Nimepata ajira wife ameongeza matumizi ya pesa zaidi ya mara mbili


Umenichekesha sana kiongozi
 
Umenena vyema lakini katika kununua vitu in bulk, usije ukafanya kosa la kununua mafuta ya kula mengi.

Mimi nilikuwa natoka safari nahakikisha nimeleta madumu ya lita 5 kama matano na ninaweka ndani. Baada ya muda ambao hutegemei, unaambiwa mafuta yameisha.

Matumizi mabaya ya mafuta kwenye chakula ni tatizo kubwa kwenye familia zetu, hata umwambie house girl vipi, yeye haelewi.

Usije ukanunua mafuta mengi kwenye nyumba yako. Utauwa familia yako.
 
Sio kweli mchele, unga maaharage hajapanda kihivyo nikupe mfano mimi huwa naagiza mchele kutoka kilombero kilo ni gunia la kilo 100 ni 75,000tsh gharama ya kusafirisha mpaka tazara ni 26,000, Mahindi gunia 25,000 usafiri toka kibaigwa 16,000, huo mchele nitakula zaidi miezi 7 na mahindi ni mwaka mzima na napata na makande hapo
 
Acha ubahili weye!!!
 

Ndugu yangu nimeshajaribu mwarobaini huu, alinipigia hesabu ya mwezi wa kwanza laki 3 na kidogo hivi miezi iliyofuata kiasi hicho hakitoboi na mbaya zaidi tofauti na mwanzoni hataki hata nijue pesa imeotaje mabawa!!!
 
Pole sana na hongera kwa kuajiriwa na kupata mshahara mnono.Kwa issue ya mkeo,nakushauri mwambie ,akupe mchanganuo wa matumizi ya nyumbani kwa siku.Hii itawezekana kwa kupanga ratiba ya chakula kuanzia J3 Hadi.pili,hivyo mtapata matumizi ya wiki then zidisha Mara wiki nne.Vilevile akupigie mahesabu ya matumizi yake binafsi, malipo ya housegiri(Kama yupo) na vitu vingine ambavyo vipo nje ya ratiba ya chakula. Ukishajua kiasi gani kinatumika kwa mwezi ,mpe hiyo hela yote kila mwisho wa mwezi.Kama kutakua na dharula ambayo imeingilia bajeti atakujulisha ili uweze kuisolve.Ukimnunulia vyakula vyote ukaweka ndani kunawezekano tatizo lisiwe solved kwa maana anaweza akavitumia hovyo ,akagawa na hata kuviuza na bado akakwambia kwamba vimeisha hivyo utalazimika kununua vingine hivyo gharama ya matumizi kuwa juu. Mimi familia yangu Ni ya watu wanne,matumizi kwa siku Ni sh.15000/= hii inacover kila kitu except Kodi,umeme ,maji matibabu na Ada ya watoto.
 

Mzee wangu nakushukuru sana kwa ushauri wako, nakuahidi kuufanyia kazi nione nadhani itasaidia. Asante sana
 
Kumbe na wewe unajua kuwa bei ya vitu imepanda plus tozo? Ajabu na kweli!
Miaka2 sio sasa. Umeskia bei ya mafuta ña vyakula ilivyopanda?

Halafu wewe unaweza kuwa mwanaume bahili hadi kwa mkeo kweli!?
 
Reactions: BAK
Kumbe na wewe unajua kuwa bei ya vitu imepanda plus tozo? Ajabu na kweli!

Sasa kwani nani asiyejua bei za vitu hupanda...
Hujui Zamani sh 100 unanunua mchele, unga, mafuta na nyama....?? leo inanunua nini?
 
Mkuu mleta mada, kuwa mkweli ujibu swali la wakuu.

"TATIZO LILIANZIA PALE ULIPOMUONESHA SALARY SLIP"

JE NI KWELI ULIMUONESHA SALARY SLIP??
Uwe muwazi
 
Mkuu mleta mada, kuwa mkweli ujibu swali la wakuu.

"TATIZO LILIANZIA PALE ULIPOMUONESHA SALARY SLIP"

JE NI KWELI ULIMUONESHA SALARY SLIP??
Uwe muwazi

HAPANA MKUU NA WAKUU WENGINE, SEMA NILIVYOPATA TU AJIRA NDANI YA MIEZI 3 NILINUNUA KIWANJA CHA BEI KIASI NA PIA KUNUNUA SAMANI NZURI NA KIFUPI KUBADILISHA MAZINGIRA YA KWETU MIMI NA WIFE, NADHANI HAPO NDIPO ALIPOSHTUKA.
 
Unayafungia unakua unawamiminia kwenye chupa ya lita moja kwisha mchezo
 
Ubahili wa kipuuzi kama huu ndiyo unavunja ndoa. Nyinyi ndiyo wale ME ambao mnaingia jikoni kuhesabu kuna vipande vya nyama vingapi kwenye sufuria.
 
Unayafungia unakua unawamiminia kwenye chupa ya lita moja kwisha mchezo
Baada ya hapo nilijaribu hilo swala, lakini nikaja kugundua hata ufanye nini kama house girl haelewi umuhimu wa kutokuweka mafuta mengi kwenye msosi, yote yanakuwa kazi ya bure.

Onaongea kila siku lakini wapi. Mpaka mama watoto aingie jikoni ndiyo inakuwa furaha yako. Na house girl akishagundua hilo, anakwepa issue ya kupika kwa kumtegea mama watoto apike kila siku. Ni mtihani kwa kweli.
 
Mpaka umeme umepanda!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…