Nimenusurika kufa usiku huu na ajali

Nimenusurika kufa usiku huu na ajali

Jamani ajali haina kinga,

Gari aina ya canter imekuja kugonga chumbani kwangu, baada ya kuferi breki. Inaonekana lilikuwa limepaki sehemu, likajaa wanguwangu mpaka chumbani. Kishindo nilichokisikia kilikuwa kikubwa sana, tena ukitegemea nilikuwa usingizini Mungu mkubwa hakuna aliyeumia, kwenye gari kulikuwa hakuna mtu
Sema kwenye gari alikuwepo dereva peke yake...ukisema hakukuwa na mtu unamaanisha hata dereva hakuwepo, sasa hilo gari lilijiendesha lenyewe?
 
Pole na hongera kwa kupata gari lishakuwa lako hilo🤣
 
Kama watu hawakuona ..hilo gari lifungie tu humohumo ndani...chakuokota hakina baya
 
Nimefunga swahumu mwezi mzima,yaani nimeshatajitayalisha na kanzu zangu kwa ajili ya kwenda kuswali kesho,ndiyo yametokea haya,kila kitu hupangwa na Mwenyezi Mungu.
Ungekufa hali ya kuwa umefunga si fahari hiyo? kufa Ktk hali nzuri kama wengine wanaokufa wakiwa wanahiji au msikiti wanaswali (joking)
 
Jamani ajali haina kinga,

Gari aina ya canter imekuja kugonga chumbani kwangu, baada ya kuferi breki. Inaonekana lilikuwa limepaki sehemu, likajaa wanguwangu mpaka chumbani. Kishindo nilichokisikia kilikuwa kikubwa sana, tena ukitegemea nilikuwa usingizini Mungu mkubwa hakuna aliyeumia, kwenye gari kulikuwa hakuna mtu
Pole sana Mkuu, MUNGU ni mwema.
 
Pole mkuu, picha usisahau ili tuone hali halisi
 
Sema kwenye gari alikuwepo dereva peke yake...ukisema hakukuwa na mtu unamaanisha hata dereva hakuwepo, sasa hilo gari lilijiendesha lenyewe?
Kwa nini unamlisha maneno,amesema kulikua hakuna dereva mbona kaeleweka,hiyo gari dereva alisahau kuweka hand break,pia wengine uweka Mawr kabisa kwenye tairi au vigogo,gari lilikua apo kuna kimteremko
 
Sema kwenye gari alikuwepo dereva peke yake...ukisema hakukuwa na mtu unamaanisha hata dereva hakuwepo, sasa hilo gari lilijiendesha lenyewe?
Samahani nilikuwa kwenye swala ya Iddy ili kumshukuru Mungu yawezekana leo ningekuwa nazikwa,yaani nimesikia kishindo kikubwa na kuona udongo ukimwagika ndani,sasa nyumba ninayoishi iko kalibu na barabara nikajua gari imegonga nyumba.

Kuchungulia dirishani natizamana na canter uso kwa kwa uso,baada ya kutoka nawakuta wenye gari,wanasema walikuwa wameipaka kuja kuaangalia wanakuta gari inatembea mbana umbari wa kama mita 90 ndiyo kuja kugonga chumbani kwangu
 
Wawe wanaweka kigingi wakipaki kwenye mteremko
 
.... hakuna aliyeumia! mwenzetu una wake wangapi humo chumbani?
Yaani huwezi kuuamini nilikuwa na bibi mdogo,bibi mkubwa yuko Tanzania,na jana tumenunua mazagazaga yote kwa ajili ya kupika leo,na kanzu yangu nimeitayarisha kwa ajili ya swala ya Iddy,kifo kinafumbo kubwa sana.
 
Kesha kuambia lilikuwa limeegeshwa, dereva aliliacha bila kufunga breki ya mkono na huenda kuna mteremko.
Gari imekuja peke yeke,kulikukwa hakuna mtu,yaani kosa varanda ya mbele ya unyumba wenda leo ningekuwa maiti,maana ukuta ungenifunika
 
Hu
Ungekufa hali ya kuwa umefunga si fahari hiyo? kufa Ktk hali nzuri kama wengine wanaokufa wakiwa wanahiji au msikiti

Ungekufa hali ya kuwa umefunga si fahari hiyo? kufa Ktk hali nzuri kama wengine wanaokufa wakiwa wanahiji au msikiti wanaswali (joking)
Yaani acha tu,kifo hakina Hodi,na kanzu yangu nilikuwa nimeianda kwa ajili ya swala ya Iddy,na Alarm nimeweke kwa ajili ya kuniamsha swala ya Alfajiri.Lakini nashukuru nimejihimu msikitini,na kufanya kazi ya kutandika maturubai uwanjani kwa ajili ya swala Iddy,na nimefanya kazi kwelikweli ilikuwa kila nikikumbuka usiku wa ajali
 
Back
Top Bottom