Sijajua unapoushi wewe lakini kama ni familia changa ya watu wawili mfano Morogoro : Mchicha fungu la haja Mia tano fungu mbili buku. Nyama nusu kilo 3500, vitunguu fungu la maana Mia tano, nyanya mia tano, mafuta lita elfu 4 lakini hununui kila siku, mchele kilo elfu moja Mia mbili mpaka Mia nne. Kiukweli elfu 10 ilitakiwa iwe inatosha kabisa. Ushauri wangu ni huu ukipata salary nunua vitu vya jumla vifuatavyo: mchele nenda mashine za kukoboa nunua 50kgs, unga nunua kufuko cha 25kgs, mafuta ya kupika lita tano, ngano ya Azam 5kgs, sukari, chumvi, nazi za pakiti, vitunguu, maharage, dagaa etc... Baada ya hapo mpe pesa kwa matumizi yake binafsi kulingana na kipato chako, na pia pesa ya matumizi madogo ya ndani kama nyama, nyanya etc... Mwisho kaa naye mkubaliane nini malengo yenu kwa huo mwaka na miaka mitano ijayo? Mfano kuanzia Mwaka huu tuanze kufanya serving kwa ajili ya kununua gari au kiwanja au kupata mtoto ili aone umuhimu wa serving na kubana matumizi. Asante.