Nimepanda basi toka Dar kwenda Mwanza kukiwasha japo kwa shingo upande

Kwahiyo we unaamini ikiingia chadema madarakani itakonga nyoyo yako? Yani kwamba ndo bei ya mafuta na mchele itashuka? Kwamba mafisadi ndo hawatokuwepo. Huyo aliekuja na kutanguliza agenda ya kutaka kulipwa milioni mia zake na madeni yake ya kujitibia🤣 kwahiyo watu wazima na sharubu zenu mnaamini kaja kwaajili yenu🤣🤣🤣🤣
 
Naelekea Mwanza kwenda kukiwasha.

CCM ni janga la taifa. Limezidi kuwakandamiza watanzania kwa kuendeleza umasikini. Tozo haramu, ufisadi na ubwanyenye.

Nitakiwasha jukwaani uwanja wa furahisha mpaka kieleweke.
Huna nafasi hiyo wewe ndani ya cdm labda umeenda kuvua dagaa tu.

Ulishafukuzwa cdm kipindi kirefu yanini kufuatilia mambo ya cdm?

Ulipofukuzwa ulisema kuwa ccm wanakuhitaji sasa yanini tena cdm?
 
Tena ndio WaTz watakufa kwa sonana hadi waseme hiki nini
 
Huu mnyororo wa wizi ni mgumu kukatika pasipo kusimamia katiba
Utasema CCM ni kweli wengi huenda huko kwa sababu ni chama chenye mamlaka wakijua ndo sehemu ya kupata mamlaka (cheo) / uongozi Ili wapate hela ukitaka kuamini Hilo watu wanafata hivyo vitu siku chama pinzani kishinde uone watu wanavyorudisha kadi na huhamia chama kilichoshinda

Waungwana njaa mbaya asilimia chache wenye Nia thabiti na hili taifa nao wamefunikwa nguvu na wachepushaji kikubwa tuwe na sera nzuri kusimamia katiba. Binafsi wapo baadhi ya viongozi nakubali juhudi zao ila Kuna sehemu zingine uozo mwingi
 
Kuwasha nini?Kumuwashia nani?Kama una namna ya kuweza kushusha bei ya unga wa ugali uwe chini ya 1000 na Mchele uwe chini 2000 na petrol iwe chini ya 2000 na mafuta ya kula yawe chini ya 4000 basi utakiwasha kweli.Ila kama ni kwenda kupiga kelele jukwaani bila sera ... Mungu akusaidie
 
Na supreme leader akiwa ndio kinara ,al in all CCM itaendelea kutawala nendeni tuu furahisha mkaujaze uwanja.
 
Wakiona moto umezidi wataifungia tena hii mikutano.
Wamepanga watu wa kuja kufanya vurugu kwenye mikutano yetu ili ionekane kuwa mikutano hiyo ni chanzo cha uvunjifu wa amani ili waifungie tena na mleta uzi huu ni mmoja wa uvccm ambao wana Kadi na nguo bandia za Chadema.
 
Na supreme leader akiwa ndio kinara ,al in all CCM itaendelea kutawala nendeni tuu furahisha mkaujaze uwanja.
Kwa watu wasio na akili kama wewe lazima uamini hivyo maaana bila watu kama nyinyi ccm ingeshakufa
 
Wamepanga watu wa kuja kufanya vurugu kwenye mikutano yetu ili ionekane kuwa mikutano hiyo ni chanzo cha uvunjifu wa amani ili waifungie tena na mleta uzi huu ni mmoja wa uvccm ambao wana Kadi na nguo bandia za Chadema.
Upo sahihi maana huyo mtu alishafukuzwa cdm kipindi kirefu sana
 
siipendi ccm lakini chadema hamtakuja kutawala nchi hii milele ccm itaendelea kutawala watakuja watu wazuri kama makufuli na kututawala
 
chadema ukabila na udini ndio umejaa huko sikubali kutawaliwa na chadema bora aje mkoloni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…