Nimeoa wiki mbili tu zilizopita lakini tayari nimechoshwa na maisha haya

Nimeoa wiki mbili tu zilizopita lakini tayari nimechoshwa na maisha haya

Sasa we ndugu kama umefungua biashara bila kufanya utafiti wa eneo, wateja aina ya bidhaa faida yake, je Biashara ikikudodea unalaumu wafanyabiashara wengine? Ebo, Lete kisa hapa kwa nini kanuna? Tunataka tukalale na wake zetu. Na wewe ulioa kwa lengo gani?
 
Nimeoa wiki mbili tu zilizopita, lakini tayari nimechoshwa na maisha haya. Nahisi kama ninaishi maisha ya kipumbavu . Nashangaa jinsi watu ambao wamekuwa kwenye ndoa kwa miaka mitano au zaidi wanawezaje kuvumilia huu ujinga!

Niko kitandani na huyu Binadamu , lakini ameninunia tangu jana. Nimejaribu kuzungumza naye, lakini hataki kuonyesha ushirikiano .

Nafikiria kumfukuza arudi kwao.

Nadhani ni bora niishi peke yangu kuliko kuishi na mtu huyu.

Ninahisi kuchanganyikiwa na kukata tamaa. Je, kuna mtu yeyote anaweza kunipa ushauri?
Kammis msela wake anatafta sababu akapashe kiporoooo
 
Ndugu inabidi uwaelewe wanawake aisee.Haya mambo hutaambiwa au kufundishwa na mchungaji wako au padre haya mambo utaambiwa na wanaume wenzio.
1.Jitahidi usimind vitu vidogo hivyo
2.Wanawake wako very complex kuliko wanaume - wanahisia na kusumbuliwa na vitu vingi.
3.Jifunze mkeo akinuna usimchokonoe na kupambana kujua tatizo ni nini au ukaanza kujihisi.Utakuta hata wewe huusiki wala hakuwazi wewe - hormones zimechangamka au ana mambo personal yanamsumbua
4.Kuwa busy: na kama huwezi basi nenda katembee huko kwa wadau piga moja mbili ukirudi nyumbani unapumzika
5.Usilazimishe kula mzigo kama unavyoshauriwa humu - utazidi kuharibu - just give her space atakuwa tu sawa.
6.Tambua hata unyumba jiandae kupitisha hata miezi 4 - usije sasa ukarudi humu kuanzisha uzi wa kuvunja ndoa kisa mzigo.
7.Uliza wanaume wenzio wanasurvive vipi then jifunze, acha kulalamika mitandaoni au kwa watu wa mtaani ovyo utamdhalilisha na wote mtajivunjia heshima.
Unalalamika kununiwa hivi husomi mitandaoni wenzako wanafilisiwa na wake zao wa ndoa wanarudi kuwa maskini.Ishi na mkeo kwa akili - muelewe, mchukulie madhaifu yake, sononeka, muonee huruma, they are very weak physically, emotionally n.k Wanaume wote unaokutana nao nje huko wana mabalaa hili la kwako cha mtoto - wengine wanakutamia kabisa - watu wanabeba misalaba sio mchezo.
Asante kwa ushauri wako, nimekuelewa vyema mkuu!
 
Nimeoa wiki mbili tu zilizopita, lakini tayari nimechoshwa na maisha haya. Nahisi kama ninaishi maisha ya kipumbavu . Nashangaa jinsi watu ambao wamekuwa kwenye ndoa kwa miaka mitano au zaidi wanawezaje kuvumilia huu ujinga!

Niko kitandani na huyu Binadamu , lakini ameninunia tangu jana. Nimejaribu kuzungumza naye, lakini hataki kuonyesha ushirikiano .

Nafikiria kumfukuza arudi kwao.

Nadhani ni bora niishi peke yangu kuliko kuishi na mtu huyu.

Ninahisi kuchanganyikiwa na kukata tamaa. Je, kuna mtu yeyote anaweza kunipa ushauri?
Atakuja akuue huyo mental health is real mkuu inaweza ukawa unaishi na mgonjwa wa akili
 
Back
Top Bottom