Nimenyimwa kibali baada ya kuomba kujenga Magereza binafsi

Nimenyimwa kibali baada ya kuomba kujenga Magereza binafsi

Katika nyakati hizi ambazo ajira ni changamoto . baadhi ya wawekezaji hatupewi nafasi ya kutosha katika kutimiza ndoto zetu za uwekezaji.

Nimetoa pendekezo kuhusu kujenga magereza binafsi pamoja na mortuary binafsi.

Ila naona feedback ni ndogo Sana . Magereza binafsi zingekuepo hizi ndo faida zake

Kutoa ajira. Kuweka mazingira bora Kwa mahabusu na wafungwa.

Kuisadia serikali katika kuhudumia wafungwa na mahabusu.

Vile vile mortuary binafsi zingetoa ajira, Zingeisadia serikali

Tuna low thinkers wengi katika ufanyaji maamuzi.
anzisha kituo cha fire uwe na magari yako kwa ajili ya majanga
 
Gereza zima linaendeshwa kibiashara.

Kampuni inalipwa na serikali kwa kuhesabu wafungwa, hivyo inakuwa na incentive ya kuongeza wafungwa.

Pia, wafungwa wanauziwa goods and services at inflated prices. Kuna mchizi wangu alikuwa ndani huku US kuongea naye kwenye simu tu ni maumivu makubwa sana kwa sababu unaweza kutumia karibu dola moja kwa dakika kuongea naye.

Makampuni yanafanya Magereza kama real estate deal yanawachaji serikali bei ya juu kama.kuwakodisha.

Makampuni yana lobby kupandisha bei ya vitu ili kupata faida zaidi. Suala zima la watu jufungwa linakuwa biashara tu badala ya ethics za kubadiki watu.

Pia wafungwa wanafanyishwa kazi sehemu nyingine hata kinyume na masharti ya ILO na haki za binadamu.

Kifupi watu wanaangalia wafungwa kama vichwa vya kutengenezea pesa tu.
Aseee shukrani sana , kwa maelezo murua
 
Mkuu omba kibali cha kujenga mochwari , wakikupa kibali unaongeza huduma ya mazishi kwa njia mbali mbali kuna wanaotaka kuzika kwenye makaburi , kuna wanaotaka kuchoma miili na kuna baadhi wanataka kuozesha miili kwa ajili ya kutengenezea mboji "composite"

Unatengeza facility yako una offer hizo huduma na unatoa elimu kwa raia kwamba sio lazima mtu azikwe , anaweza kuchomwa familia ikatunza majivu au anaweza kuozeshwa kwenye kifaa maalum kwa siku 90 then ile mboji iliyotokana na mwili wake ikatumika kuoteshea miche au mimea ikaweka kumbukumbu kwamba mtu huyo hajafa ila amebadili mazingira na kuwa mmea

Zipo njia mbalimbali za mazishi.

Hapo hapo kwenye taasisi yako unaweza ukaanzisha ujengaji wa makaburi yaan zile tombstone za kibabe na ujengeaji wa makaburi kwa design nzuri kulingana na familia itakavyonyoosha mkono 🤣

Pia unaanzisha website ambayo watu inakua na list ya makaburi yote hata kama sio uliyoyaandaa wewe ambapo utaweka historia za hao waliofariki picha zao kama unaweza kuzipata hayo makaburi unayasajiri unatembelea grave yard zote hapa bongo hata za jeshi na makanisani ! Hata kama itakua ni tarehe( kuz-kufa) na majina ya marehemu, picha n.k

Mkuu nitafute tuongee 🤣🤣
 
Back
Top Bottom