Nakusapoti mkuu. Mi nakaribia mwaka wa pili nilimuachia kila kitu nikaanza upya.
Iko hivi mwaka 2019/2020 ndio nimemaliza chuo nilipanga na mke wangu hapa centa yetu, msimu ukafika nililima mpunga majuruba ya kwetu nusu ekari, kwao tulipewa ekari moja na nusu, tukavuna kama gunia 25, majuruba ya kwao tulipata gunia 18. Nilianza kusimangwa kwa hivyo vigunia kulivyolima kwao.
Ikafika nikawa naambiwa sina lolote, siwezi hata kuajiriwa. Nilichofanya niliuza gunia 7 za mpunga tulizopata kutoka majaruba ya kwetu, vingine vyote nilimwachia, vitu vya ndani, mpunga na gunia za mahindi tano. Nilianza upya sahiv afadhali, yeye akauza mpunga akapewa kiwanja hapohapo kwao akajenga slopu mbili chumba na sebule.
Saa hivi naambiwa tujenge tuwe wamoja hapo alipo amepachoka, maana alipojenga kuna mkubwa wake pia single mother na watoto watano, jumlisha kwao, msongamano unamsumbua.