Nimepata ajira wife ameongeza matumizi ya pesa zaidi ya mara mbili

mkuu nami pia naomba wadau na wewe mnishauri
Nilipopata kazi ya kuuza bucha kwa muhindi.. Mke wangu mama p akaanza mbwembwe mara anunue kijola halafu aende kwenye kigodoro. Mara anunue kitimoto kilo 2 mixer Safari lager na K vant aka kifutio,
Nikaacha kazi kwa muhindi na kuanza kuuza samaki, hapo ndipo akaanza kunipelekesha baada ya yeye kuchaguliwa mwenyekiti wa vikoba,

Mara anataka kisigino cha kuku mwenye mdonde, mara samaki mwenye matege, sasa ntampata wapi jamani, hata kunanii tu anasema tufanye muda wa wimbo wa taifa..
naombeni chama cha kutetea haki za wanaume mnisaidie.
 
Habarini wapendwa, nimeona watu kadhaa wamekuwa waki share kadhia anuai katika jamvi hili na ushauri mzuri umekuwa ukitolewa ambao nadhani umekuwa msaada kwao.
Ulipokosea ni mkeo kujuwa mshaara wako nikosa sana, hata kama mna pendana sana na mnaaminiana kuna vitu vingine mkeo hatakiwi kuvifaham kabisa, chakufanya kaa na mkeo kitako umweleze nia na malengo yako anapaswa kujuwa kuwa mnatakiwa kujibana ili mfanye maendeleo
 
Daaah nimecheka kwa sauti itabidi tuanzishe chama Cha kutetea haki za wanaume yaaan hatupoi[emoji86][emoji87][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji1241]
 
Kwani huoni hata 'mama' alivyoongeza matumizi baada ya kuonyeshwa kibubu alichokuwa anakusanyia 'baba'
Daaah jamani ebu acheni hizo yaaan sio kwa kufurahisha huku kwa maoni mnayotoa humu mnasababisha nicheke kwa sauti Kuna watu mna vipaji vya kufurahisha.Ila wanaume tunaogopa majukumu kumbe ndio maana baadhi yao huogopaga kuoa mapema.,utasikia unaowa lini bado niponipo Kwanza kumbe na kaubahili kanasumbua[emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji86][emoji1241].utani kidogo tu.[emoji3578]
 
Nilikuwa nioe 2025 kupitia maon ya wenye ndoa, matatizo yao na changamoto tukutane 2030 kama hali itaendelea hiv 2035
 
Ukweli maisha yamepanda sana vitu vimekuwa bei juu ila kama unataka kufanya maendeleo mwambie akupigie bajeti ya mwezi mzima kisha wewe angalia katika mshahara wako yaani asitake pesa mpaka mwisho wa mwezi...!! Ikishindikana hapo nunua vitu vyote mchele,unga,sukar,majani ya chai,gesi ao gunia la mkaa,maharagwe kilo 20, Kisha kwa siku acha elfu 3 acheze vicoba
 
Uliona sifa mwenyewe kumuonesha salary slip mkeo [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Take this advice we mwanandoa mchanga
 
Mpige chini
Habarini wapendwa, nimeona watu kadhaa wamekuwa waki share kadhia anuai katika jamvi hili na ushauri mzuri umekuwa ukitolewa ambao nadhani umekuwa msaada kwao.


Asanteni sana

“Aquila non capit muscas”
 
Habarini wapendwa, nimeona watu kadhaa wamekuwa waki share kadhia anuai katika jamvi hili na ushauri mzuri umekuwa ukitolewa ambao nadhani umekuwa msaada kwao.



“Aquila non capit muscas”
Mkuu hawa wa mama tunapenda ila tuishi nao kwa akili kubwa sana, hakikisha unanua vitu vya mwezi mzima, pia mpe hela ya matumizi yake ya mwezi mmoja
 

SHUKRANI SANA KAKA, NIMEFURAHI SANA KWA USHAURI WAKO MZURI
 

Asante kaka japo duuuh
 
Kwani wakati hana kazi ya ajira walikuwa hawali?

Walikua wanakula elfu5 kwa siku 2yrs ago

Sasa muulize walikua wangapi? Walikua wanakula milo mingapi? Vyakula vilikua bei gani......

Kama kujenga ni bora kuliko kula ajenge tuu, akifa sababu ya kutokula inavyopaswa tunaojua kula tutaishi humo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…