Nimemsikia Sheikh Ponda akisema kuwa hakubaliana na Wizara ya Katiba na Sheria kupeleka muswada wa umri wa ndoa kuwa miaka 18

Nimemsikia Sheikh Ponda akisema kuwa hakubaliana na Wizara ya Katiba na Sheria kupeleka muswada wa umri wa ndoa kuwa miaka 18

Kwahiyo Taifa tuanze kufuata sheria za dini fulani tuache kufuata sheria za kitaifa

Wakati mwingine wakaage kimya kuliko kujidharaulisha kama hivi

taifa letu halina dini

Hoja ya Sheikh Ponda ni kuwa, hiyo sheria ya kitaifa inatokana na muongoza wa Dini fulani. Je unabisha hilo?
 
Sheria ya mtoto inataka mtoto asiolewe ila sheria ya ndoa inatoa idhini ya mtoto wa miaka 14 kuolewa kwa amri ya mahakama. Sasa watu wanataka kuondoa huo mkanganyiko na kumlinda mtoto ajulikane ni yule aliye na chini ya miaka 18.

Mtoto asiolewe. Shehe apunguze udini maana unaumiza watoto wetu

Mkuu uliwahi kulazimishwa kuwa mtoto wako aolewe akiwa na 14?
 
View attachment 2579272
Leo nimemsikia Sheikh Ponda akisema kuwa hakubaliana na Wizara ya Katiba na Sheria kupeleka muswada wa umri wa ndoa kuwa miaka 18. Anadai kuwa ni kinyume na dini ya Kiislamu kwa sababu miaka 18 ni sera ya Wakatoliki.

Kusema kweli kwa maneno haya nimeanza rasmi kumdharau Sheikh Ponda kwa sababu nchini Saudi Arabia, nchi ambayo ndo kitovu cha imani ya dini ya Kiislamu ulimwenguni umri wa ndoa ni miaka 18.

Sasa Sheikh Ponda sijui anasema Uislamu gani? Ifike kipindi sasa watu waache kutumia dini kuendekeza tabia zao za kipuuzi. Serikali iko sahihi kuweka umri wa ndoa kuwa miaka 18.

View attachment 2577735
Ni tatizo kubwa sana kuwa na kiongozi wa dini anayedhani ndoa ni kuti.ana tu. Psychological maturity ambacho ndicho muhimu sana katika ndoa huanza kukomaa mtu anapofikisha miaka 18.
 
Mimi Sikubaliani na kauli ya sheikh ponda kwa kuonyesha kana kwamba Kuna umri umewekwa kwenye Quran wa ndoa ,Quran haijataja umri mwanamke kolewe Bali kilichoelezwa kwenye Quran ni kwaba inazingatia utu uzima wa akili (rushdh) ndio kigezo Cha ndoa.
(4:6)

Quran inazingatia ukomavu wa kiakili (ambao siku zote huangukia zaidi ya umri wa balehe) kuwa msingi wa kufikia umri wa kuolewa. Hivyo mwanamke anapofika hatua ya kukomaa kiakili na kimwili ndio muda wa kuolewa kwa mujibu wa Quran

sio sawa kuiita Sheria ya miaka 18 ni mfumo wa kikatoriki , kwa Sababu kwa Karne yetu kwa mabadiliko tuliyokuwa nayo mwanamke wa 18 yrs ndio anaweza kuingia sifa zilizotajwa na Quran

Na hii ndio Sababu Quran haikutaja umri wa mwanamke kuolewa,kama labda ingesema akifika miaka 14 aolowe ingekuwa ni disaster ukiangalia hata mtaani kwako mwenye umri huo bado mtoto hajakomaa mwili Wala akili.

Japo hio ilikuwa kawaida miaka ya zaman jamii za kiyaudi kipindi Cha yesu , Issac na Joseph vilifanyika sana hata huko ulaya wafalme wengi walioa under 18 na labda kwasababu wenzetu walijaaliwa miili mikubwa iliyopevuka mapema.

