake, bila ya kujali ni Mwarabu au si Mwarabu.

Kama alivyo sema mtume mwenyewe hakuna Bora kwa mweupe kwa asiyekuwa mweupe Wala mwarabu kwa asiyekuwa mwarabu.....Bora kati yenu ni mwenye kumcha mwenyezi Mungu.

Hakuna kitu kama hicho kwenye uislamu.
 
Back
Top Bottom