Nimemuelewa DC Sabaya, inawezekana kabisa Godbless Lema alisaidiwa na CCM Arusha kwenda uhamishoni!

Nimemuelewa DC Sabaya, inawezekana kabisa Godbless Lema alisaidiwa na CCM Arusha kwenda uhamishoni!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
DC Ole Sabaya amesema mambo mawili makubwa:

Mosi, CCM Arusha kuna kandarasi ya majungu ambayo mradi wake mkubwa ni kuwapiga vita wazalendo wa kweli kama yeye.

Pili, Kuvuka mpaka na kwenda kupata ukimbizi nchi nyingine siyo jambo rahisi na mtu mwepesi mwepesi kamwe hawezi kupata fursa kama hiyo.

Lakini, kwa nyongeza kasema Kandarasi ya majungu ya CCM Arusha inamtumia mkimbizi Ansbert Ngurumo kumchafua.

Niliwahi kujiuliza iliwezekanaje Godbless Lema kufanikiwa kuondoka nchini akiwa na familia yake yote hadi beki tatu?

Nimemuelewa sana DC Ole Sabaya.

Maendeleo hayana vyama!
 
Lema ni jemedari asiye na kifani. Hapo aliwapiga vibaya UVCCM, CCM, pamoja na washikilia bunduki-Man U. Walikuja kuzinduka baada ya jamaa mwenyewe kutoa taarifa kuwa yuko upande wa pili wa mto anapiga msosi. Walichanganyikiwa sana hadi wakatamani kuvuka mpaka kumrejesha nyumbani Kenya ikakaza wakaufyata wakarudi wakitoa sauti mithiri ya mbwa aliyekimbizwa na fisi.
 
Dc sabaya ni mwajiriwa huko Hai kilimanjaro, anaishi nyumba ya serikali huko Hai, kilimanjaro. Inakuaje kila siku anazingumziwa kwenye matukio ya arusha? Ninashauri pangua pangua inayokuja ya kuwahamisha wakuu wa Wilaya ,sabaya apangiwe kuwa DC wilaya ya kakonko au biharamulo.
 
Nadhani ndio atapewa mkoa wa Arusha!
 
Back
Top Bottom