Mkuu kama wewe ni muislamu upo kwenye hasara
 
Mkuu uko sawa kweli? Kwahiyo Kila wanachofanya wazungu unataka na sie huku tuige sio? Hayo hayo majimbo unayoyasema yanaunga mkono ushoga kwahiyo unakubaliana nao?

kwani nyinyi mnaiga nani? hiyo dhana ya kuwa mtumzima ni kuanzia 18 years unafikiri imeletwa na nani kama sio wazungu?
 
Wanaume wa kiislamu wanatakiwa kupinga ndoa za utotoni

Muislamu hatakiwi kuishi kwa mawazo yake, Bali kwa taratibu alizopangiwa katika dini yake. Sio watu wote na mapagani kama nyinyi.
 
Kwanini unalazmisha kuitaja Saudi Arabia katika jambo linalohusu uislamu na Qur'an?

Ama saudi Arabia ni mtume katika uislam?.

Sioni mantiki yoyote ya wewe kuirejea Saudi Arabia katika jambo lolote linalohusu uislamu na Qur'an.
Acha ujinga wewe ngumbaru. Hao ndo walowaletea uislamu nyie makenge. They are more muslims than you stupid monkeys
 
Kwani UN inasemaje Kuhusu umri wa mtoto unaishia miaka mingapi?
Watu wasitumie dini. Sheikh asituzingue. Hiyo haki anayopigania kila siku ndio hii?
Katiba inasema miaka 18 mtu tu aje na miaka yake kwa manufaa binafsi. Asituzingue

kwahuyo UN kwako ndio wakuwamini kuliko Dini unayifuata?
 
Pamoja na kufunga tena mtu mzima na akili zake anakuja na upumbavu kama huu🤔🤔, wanawe wangapi wameolewa wakiwa na miaka 14, tamaa zao za mwili wao watu wachache zisiwanyime watoto haki zao za msingi
 
Wagalatia kwanini munateseka na Uislmau? Kwani mumelazimishwa nyinyi kuoza mabintu wenu wakiwa na 15? Waachane wanaotaka wafanye, na acheni kuteseka na Imani za watu.
 
Hujui kitu, na ukitaka kujua fanya tafiti ujue hadithi ni nini.

Kama vile ktk bible ukiulizwa wapi Yesu kasema mimi yesu ni Mungu. Hutopata. Lkn yako maandishi ya Paulo yanayosema Yesu ndie mungu.

Sasa nikikwambia maneno ya Paulo ni uongo Uliotengenezwa utasema ninakana, naona aibu.?!?!

Hadhithi zimechezewa sana na ilivyochezewa biblia.

Yesu kazingiziwa Sana na biblia. Muhamad kasingiziwa mengi kupitia hadithi.

Quran imebaki kuwa safi na hatoweza kuchafua kwa kuwa imefungwa kwa code maalum
Na kumbuka hakuna sehemu kwenye biblia Yesu anasema YEYE SI MUNGU.
wanaosema si Mungu uishia kujenga hoja tu si kutoa ushahidi kwenye biblia.

By the way ponda ana hoja.. Ponda karejeaa mafundisho dini yake kuhusu ndoa ila watu wanarejea sheria ya Saudi arabia kuhusu ndoa ili kuzima hoja ya Ponda.

Saudi Arabia na uislamu ni vitu viwili tofauti, wanao lazimisha kuwa ni kitu kimoja either ni wajinga ama wanaitumia Saudi Arabia kukwepa hoja ya msingi ya ponda.
 
Muislamu hatakiwi kuishi kwa mawazo yake, Bali kwa taratibu alizopangiwa katika dini yake. Sio watu wote na mapagani kama nyinyi.

Haya endeleeni kuozesha watoto wenu wa miaka 14
Ila madhila yanayowapata wengine wanajuta kuzaliwa na wengine wanakimbia ndoa na kuishia kusitirika kwa hao mnaowaita mapagani. Sasa sijui hekima ya Mungu ndani yenu ilienda wapi
 
Sipendi kuzungumzia sana historia. Kwani si kazi yetu sisi wanadamu kuisoma na kiubugu kama tunavyofanya, kutaka kukaza mishipa ya shingo kukutolea maandiko ya historia ambayo hayana msaada wowote kwetu kwa sasa.

