Nimepata ajira wife ameongeza matumizi ya pesa zaidi ya mara mbili

Habarini wapendwa, nimeona watu kadhaa wamekuwa waki share kadhia anuai katika jamvi hili na ushauri mzuri umekuwa ukitolewa ambao nadhani umekuwa msaada kwao.



“Aquila non capit muscas”
Dah....simpo Sana...mwambie akupe bajeti yake ya mahitaji ya nyumbani ya siku....Kisha ya wiki...akiweza hata ya mwezi.....Kama upo Dar..Sunday ingia naye Manzese maduka ya jumla piga shopping Kisha uende Mabibo piga shopping ya wiki nzima....hakikisha umenunua kila kitu....Kisha mpe Kama laki hivi mwambie AIWEKE....utakuja nishukuru 🤣🤣🤣🤭
 
Kwani tuambie ukweli wewe unakinga kias gani kwa mwezi
 
ushauri kuntu, no goals no need to save money...hahahahhahah
Ndugu yangu nimeshajaribu mwarobaini huu, alinipigia hesabu ya mwezi wa kwanza laki 3 na kidogo hivi miezi iliyofuata kiasi hicho hakitoboi na mbaya zaidi tofauti na mwanzoni hataki hata nijue pesa imeotaje mabawa!!!
heee unataka akuambie na bei aliyonunulilia nyanya? mkuu kwa namna hii hutoboi kabsa..,,,nani anapenda hela za kutoa mrejesho kila siku? bora yangu mie ninazo za kwangu
 
nimecheka kwa nguvu kama mazuri, yaani unataka kutuaminisha walio oa hawasemi mshahara kamili kwa wake zao?

mbavu zangu mie loooh
mh...umenitafsiri vibaya....lakini hata nisipo kwambia haiondoi kuwa majukumu ya kulea familia bado yatabaki kwangu..kwahiyo nikwambie mshahala nisikwambie...bado nitakae husika kule familia ni mimi baba
 
iyo tu kutuambia mshahara wako ni mtamu tayari inaonekana shida ni wewe.
 
Hauko pekee yako kwa haya yanayokutokea. Nimekuwa consulted na wana ndoa wengi kwa kesi kama hii. Na hapa ndiyo matatizo ndani ya familia yanapoanzia. Matumizi ya pesa bila mpango, na bila kujali future kisa baba ameajiriwa na ana mshahara ambao kwa kweli si haba.
 
Mpe talaka.
 
Vimepanda baada ya yeye kupata Kazi?

#YNWA
 
Mm wngu anapambana sana kutaka kujua kwenye BZNES zangu naingiza kiasi gani kwa wiki na mwezi. Mpk ameenda kwa dada yake eti analalama.
Kwakua kila jambo ninalo ona la msingi ndio pesa inatoka bila shida. Mambo y ovyo BIG NO
 
Bila kupepesa Macho
Mtoa mada apitie hapa

Nimetaman kujua zaidi [emoji849]
 
Pole sana Mkuu hapo nyumbani kwenu mnaishi watu wangapi jumla?
Mfano mdogo kwangu ni familia ya watu 4.
Budget ya chakula kwa mwezi ni 300,000
Umeme 30,000
Kifurushi azam 28,000
Maji 15,000
Mshahara wa mfanyakazi 50,000
Jumla 423,000

Kaa nae chini mpige mahesabu ya vitu vyote muhimu kwa mwezi mzima. Mimi hua nanunua kila kitu kinakua ndani, kuanzia mchele,mafuta,dagaa,maharagwe chumvi,sukari,nyama,samaki,viungo vyote ndani. Na hua vinapitiliza mwezi nimetenga na ratiba kabisaa.
 
Fanya shopping ya mwezi mzima nunua vile vitu muhimu jaza home, hii inasaidia sana
 

Asante sana kaka kwa ushauri mzuri, home yupo wife, house girl na firstborn ambaye hajaanza bado kula. Mimi nipo mbali kiutafutaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…