Nimenunua pikipiki sijui kuendesha vip hawa vijana hawatanipiga hesabu za siku?

Nimenunua pikipiki sijui kuendesha vip hawa vijana hawatanipiga hesabu za siku?

Mkuu Mimi ninafanya hii biashara unachotakiwa ni kufunga naye mkataba wa miezi kadhaa ambapo kila wiki isipungue 70,000/=

Mimi kila wiki analipa 75,000/= ambapo kwa mwezi ni Tsh.300,000/=

Mafuta, oil na service nyingine juu yake, akimaliza muda wa mkataba bila shida anachukua Pikipiki.

Kiukweli zinalipa, usikatishwe tamaa pambana!

NB: miezi ya mkataba inategemeana na Bei Yako uliyonunulia ili pesa irudi na Faida upate ya kutosha.
 
Hata kama huwezi kuendesha ndio ujaze Oil ful tank?

Unatakiwa kujaza Fuel full tank oil unaweka lita moja tu baada ya muda kadhaa kutokana na mizunguko yako...
Kwa piki piki ili usipate tabu
Mpe mtu mkataba kila siku uletewe 10
Nakazia
 
Wale wazoefu naomba msaada jinsi ya kuweza kuepuka kuletewa hesabu finyu. Nimewza niwe najaza oil full tank then yy anipe hesabu yote kisha nimlipe mwisho wa mwezi. Naomba ushauri, pia maeneo gani yana kua na wateja wa kutosha ili dogo atege hayo maeneo. Nipo iringa.
Nunua na dawa za presha kabisa hapo naenda kuu wa mda si mrefu. Yani we ukae tu mtu akutafutie pesa akuletee na yeye anamahitaji yake na hana pesa. HAIWEZEKANI
 
Mkuu Mimi ninafanya hii biashara unachotakiwa ni kufunga naye mkataba wa miezi kadhaa ambapo kila wiki isipungue 70,000/=

Mimi kila wiki analipa 75,000/= ambapo kwa mwezi ni Tsh.300,000/=

Mafuta, oil na service nyingine juu yake, akimaliza muda wa mkataba bila shida anachukua Pikipiki.

Kiukweli zinalipa, usikatishwe tamaa pambana!

NB: miezi ya mkataba inategemeana na Bei Yako uliyonunulia ili pesa irudi na Faida upate ya kutosha.
Nakushukuru mkuu vip ushamalizana nae?
 
ili aje atuvunje viuno barabarani..?
Kuna mwana mmoja kitaa mjivuni sana mtu wa Tambo alikuja na pigo hizo hizo kusema pikipiki anaweza kuendesha lakini watu wanajua hajui

Wana wakasema hawez , kwa nini asifosi watu wakampa chombo alafu mazingira yenyewe sio mazuri kwa mtu anayejifunza ni bora,ingekuwa uwanjani,
Jamaa akapanda chombo kspiga stata kaingizd gia fresh sasa akavuta moto kwa kasi akaichia na krachi 😀😀 ebhana ile pikipiki ilianza kuandoka kwa kasi asijue afanye nini huku anaongeza moto ulikuwa noma sana asee ilimtupa vibaya sana
Watu huku kicheko sababu ya ujuaji wake
 
T
Keshajimix
Madogo wengi wanaofanya hii kazi wana ulimbukeni.
Akianza kushika vihela vya ghafla anajisahau,wanawake aliokuwa anawaota kwenye ndoto atataka awagegede wotee.
Hapo ndo boss utakapoanza kujutaa
Tatizo wanapokuwa na shida wanakuja mikono nyuma na shingo upande wakishaanza kupata pesa wanakuona kavu hesabu utapata kwa manati

Vijana wa boda uaminifu ni zero
 
Wale wazoefu naomba msaada jinsi ya kuweza kuepuka kuletewa hesabu finyu. Nimewza niwe najaza oil full tank then yy anipe hesabu yote kisha nimlipe mwisho wa mwezi. Naomba ushauri, pia maeneo gani yana kua na wateja wa kutosha ili dogo atege hayo maeneo. Nipo iringa.
1. Mpaka hapo pikipiki yako itakuwa imeharibika (oil full tank badala ya petrol)

2. Hakuna biashara yenye risk kama bodaboda, huwezi kumlipa mwisho wa mwezi kwasababu kuna wakati biashara huwa mbaya.

3. Jifunze kuendesha mwenyewe

4. Siku nyingine usianze kununua vifaa kisha ndio ujifunze kusimamia. Fanya unachoeeza kusimamia
 
Tafuta kijana mpe mkataba. Hapo utafanikiwa vingenevyo jipange kugombana nao kila siku
 
Back
Top Bottom