Historia inafanya kazi kipindi hiki pale tu unapoona kwamba una matatizo, na tunachotakiwa kufanya ni kuchunguza njia ya kihistoria inayotumiwa duniani kote na wengine ambao walikuwa na matatizo sawa na yetu.

Na unapogundua wao jinsi walivyopata suluhisho wasi tukocopy kuumiza kichwa ni jinsi gani unaweza kupata masuluhisho ya kwaako..

Kama alivyokuwa Yesu, Muhammad pia hawakutaka kukariri historia walizozikuta. Walitaka wao watengeneze historia yao. Kwa maana nyingine badala ya sisi ya kulipa kazi ya kusema historia; sisi tunapaswa tuipe kazi historia ituandike.

We need to make history than read history.

Lakini tuelewane historia utakayoiandika leo baada ya 50 itakuwa imeshapotoshwa na waandishi kwa asilimia 99%.

Sawa na vitabu vya dini. Kalamu za waandishi zimeifanya kuwa uwongo. (Yeremia 8:8)

Kwa kuzingatia hilo Quran ikawekwa Code ili anaetaka kupotosha ajione mwenyewe yu mjinga.


sasa moja ya sifa ya hadithi ni lazima iendane na ayah ya quran. Ambayo hii haina mashaka. Pili moja ya sifa ya quran ibaendana na kanuni ya naumbile (universal). Aya zote ziko hivyo.

Sasa ukiona hadithi unapingana na kanuni za maumbile hizo ni hadithi bandia au hutumika neno Dhaifu.

Sahihi bukhari ni kitabu kilichotungwa miaka 200 iliyopita. Kinaweza kuwa na mapumgufu kwa bahati mbaya au yaliyotengezwa.

======
nijibu sasa imgawa siko tayari kuendelea na

Hakuna Mahali Paulo amesema Yesu ni Mungu. NARUDIA TENA, HAKUNA. Na hata nikikuambia unioneshe hapo mahali HUTOWEZA, kwa sababu Hapapo.

Tito 2:13 Warumi 9:5 Wafilipi 2:5

Pili, Bible haijachezewa... nikikutaka unionyeshe mahali Bible ilipochezewa HUTAWEZA kunionesha.
Yeremia 8:8

=======

Muhimu wasichana mwenye matamanio na aoelewe.

Hakuna kuendeleza zinaa na mkishajuana kuja kama mnavyopigania.

Ibaki hivyo. Tusije ondoka mwenye
mada kuu.

Na ukitaka ushahidi wa hadithi ndio huo hadithi yyt isiyoendana na Quran, au maumbile hilo si andiko na mwongozo wa waislam hao ni kina luka na Theofilo ambao hata yesu hakumuona lkn nao ni mwanafunzi wake. Luka 1:1

Unaweza kuwandikia historia sahihi ya uhuru watoto wako ambapo wewe hukushuhudilia.
Historia haina maana yyt iwapo tutaamua kuiabudu.

Mjadala mkuu ni kutaka kutengeza historia ya watoto wetu

Na suala muhimu la kulijadili na pengine kulipigia kura ni je watoto wetu aruhusiwe kuoa au kuolewa huku zikiendelea kusoma au waendelee kufanya zinaa huku zikiendelea kusoma.

Bila shaka kura za maoni zitaakisi matenzo yetu tuliyoyashadidia na kutaka jamii yote iige.

Sisi wengine hatuko tayari kuoshi kwanza kwa kusomana na baadae kubariki ndoa. Si ktk mafundisho ya Elio au Allah
Mohamad alimuoa aisha akiwa na miaka 6 na akalala naye akiwa na miaka 9.

Ni mambo ya aibu, ila Huo ndio ukweli wa vitabu vyenu mlivyoandika wenyewe.

Usipingane na ukweli mliouandika wenyewe.
 
kwani nyinyi mnaiga nani? hiyo dhana ya kuwa mtumzima ni kuanzia 18 years unafikiri imeletwa na nani kama sio wazungu?
Na kwa hili wazungu wapo sahihi. Hata waarabu wa Saudi Arabia wamewafuata wazungu...mmebaki nyie waarabu wa ikwiriri tu
 
Back
Top Bottom