Mkuu kuna sehemu nimesema kubwia unga ni jambo la kimwiliKwa hivyo kuvuta madawa ya kulevya sio shida ma'am ni mwili tu. Tuache utapeli. Unapokuwa mtumishi wa Mungu lazima uwe kielelezo Cha uungu sio shetani. Hizo tattoo Wala sio za wakati wa Muziki Bali amechora zingine ndio maana anapenda kuacha mikono wazi.
Vya bure vina gharamaLast week niliandika Uzi hapa kuhusu namna unavyo weza kutengeneza pesa, network na connection kwa kufanya kazi ya KUBADILISHA UPEPO kuhusu watu wanao tuhumiwa au nyooshewa vidole na jamii kuhusu mambo mbalimbali.
Leo nimefanya jambo hilo kwa vitendo na nimekuwa monetary rewarded.
Ni hivi kama siku mbili zimepita zimesambaa picha mitandaoni zikimuonyesha mtu anae itwa Prophet Lovi.
Watanzania wana question kuhusu utumishi wa huyo mwamba kwa sababu.
1. Ana tatoo.
2. Ana rasta.
3. Ana vaa kipini.
Huko insta kwenye page husika, Mimi niliweka comment moja tu kwamba " watanzania Msiwe wavivu wa kufikiri hizo tatoo alizichora akiwa bado hajaokoka"
Dakika kumi nyingi nimepokea dm kutoka kwa mmoja kati ya sponsors wa mkutano wa mh.nabii.
Jamaa kapendezwa na comment yangu na kaomba niingie kwenye kamati ya (jina kapuni) na kibunda cha awali kimethibitishwa kwenye simu yangu (hawa jamaa.kumbe wanapiga hela sana aisee. Am thinking about something now)
Ndugu zangu katika zama hizi za maisha ya mtandaoni tujifunze kuzitumia fursa vizuri. Kila kitu ni fursa.
Tujifunze kutazama mambo kwa jicho la Engineer au mganga wa kienyeji.
Wakati nyinyi mnaona mto,ziwa au bahari, injinia anaona daraja.
Wakati wewe unajiona upo Sawa, mganga anakuona una jini mahaba.
Kwa hiyo, mtu kumsemea mwingine na anachokiamini ni kuwekwa kwenye payroll?Wewe ushawekwa kwenye payroll tunajua.
LIKUD alisema mwenyewe kwamba amewekwa kwenye payroll.Kwa hiyo, mtu kumsemea mwingine na anachokiamini ni kuwekwa kwenye payroll?
Wewe umekuwa mdau mkubwa wa kupinga uwepo wa Mungu, je nawe pia upo kwenye payroll ya Wapingaji hao?
Acha uongo tattoo zingine kajichora akiwa tayari kaacha muziki. Pia kuhusu kipini umetudanganya huyo Nabii sio Mshona Wala Nini ni mkongomani aliyezaliwa na mama wa kikenya. Halafu kasome Biblia vizuri Samson hakuwa rasta Bali alikuwa na nywele nyingi.
Huyo ni mfanyabiashara wa dini kama ilivyo kina Mwamposa.
Mavazi yake na muonekano wake kwa ujumla ni sehemu ya packaging aliyochagua kufikia hadhira yake.
Mwisho wa siku wajinga ndio waliwao.
Kesho utaona vijana wa kupenda vinjunga watakavyojaa kupakwa mafuta.
Achana na hearsay.LIKUD alisema mwenyewe kwamba amewekwa kwenye payroll.
Mimi sikuwahi kusema niko kwenye payroll.
Mimi sijasema chochote ambacho LIKUD hajasema mwenyewe.
Ushaelewa?
Kama hayupo kwenye payroll thibitisha hilo, pia ni kosa lake na stahili kuchukuliwa kuwa yupo kwenye payroll.Achana na hearsay.
Una uhakika kuwa amewekwa kwenye hiyo payroll? Ama anabwabwaja?
Tukikuambia utuletee kithibitisho kuwa yupo kwenye payroll utaleta? Kama huwezi kuleta kwa nini uamini kiasi cha kueleza jukwaani kwamba yupo humo?
Si wewe ambaye kila wa leo unatafuta kidhihirisho cha wazi kuwa Mungu yupo? Na kwa kuwa haonekani wazi, umekuwa ng'ang'ari kila wakati?
Kwa kuwa umemuamini LIKUD kwa maneno yake pasipo kukuthibitishia, kwa nini huwa unawaona waaminio kuwa mahayawani? Nawe pia hayawani kwa muktadha huo?
Umeelewa?